Je, Hili linaukweli kwa kiasi gani?

Je, Hili linaukweli kwa kiasi gani?

mapipando

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2015
Posts
2,922
Reaction score
3,563
Heshima kwenu wakuu,

Kuna jamaa hapa kazini alikuwa anazungumzia mambo kadha wa kadha kuhusu mahusiano.Jambo moja kati ya hayo limenifanya kulipa uzito wake na kuona ni vyema nikalifikisha hapa angalau lijadiliwe kwa mapana yake.

Amesema hivi,mtu yeyote ambaye tarehe yake ya kuzaliwa ni tasa, mtu huyo kamwe hatadumu kwenye ndoa yake kama ataoa ama kuolewa na mtu ambaye tarehe yake ya kuzaliwa pia ni tasa. Ikiwa sababu moja kubwa ni kwamba watu wa namna hiyo huwa siku zote wanapenda kuwa juu na wababe hata kama wamekosa.

Kaenda mbali zaidi na kusema kuwa amefanya utafiti hasa katika ndoa zilizovunjika na zile zenye migogoro mikubwa na kugundua kuwa watu hao tarehe zao za kuzaliwa ni tasa.

Nini mtazamo na uelewa wako juu ya hili?
Karibuni tujadiliane pengine tutapata ufumbuzi wa matatizo ya kuvunjika kwa mahusiano/ndoa.
 
  • Thanks
Reactions: THT
Heshima kwenu wakuu,

Kuna jamaa hapa kazini alikuwa anazungumzia mambo kadha wa kadha kuhusu mahusiano.Jambo moja kati ya hayo limenifanya kulipa uzito wake na kuona ni vyema nikalifikisha hapa angalau lijadiliwe kwa mapana yake.

Amesema hivi,mtu yeyote ambaye tarehe yake ya kuzaliwa ni tasa,mtu huyo kamwe hatadumu kwenye ndoa yake kama ataoa ama kuolewa na mtu ambaye tarehe yake ya kuzaliwa pia ni tasa. Ikiwa sababu moja kubwa ni kwamba watu wa namna hiyo huwa siku zote wanapenda kuwa juu na wababe hata kama wamekosa.

Kaenda mbali zaidi na kusema kuwa amefanya utafiti hasa katika ndoa zilizovunjika na zile zenye migogoro mikubwa na kugundua kuwa watu hao tarehe zao za kuzaliwa ni tasa.

Nini mtazamo na uelewa wako juu ya hili?
Karibuni tujadiliane pengine tutapata ufumbuzi wa matatizo ya kuvunjika kwa mahusiano/ndoa.
FALLACY.....Hamna ukweli wowote mkuu wazazi wangu wote wamezaliwa kwenye tarehe tasa, ila wana heshimina balaa...wanapendana sana...Nawaombea wadumu na mioyo hiyo.
 
Tatizo kubwa la ndoa kuvunjika, ni watu kutojua wajibu wake katika maisha ya ndoa.

Binafsi mimi na mama chanja tarehe moja kasoro miezi tu.
 
Tatizo kubwa la ndoa mpaka kuelekea watu kutengana, ni watu kutojua wajibu na nini hasa kipaumbele chao katika maisha ya ndoa.
 
FALLACY.....Hamna ukweli wowote mkuu wazazi wangu wote wamezaliwa kwenye tarehe tasa, ila wana heshimina balaa...wanapendana sana...Nawaombea wadumu na mioyo hiyo.
Angalau wewe umekuja na hoja ya kuipinga hii dhana.
Lakini umejaribu kuangalia kwa mapana zaidi ama umewaangalia wazazi tu?
 
  • Thanks
Reactions: THT
Ndoa hujengwa kwa upendo, uvumilivu, maelewano na msamaha hayo ya tarehe Hanna kitu kama hicho
 
Angalau wewe umekuja na hoja ya kuipinga hii dhana.
Lakini umejaribu kuangalia kwa mapana zaidi ama umewaangalia wazazi tu?
Hapo amna ukweli, migororo kwenye ndoa yaweza kusababishwa na chochote....Kwa mfano wewe na mkeo muwe mmezaliwa tarehe tofauti na tasa, then mkeo abebe mimba ya boya mwingine(sikuombei yakupate) hauta react???
 
Nikwel kabisaa na evidence ninazo
 
Wapo wanao amini kwamba tabia za binadamu zinauhusiano flani na tarehe zao za kuzaliwa if u learn about astrology. Kwa mfano kuna watu wanapenda sana madaraka, wengine wivu sana, wengine wapole n.k hivyo basi inaweza kuwa na uhusiano kwa sababu mtu ana husisha general characters na experience aliyonayo. ila hiyo elimu inasaidia tu kujua kwanini vitu vinatokea, ukisha mjua mwenzio anatabia gani na wewe unatabia gani, ni uamuzi wenu tu nani ajishushe ili muweze kuishi.
 
Hapo amna ukweli, migororo kwenye ndoa yaweza kusababishwa na chochote....Kwa mfano wewe na mkeo muwe mmezaliwa tarehe tofauti na tasa, then mkeo abebe mimba ya boya mwingine(sikuombei yakupate) hauta react???
Kweli nita-over-re-act,na ni kweli haya mambo hutokea kwa hata wasozaliwa kwenye tarehe tasa,jambo kubwa hapa ni kwa kiwango kipi wenye tarehe tasa na waso na tarehe watofautiana katika kuachana ama migogoro?
 
Wapo wanao amini kwamba tabia za binadamu zinauhusiano flani na tarehe zao za kuzaliwa if u learn about astrology. Kwa mfano kuna watu wanapenda sana madaraka, wengine wivu sana, wengine wapole n.k hivyo basi inaweza kuwa na uhusiano kwa sababu mtu ana husisha general characters na experience aliyonayo. ila hiyo elimu inasaidia tu kujua kwanini vitu vinatokea, ukisha mjua mwenzio anatabia gani na wewe unatabia gani, ni uamuzi wenu tu nani ajishushe ili muweze kuishi.
Umesema vyema mkuu, na hiyo ndio SILAHA KUU ya kulinda ndoa/mahusiano.
 
Back
Top Bottom