Je, hili la TANESCO siyo "utapeli"?

Je, hili la TANESCO siyo "utapeli"?

Hashim bin Faustin

Senior Member
Joined
Jan 30, 2017
Posts
177
Reaction score
216
Ndugu wadau,

Kuna jambo linanitatiza katika mpangilio wa ufanyaji biashara wa hili shirika la umeme TANESCO. Mimi nahitaji kuunganishiwa umeme katika nyumba yangu umeme ambao nitakuwa naulipia kwa kadiri ya matumizi yangu. Lakini ninakerwa na huu utaratibu wa malipo ya vifaa vya kuunganishiwa umeme.

Kwa mfano natakiwa nilipie nguzo kadhaa, waya mita kadhaa, Transformer, na kadhalika jumla ya ngarama naambia ni Tshs Mil. 15, eti kwa ajili ya kuweka miundombinu ya kufikisha umeme ndani ya nyumba yangu. Lakini cha kushangaza baada ya kulipia vifaa hivi kwa Mil 15, vifaa husika vinageuzwa kuwa mali ya TANESCO Bila mimi muhusika kufahamishwa au kuombwa na Shirika hili.

Kupitia miundo mbinu hii niliyo nunua kwa pesa zangu za kudunduliza na mikopo, utaona TANESCO wakianza kuunganishia umeme watu wengine jirani yangu kwa bei nafuu bila kuulizwa au kuombwa na wahusika. Je hii ni haki? Shirika kujinufaisha kupitia mpango huu! Au kwa kuwa ni Shirika la Serikali linafanya litakavyo?

Je kujenga miundombinu ya umeme ni kazi ya mlaji au ni kazi ya msambazaji?
 
Mkuu wala hujatapeliwa, watu wengi wavivu kusoma terms and conditions,

Miundo mbinu yote ya TANESCO ambayo umelipia haijalishi thamani yake bado vitabaki kuwa vyao. Hilo limeainishwa wazi kabisa bila kificho.

Wakati mwingine tunalalamika wakati utaratibu upo wazi kabisa
 
Mkuu inaonesha huo umeme ulikuwa umeishia mbali naulipo wewe nandiomana ikawa hivyo ila nachoona niwewe mwenyewe uliamua kujiingiza huko kwasababu hela ulikuwa nayo ila ilikuwa vizur ungevuta subira maana kwausawa huu milioni 15 sio haba nusu yagharama yanyumba nyingine
 
me nijuavyo watakaohitaj conection itabidi wakulipe
 
Sasa na wewe ungepataje huo umeme kama usingeanzia kwenye nguzo ya mtu mwingine aliyeilipia?.Je na wewe ulipishwe.Tuache ubinafsi.
 
me nijuavyo watakaohitaj conection itabidi wakulipe
Siyo kweli unapotosha! miundo mbinu hiyo tiyari imeshakuwa mali ya SHIRIKA, alichokosa yeye ni subra ya kuwasubiria TANESCO wafanye Installations ya miundo mbinu yao wenyewe kwa kuwa PESA alikuwa nayo na sasa analazimisha FIDIA kitu ambacho hakiwezekani. Labda kama utaratibu umebadilika
 
Ndugu wadau,

Kuna jambo linanitatiza katika mpangilio wa ufanyaji biashara wa hili shirika la umeme TANESCO. Mimi nahitaji kuunganishiwa umeme katika nyumba yangu umeme ambao nitakuwa naulipia kwa kadiri ya matumizi yangu. Lakini ninakerwa na huu utaratibu wa malipo ya vifaa vya kuunganishiwa umeme.

Kwa mfano natakiwa nilipie nguzo kadhaa, waya mita kadhaa, Transformer, na kadhalika jumla ya ngarama naambia ni Tshs Mil. 15, eti kwa ajili ya kuweka miundombinu ya kufikisha umeme ndani ya nyumba yangu. Lakini cha kushangaza baada ya kulipia vifaa hivi kwa Mil 15, vifaa husika vinageuzwa kuwa mali ya TANESCO Bila mimi muhusika kufahamishwa au kuombwa na Shirika hili.

Kupitia miundo mbinu hii niliyo nunua kwa pesa zangu za kudunduliza na mikopo, utaona TANESCO wakianza kuunganishia umeme watu wengine jirani yangu kwa bei nafuu bila kuulizwa au kuombwa na wahusika. Je hii ni haki? Shirika kujinufaisha kupitia mpango huu! Au kwa kuwa ni Shirika la Serikali linafanya litakavyo?

Je kujenga miundombinu ya umeme ni kazi ya mlaji au ni kazi ya msambazaji?
Duuuh mkuu gharama yote hiyo na bado vifaa ni mali ya tanesco, chamsingi kuliko kulipa pesa yote hiyo toa mil 5 tu itafute solar tu, naamin hiyo solar system utakyoiweka kwa gharam hiyo itakuwa na uwezo mkubwa sana , ambayo itakusaidia mpaka kipind umeme utakapofika karibu na nyumba yako
 
Mkuu wala hujatapeliwa, watu wengi wavivu kusoma terms and conditions,

Miundo mbinu yote ya TANESCO ambayo umelipia haijalishi thamani yake bado vitabaki kuwa vyao. Hilo limeainishwa wazi kabisa bila kificho.

Wakati mwingine tunalalamika wakati utaratibu upo wazi kabisa
Vigezo vya namna hii ni aina ya ukandamizaji, na vipo tu kwa kuwa hakuna namna mbadala wa kupata huduma hii.
Haiingii akilini mtu uambiwe ugharamie kitu ambacho hakikuhusu.
 
Tatizo kwanini wasisambaze kwa ela yao kama vifaa vya kwao mbona kampuni za simu hazichangishi minara?
 
Mkuu wala hujatapeliwa, watu wengi wavivu kusoma terms and conditions,

Miundo mbinu yote ya TANESCO ambayo umelipia haijalishi thamani yake bado vitabaki kuwa vyao. Hilo limeainishwa wazi kabisa bila kificho.

Wakati mwingine tunalalamika wakati utaratibu upo wazi kabisa
Kun mteja alilishitaki shirika la umeme(TANESCO) kwa kuwaunganishia wateja wengine ktk nguzo alizokuwa kazilipia yeye,huyo mteja alishinda kesi na TANESCO walimfidia zile gharama..!!
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Naamini mleta mada anayo hoja. Ni utaratatibu ambao haupo fair. Kuna wachache wanaumia kuliko wengine.

Kungeweza kuwa na namna bora zaidi kuliko kuwalipisha wanaotaka kuunganishwa hasa kwa miundo mbinu ambayo ni ya kuchangia. Sina tatizo sana na vitu kama mita. Lakini nguzo ingepaswa gharama ibebwe na Tanesco.

Mojawapo sababu katika mgogoro kati ya tanesco na zanzibar ni katika hili la gharama za miundo mbinu.

Lakini hilo ni tatizo la Tanesco kuwa na monopoly kwenye biashara ya umeme. TTCL nao walikuwa kama hivyo kwenye simu na baada ya ushindani wameshika "adabu". Mteja ni mfalme!

Kungekuwa na ushindani naamini wenyewe Tanesco kama mmoja wapowa watoa huduma wangekuwa wa kwanza kuweka nguzo na miundo mbinu wakiona mtu ameanza kuchimba msingi wa nyumba tu.
 
Vigezo vya namna hii ni aina ya ukandamizaji, na vipo tu kwa kuwa hakuna namna mbadala wa kupata huduma hii.
Haiingii akilini mtu uambiwe ugharamie kitu ambacho hakikuhusu.
Niwakati wa Kutoka usingizini na kudai Haki na kulaani utapeli huu.
 
Back
Top Bottom