Faida wanayoipata makampuni makubwa ya mtandaoni Kama vile Facebook, Google, YouTube, Twitter, N.k. faida inatokana na matangazo(ads)yanayopatikana kwenye website husika mf. Unapoangalia video YouTube kunatangazo linatokea mwanzo, katikati, mwisho mwa video basi kilo tangazo ndio faida ya YouTube pamoja na mwenye channel husika aliyepakiza hiyo video kwenye YouTube wanagawana kwa asilimia (mwenye channel I anachukua 55% na YouTube ambayo inamilikiwa na Google wanabakiwa na 45%) hata Google ni hivyohivyo wanatumia Google adsence ambapo hata wewe Kama una website ambayo inakidhi vigezo na masharti ya Google adsence unaweza ukaomba matangazo na mkagawana faida.
Kwa Facebook na Instagram faida ya matangazo inachukuliwa na kampuni 100%.
Kwa WhatsApp bado sijajua faida anapata upande gani lakini magunduzi wa WhatsApp wale jamaa wawili walikuwa na lengo la kutokuweka matagazo kwenye app yao lengo lao liliendelea Hadi iliponunuliwa WhatsApp kwa $16 billion na kampuni la Facebook ndipo bwana Mark (mmiliki wa Facebook, Instagram na WhatsApp) akaamua kuja na mpango wa matangazo na mwaka 2020 matagazo yataanza kuonekana kwenye app ya WhatsApp upande wa status. Ndio sababu ya GB WhatsApp, Yo WhatsApp na FM WhatsApp kufutwa rasimi ili WhatsApp orginal ije na matangazo na kuongeza faida.