Je hili ni sawa halmashauri ya wilaya ya meru?. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je hili ni sawa halmashauri ya wilaya ya meru?.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Chilli, Feb 14, 2012.

 1. Chilli

  Chilli JF-Expert Member

  #1
  Feb 14, 2012
  Joined: Jul 17, 2011
  Messages: 1,638
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Nimekua ndani ya wilaya hii ya Meru kwa muda sasa nikijaribu kuangalia hali halisi ya maisha ya kila siku ya ndugu zangu Wameru lakini kuna jambo lililonishangaza na kunikera sana.
  Jambo lenyewe ni kuwepo kwa kizuizi katika barabara ya kutoka Kikatiti kwenda maeneo ya Sakila. Kizuizi hiki ambacho kimewekwa kwenye barabara hii mbovu ya vumbi na vilima kimewekwa na uongozi wa kijiji kimojawapo katika barabara hiyo kikiwa na lengo cha kuwatoza watumiaji wa barabara hiyo ushuru wa shilingi mia tano (500 tsh) kwa kila safari unayopita kwa gari na 200 kwa pikipiki.
  Nilipofatilia niliambiwa kwamba kuna watu walijitolea kutengeneza barabara hiyo (ingawa kiukweli naona imechimbwachimbwa tu) hivyo uongozi wa kjiji ukawaruhusu kuweke kizuizi hicho cha miti na mawe ili wajilipe. Na cha kushangaza zaidi ni kwamba kizuizi hiki huwekwa siku ya Jumanne na Ijumaa ambazo ni siku za soko.
  Swali nililojiuliza ni Je, hili jambo ni sawa kisheria? Halafu, jukumu la kutengeneza barabara ni la nani? Mamlaka ya watu kuchimbachimba barabara kisha kutoza wananchi wengine gharama za kutengeneza, kwa lazima yanatoka wapi?
  Kwa faida ya wengi, eneo hili lipo ndani ya jimbo la Arumeru Mashariki lililokua la Marehemu Jeremiah Sumari (RIP).
   
 2. SOBY

  SOBY JF-Expert Member

  #2
  Feb 14, 2012
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 1,265
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Sioni cha kushangaza hapo.
   
 3. Chilli

  Chilli JF-Expert Member

  #3
  Feb 14, 2012
  Joined: Jul 17, 2011
  Messages: 1,638
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Sikushangai.
   
Loading...