Je, huku ndiko kuokoka?

Je, huku ndiko kuokoka?

Nafaka

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
12,157
Reaction score
31,334
Kuna ndugu yangu flani huu ni mwaka wa tatu anadai ameokoka, anasali sana, anafunga sana. Lakini tatizo langu kwake ni kwamba anajitenga na watu kasoro familia na marafiki wa karibu wa huyo anayedai ni mama wake wa kiroho. Ila waliobaki anasema ni wachawi. Story zake kila siku anasema wamempiga flani katika maombi, yani story zake ni za kuwapiga watu katika maombi tu.

Mara fulani kafa ile ajali ilikuwa imetegeshewa sisi ili Mungu katuokoa ikampata fulani. Kuna kipindi alipkuwa anaiona anasema oooh mara sijui ndugu yetu gani alikuwa kanifuata ananiroga basi anaanza kuniombea nanivuta nywele na masikio.

Nikaona isiwe tabu nikawa simtembelei sana. Yani kila failure ya maisha yake anasema karogwa japo mambo mengi kafail kwa kutofuata ushauri na kufanya kama inavyotakiwa.

Sasa jana tumekorofishana baada ya kuniambia kuwa sijui mwanangu karogwa, anahitaji kuombewa nitoe sadaka awekewe wakifu eti anadai wakati wanasali na mama yake wa kiroho wameambiwa hivyo na Mungu.

Ikabidi nijaribu kumwelewesha kwamba, mimi mambo yake mengi siyaamini. Nikamwambia kajitenga na kila rafiki yake kwasababu ya kuamini kila mtu mchawi, hadi mijusi anaiua anasema inatumwa na wachawi wanaitumia kupeleleza.

nikajaribu kureason naye nikamwambia mimi naona failure ya maisha yake nyingi zimetokana na yeye mwenyewe ajifunze kutokana na makosa kuliko kutafuta scapegoat.

Kuna kipindi kila mara alikuwa anaanguka akiwa anaomba eti roho mtakatifu amempanda anasema kuongea na kutoa utabiri ambao kwa maono yangu haukuwahi kutokea. Nikamwambia kipindi hicho nilianza kuwa na mashaka kuwa huenda kapata tatizo la kisaikolojia.

Nilivyo mwambia hivyo akasema Mungu anisamehe akanikatia simu. Nimebaki ninasikitika muda mwingine ninawaza au mimi ndiye nimepotoka nina imani haba. Maana mimi naona anapotea anatumia muda mwingi akiomba saana pasipo kujishughulisha wala kuwaza atatokaje.
 
Biblia inasema katika hosea 4:6

My people are destroyed for lack of knowledge: because thou hast rejected knowledge,

Huyo boya hajielewi biblia yenyewe inawashangaa kinoma.
 
aisee kumbe watu wa hivyo wapo wengi me nilijua ni ndugu yangu tu ndo ako na matatizo ya hivyo yaani copyright kabisaa na huyo... kaah nimecheka mie

Sent using Jamii Forums mobile app
Umemsaidiaje maana yani sijui hata nimsaidieje yani... huyo anayemwita mamake wa kiroho ana mtoto wa kike ni hustler sana yani mtafutaji hakai kusali tu akisubiri Mungu amletee tu bila kujishughulisha. Lakini ndugu yangu yeye muda wowote anaitwa na huyo mama wa kiroho yani muda wowote anampelekesha
 
Kweli wajinga ndio waliwao.
Mtu wa hvyo unakuta hajishughulishi wala kufanya kazi na kila anachopata anampelekea huyo mama wa kiroho.
Msaada mkubwa ambao unaweza mpatia ni kumuombea tu Mungu atambadilisha mwenyew, wanakuaga wabishi sana hao watu na hawapokei ushauri wa yoyote zaidi ya wapendwa wenzake.
 
Wahi kitanda Milembe. Soon ataanza kujiita nabii mara askofu. Kaa chonjo. Watu wengi wamechanganyikiwa wanadhani wakiingia hizi dini za wasaka tonge watapona. Milembe, Bugando au Muhimbili basi.
 
Mkuu mpeleke akapimwe kichaa aanze dozi mapema.
 
Umemsaidiaje maana yani sijui hata nimsaidieje yani... huyo anayemwita mamake wa kiroho ana mtoto wa kike ni hustler sana yani mtafutaji hakai kusali tu akisubiri Mungu amletee tu bila kujishughulisha. Lakini ndugu yangu yeye muda wowote anaitwa na huyo mama wa kiroho yani muda wowote anampelekesha
Hatujamsaidia chochote maana Kama ni kumshauri mnaweza mkabishana siku nzima na kuishia kununiana,kwahiyo tunamuachia Mungu amfungue akili...Hayo yanakuwaga ni mapepo huenda ndugu yako ana mapepo maana siye huyu tunaonaga Kama hayupo sawa kabisaa,ni mwajiriwa ila Kuna kipindi alitaka aache kazi akidai anarogwa huko kazini..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
endelea na mambo yako acha kumfuatilia mwamume mwenzako kihivyo
wewe unamuona hayuko sawa ,na yeye itakuwa hivyo hivyo hamtafikia mwafaka
 
Kuna ndugu yangu flani huu ni mwaka wa tatu anadai ameokoka, anasali sana, anafunga sana. Lakini tatizo langu kwake ni kwamba anajitenga na watu kasoro familia na marafiki wa karibu wa huyo anayedai ni mama wake wa kiroho. Ila waliobaki anasema ni wachawi. Story zake kila siku anasema wamempiga flani katika maombi, yani story zake ni za kuwapiga watu katika maombi tu.

Mara fulani kafa ile ajali ilikuwa imetegeshewa sisi ili Mungu katuokoa ikampata fulani. Kuna kipindi alipkuwa anaiona anasema oooh mara sijui ndugu yetu gani alikuwa kanifuata ananiroga basi anaanza kuniombea nanivuta nywele na masikio.

Nikaona isiwe tabu nikawa simtembelei sana. Yani kila failure ya maisha yake anasema karogwa japo mambo mengi kafail kwa kutofuata ushauri na kufanya kama inavyotakiwa.

Sasa jana tumekorofishana baada ya kuniambia kuwa sijui mwanangu karogwa, anahitaji kuombewa nitoe sadaka awekewe wakifu eti anadai wakati wanasali na mama yake wa kiroho wameambiwa hivyo na Mungu.

Ikabidi nijaribu kumwelewesha kwamba, mimi mambo yake mengi siyaamini. Nikamwambia kajitenga na kila rafiki yake kwasababu ya kuamini kila mtu mchawi, hadi mijusi anaiua anasema inatumwa na wachawi wanaitumia kupeleleza.

nikajaribu kureason naye nikamwambia mimi naona failure ya maisha yake nyingi zimetokana na yeye mwenyewe ajifunze kutokana na makosa kuliko kutafuta scapegoat.

Kuna kipindi kila mara alikuwa anaanguka akiwa anaomba eti roho mtakatifu amempanda anasema kuongea na kutoa utabiri ambao kwa maono yangu haukuwahi kutokea. Nikamwambia kipindi hicho nilianza kuwa na mashaka kuwa huenda kapata tatizo la kisaikolojia.

Nilivyo mwambia hivyo akasema Mungu anisamehe akanikatia simu. Nimebaki ninasikitika muda mwingine ninawaza au mimi ndiye nimepotoka nina imani haba. Maana mimi naona anapotea anatumia muda mwingi akiomba saana pasipo kujishughulisha wala kuwaza atatokaje.
Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom