Je, Hili nalo lina Ukweli....?

ukiona wee ndio unawekeza sana unaanza kukata tamaa pole pole mwishowe waweza tema mzigo hivi hivi.

Afu ukutane na mtu mgumu 'kurenew statement'
yaani alivyokuambia anakupenda siku mnatongozana ndo basi tena hatakaa arudie kusema neno hilo.

Kama hukumrekodi kipindi cha matongozo ili uwe unajikumbushia imekula kwako.
Kongosho katika maisha ya mahusiano hasa yanapofikia hatua ya kuzoeana sana kuna vitabia huwa vinaondoka na vingine vina develope ambavyo tena vinakuwa na ladha nzuri kuliko yale maneno ya mahaba mliyokuwa mnaambiana wakati mnatongozana.

mathalani watu wengi sana kadiri mahusian yanavyozidi kukua ndivyo wanavyokuwa marafiki na hawa kwao maisha ya kuambiana i love you yanaapungua yanabaki maisha ya kuambiana kirafiki tena wengine hata kwa kutumia lugha za matusi wakati wanaongea.

mfano waweza "kusema baba fulani urudi mapema leo nataka kit...o na akacheka akajibu mshkaji huchoki?"........ na anarudi mapema na mchezo anakupa. sasa katika zingira kama hilo utahesabu nini? yaani sielewi mtu anayeanza kuhesabu anatendewa nini kwenye mahusiano unless ni begginers.
 
Last edited by a moderator:
dah, viashiria ni vingi ila kimoja wapo ni ukaribu kati yenu unaongezeka au unapungua?

Nshaanza konyagi sina nguvu ya kusema zaidi hapa labda kesho.

sasa hapo ndipo mnapokosea jamani au nisiseme unakosea nikuongeze swali la pili hapo hapo ukaribu kama friends ama kama mke na mume ama kama gf na bf?
 
Once again, the phenomenon of love!
Tena
From the mighty and legend of love Ms MwanajamiiOne.... Nlichoipendea hii thread kila anachocomment Mj1 anaweka na umombo kiduchu ili aeleweke vizuri. Penzi la kiafrika bila kaneno kakiinglish huwa halinogi asee. Ndo maana mpk leo sijapata sentensi bora ya kutohoa "I MISS YOU"
 
Last edited by a moderator:
gfsonwin, najua kuambizana 'i love you' kwa mahusiano ya muda mrefu huwa si mara kwa mara.

Pamoja na kuwa mahusiano ya muda mrefu 'bond' inazidi kuwa na nguvu.

But on occasions mwenza akirudi na kurenew statement ina raha yake hata kama ni mara moja kwa mwaka au miaka miwili.

Hasa anapokuwa anammanisha na wala hujaomba ila imetoka moyoni mwake.
 
Last edited by a moderator:
ukaribu kama mke na mme au bf na gf.
Kama badala ya kuongezeka unapungua basi hapo pana ???

Lakini achia mbali wapenzi, hata marafiki wa kawaida ipo hiyo. 'mii kila siku naanza kumpigia saa hivi sipigi tena'
wote mkijikuta mnawaza hivi urafiki unakufa lakini hii ipo sana tu.

sasa hapo ndipo mnapokosea jamani au nisiseme unakosea nikuongeze swali la pili hapo hapo ukaribu kama friends ama kama mke na mume ama kama gf na bf?
 
gfsonwin, najua kuambizana 'i love you' kwa mahusiano ya muda mrefu huwa si mara kwa mara.

Pamoja na kuwa mahusiano ya muda mrefu 'bond' inazidi kuwa na nguvu.

But on occasions mwenza akirudi na kurenew statement ina raha yake hata kama ni mara moja kwa mwaka au miaka miwili.

Hasa anapokuwa anammanisha na wala hujaomba ila imetoka moyoni mwake.

hili silipingi Kongosho but unaonaje mtu anapochukulia kama ndiyo indicator ya penzi kukua ama kufa? je mtu kama huyu ambaye ataambiwa mara moja kwa mwaka aseme mapenzi hayakui? ama kwakuwa yeye huwa analisema kila mara basi ionekane kama penzi limekuwa ndani yake?
 
Last edited by a moderator:
Nna miaka 11 ya ndoa. Huyu wifey leo akachanganyikiwa akanambia I LOVE YOU, kiukweli ntampa za uso.... LOVE YOUR BOSS. For Christ's sake najua wanipenda ndo maana uko nami na wanivulia shupi lako. Twende kimatendo zaidi si kimaneno kama vikina Matesha. Na matendo hapa namaanisha ni fiftyfifty kwenye kuprovide malovee. Mna bahati leo sijalewa. Nyambaf.
 
ukaribu kama mke na mme au bf na gf.
Kama badala ya kuongezeka unapungua basi hapo pana ???

Lakini achia mbali wapenzi, hata marafiki wa kawaida ipo hiyo. 'mii kila siku naanza kumpigia saa hivi sipigi tena'
wote mkijikuta mnawaza hivi urafiki unakufa lakini hii ipo sana tu.

sasa Kongosho iko hivi katika everlasting relationships, uliza mtu yeyote atakwambia ule ukaribu kama mke na mume unapungua na unajengeka urafiki ambao mwenzi wako ndiye kila kitu kwako na ni msiri wako. Tena kama ukaribu kama mme na mke ukiongezeka kunahatari ya kuweka gap inbetween ambayo mmoja hatakuwa free na mwenzie matokeo yake ni mahusiano yenye nidhamu za woga. siku zote maisha ya kuwa mwenza wa mtu yanatakiwa yajengeke katika misingi ya urafiki na hii itaongeza uhuru na imani juu ya mwenzi wako.
 
Last edited by a moderator:
Nna miaka 11 ya ndoa. Huyu wifey leo akachanganyikiwa akanambia I LOVE YOU, kiukweli ntampa za uso.... LOVE YOUR BOSS. For Christ's sake najua wanipenda ndo maana uko nami na wanivulia shupi lako. Twende kimatendo zaidi si kimaneno kama vikina Matesha. Na matendo hapa namaanisha ni fiftyfifty kwenye kuprovide malovee. Mna bahati leo sijalewa. Nyambaf.

nilikuwa nasoma hii coment yako toka chini kwenda juu nikajisemea huyu ni Asprin sasa bado ikaning'adua mbona sign yake haipo? ikabidi ni scrow up nikakukuta lol!......... hebu wape shule wajukuu zako na kwakua hujanywa leo najua utamwaga mistari ya heshima haya twende kazini.
 
Last edited by a moderator:
Nenda kwenye biblia majibu yako wazi: UPENDO huvumilia yote, huamini yote, hutumaini yote, hustahimili yote, upendo haupungui. Upendo hautafakari, upendo hauna kipimo. Hivyo kwa vipimo unavyoweka ni wazi huo si upendo kwa maana ya LOVE bali ni mahusiano kwa maana ya SEX AFFAIRS
 
ndo maana nilisema viashiria vya penzi kukuwa ni ukaribu au 'bond' kati ya wahusika.

Hiki nachosema hapa ni kionjo tu lakini si kipimo cha penzi kukua ama kupungua.

Ntadadavua zaidi kesho leo nshaonja na uvivu wa kushugulisha akili ninao.

But kurenew statement kama kionjo ina raha yake lakini mtu hata asiporenew sivunji mahusiano.

hili silipingi Kongosho but unaonaje mtu anapochukulia kama ndiyo indicator ya penzi kukua ama kufa? je mtu kama huyu ambaye ataambiwa mara moja kwa mwaka aseme mapenzi hayakui? ama kwakuwa yeye huwa analisema kila mara basi ionekane kama penzi limekuwa ndani yake?
 
Last edited by a moderator:
ndo maana nilisema viashiria vya penzi kukuwa ni ukaribu au 'bond' kati ya wahusika.

Hiki nachosema hapa ni kionjo tu lakini si kipimo cha penzi kukua ama kupungua.

Ntadadavua zaidi kesho leo nshaonja na uvivu wa kushugulisha akili ninao.

But kurenew statement kama kionjo ina raha yake lakini mtu hata asiporenew sivunji mahusiano.

ok pumzika ila kesho nina wewe hadi nipate majibu hapa
 
Umesema vema Kongosho......mara nyingi sana hivi viuchunguzi vikianza na mapenzi huanza kulega lega hapo hapo.....unajiuliza na kujijibu mwenyewe mwisho wa siku unapunguza kumsalimia/kumjulia hali mwenzi wako.....mimi naona kama umeamua kufanya fanya bila kutegemea chochote!

Lakini mpaka uanze viuchunguzi hivyo nini huwa kinapelekea? Si kwa kuwa unaona mwenzi wako amebadilika kiana kiasi cha wewe kuanza kujiuliza maswali? Na once ukishaanza kujiuliza ndo tunaambiwa unakaribisha problems kwa relationship yako sasa je tusijiuliza hata tukiona mabadiliko?
 
mmh, sasa kwenye mahusiano mapya napo mtu anakuwa kabadilika nini wakati ndo kwanza mnaanza?

Mie hiki hukiita kihoro cha mapenzi, kwa ufupi hakina maana sana huvuruga.

Afu kama vile umeleta hii mada muda muafaka kweli, basi tu.

Lakini mpaka uanze viuchunguzi hivyo nini huwa kinapelekea? Si kwa kuwa unaona mwenzi wako amebadilika kiana kiasi cha wewe kuanza kujiuliza maswali? Na once ukishaanza kujiuliza ndo tunaambiwa unakaribisha problems kwa relationship yako sasa je tusijiuliza hata tukiona mabadiliko?
 
Mdogo wangu MJ1,

Enzi zetu kila mtu alikuwa anatimiza wajibu wake, kuanzia shambani hadi kwa room.....Hatukuwa na mambo ya maneno maneno na longo longo.....Hizi technology zenu zitawamaliza na pressure!

Bibi ataachaje kujua nampenda 99.999% wakati matenga ya matunda hayaishi ndani na magunia ya mkaa hayashuki nusu, ...achia mbali kujituma kwenye kutelekeza amri ya kuijaza dunia??

Nawashauri hivi...Just be yourself and give whatever you can to keep your love!! Ikishindikana hapo...basi chapa lapa mapema.....Nimeeleweka??

Babu DC!!
 
Lakini mpaka uanze viuchunguzi hivyo nini huwa kinapelekea? Si kwa kuwa unaona mwenzi wako amebadilika kiana kiasi cha wewe kuanza kujiuliza maswali? Na once ukishaanza kujiuliza ndo tunaambiwa unakaribisha problems kwa relationship yako sasa je tusijiuliza hata tukiona mabadiliko?

This question is very genuine, lakini before answering it let me ask you first do you normally pile up things in yourself?
 
jamani mmh.......! sijui ni kwasababu miye nishakuwa zilipendwa ama lakni ngoja niseme tu manake wanasema utuuzima dawa ingaa jalala pia.

Kwanza kabisa naoma sweetlady na Kaunga na Kongosho na MwanajamiiOne muelewe hivi na ndivyo ilivyo kwangu katika maisha mtu hupaswi kuangalia wema unaotendewa au ubaya bali unapaswa kuangalia wewe ni nini wajibu wako juu ya mtu mwingine. hii inanifanyaga miye niseme " it is not that water which i drink matters, but which i spill through" sina maana ya kusema tenda wema nenda zako la hasha bali nina maana kwamba kila kujitoa kulko kwema kwa mwenzi wako ni njia ya kuelekea mema ya mwenzi wako.

kamwe usiangalie mwenzi anatenda mangapi juu yako bali angalia wewe wajibu wako ni nini ili uelekee mema ya mwenzi wako.sijui vijan wa siku hizi nati gani zimechomoka ukicompare na siye BBC manake they are too theoretical and they have a lot of theories ambazo ni hypothetical. na mwisho wa yote ni mafundisho ya kukata tamaa kiasi kwamba ibilisi naye anapata pa kujishika lolest. Mimi niwashauri wadogo zangu ninyi wa moyoni msiishi kwa shuhuda za kushindwa jamani, mbona dunia ni njema sana na ina wema wote? hivi kwanini Mungu ampe fulan ndoa njema halafu wewe akupe mbaya wajkati alisha sema? yeye ajipatiaye mke apata kitu chema so wewe ni mwema kwa mumeo?

kwanini mnaaminishana katika maisha yenye upande mbaya tu ambapo sasa iblisi naye analiangalia na kutushtakia hili kwa Mungu? acheni haya bwana hebu tukiri wema halafu tumwambie Mungu aliye asili ya yote uone kama hatawapa yaliyo mema? vilima vipo na mabonde yapo katika maisha ila si kwa extent ambayo tunaiweka jamani ina maana Mungu aliumba watu tusifurahie maisha ya ndoa kabisa ama alitupa kitu ambacho hakuwa na uhakika nacho? nisameheni tu jamani ni uzee tu yawezekana kabisa ushamba wangu ndio unaonisumbua msinizodoe jamani.

.......Nakubaliana na wewe gfsonwin si vema kuchunguza mwenzio amekutendea yepi mazuri kulinganisha na wewe ulivyotenda but kwa hali ya ubinaadamu na maisha ya mahusiano mengi kwa wakati wa sasa kweli utavumilia kuona kuwa unamjali mtu ambaye unahisi ana mambo mingi zaidi ya wewe? (tukumbuke kuwa siku hizi hata busara ya ku'yahandle' hayo mambo mingi kisiri pasipo kumuumiza mwenzi wako imetupita kisogoni, kuna kujisahau, kuna kupitiwa na kunogewa na kazi za nje zaidi ya mwenzi wako (Kwa wale ambao wana hizo mambo). Sasa suppose una mtu wa hivi kanogewa na kujikuta unknowingly anapoteza uelekeo, wewe kutwa kucha unambebea mbelekoni kwenye kaniki yenye maandisho yasoonekana yasemayo in the name of LOVE!

Aisee analyses katika maisha ya hivi haiepukiki aisee. Mimi hata siwaelewi wazungu huwa na maana gani wakiandikaga makitu yao!
 
This question is very genuine, lakini before answering it let me ask you first do you normally pile up things in yourself?

............ Unfortunately yes I used to ingawa nowdays ninajitahidi ku'cheua' ila siwezijisifia kuwa nimefuzu itakikanavyo
 
ukiona wee ndio unawekeza sana unaanza kukata tamaa pole pole mwishowe waweza tema mzigo hivi hivi.

Afu ukutane na mtu mgumu 'kurenew statement'
yaani alivyokuambia anakupenda siku mnatongozana ndo basi tena hatakaa arudie kusema neno hilo.

Kama hukumrekodi kipindi cha matongozo ili uwe unajikumbushia imekula kwako.

Hhahahaha Kongosho lol .....kuna watu ni wagumu ati
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom