Je, hii picha imebeba ujumbe gani?

Siyo Bange kweli hizi?
 
Mna maarifa mengi kichwani lakini mnaendeshwa na miili yenu,nafsi hundeshwa na kichwa safi.
 
Kwa tafsiri yangu ya hio pic Kwamba Elimu ndio kila kitu katika maisha,Elimu yako ndio itakufanya ujitathmini wew mwenyeo na mwenendo wako wa maisha. Pia ukielimika utakua ni mtazamo unaotizamwa na watu wengi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari zenu wana jukwaa?

Hivi hii picha inaa maana gani? kwa asili huwa najitahidi kufikiri ila kwa hii picha nmeshindwa kuilewa!!

Msaada wenu unahusika zaidi hapa kufumbua!View attachment 838237
Maarifa kupitia maandiko/kitabu ndicho humuweka mtu mkamilifu.

Na kwamba kupitia nyenzo (mikono iliyoshika kichwa) mtu huweza kumjua mtu kupitia maarifa aliyoyapata.

Kwa mfano mtu unaweza kumjua tabia ya mtu kutokana na maarifa aliyonayo.

Mathani. Tabia ya Mh. Lugola inasibishwa na maarifa yake ya upoli aliyousomea na kuufanyia kazi!...tabia ya Hayati Nyerere zimejengwa ktka maarifa ya Ualimu aliousomea na kuishi kama zilivyo tabia za manesi (huruma kwa wagonjwa) na huruma ya kumsaidia mtu!

Pia mchoro huu unaonesha mfano wa mtu asiyevaa nguo. Aliye uchi. Hii inamaana kwamba nje ya kujisomea au kutafuta maarifa ni sawa na kuwa uu mtupu, maarifa hufunika soni zetu.

Hali kadhalika lazima utenganishe kichwa (ubongo) na kiwiliwili kinachowakilisha Moyo. Kwa sababu Ubongo/kichwa hufanya kazi objectively bali Moyo hufanya Subjectively kwa kuongozwa na emotions kuliko facts.
 
Habari zenu wana jukwaa?

Hivi hii picha inaa maana gani? kwa asili huwa najitahidi kufikiri ila kwa hii picha nmeshindwa kuilewa!!

Msaada wenu unahusika zaidi hapa kufumbua!View attachment 838237
Jitazame na kujichunguza kwanza wewe kabla ya kuwahukum wengine

Sent from my TECNO-Y6 using Tapatalk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…