Je hii ni sawa?

The Finest

JF-Expert Member
Jul 14, 2010
21,605
6,071
Habari wadau wa JF

Kuna jirani yetu ambaye tunakaa naye same compound alizaa watoto wawili bahati mbaya wote wakafariki kabla hawajafikisha hata umri wa miezi sita na wote walifariki kwa ugonjwa wa animonia sasa baada ya kushika mimba ya tatu ikawa imeamriwa huyu dada aende akakae kwa mama mkwe wake Dodoma ili apate uangalizi mzuri mume wa huyu dada yupo hapa Dar baada ya huyu dada kuondoka kwenda kwa mama mkwe akaletwa mdogo wake huyo dada ili aje kukaa hapo kwa mumewe na ni takribani mwaka mmoja sasa tokea yupo hapo, huyu mdogo wake amekuwa akimpikia na akimfulia nguo mume wa dada yake, Je kwa muda wa mwaka mmoja aliokaa hapo na mume wa dada yake huyu binti atakuwa anajisikiaje? Na je ni sawa kumuacha mumeo kwa muda wa mwaka mmoja ukaenda kukaa kwa mama mkwe na huku nyuma ukimuacha mumeo na mdogo wako wa kike nyumbani? Isije ikatokea kisa kama alichotuhadithia FirstLady cha Pain Over My Sister's Pregnancy For My Husband, Je hii ni sawa?
 
:confused2: mie sijaona watu wanavituko kama wa TZ.... sasa huyo Mume hawezi kukaa peke yake mpaka aletewe mtu wa kukaa nae? halafu dini inasema wala msikaribie zina thats means haifai two adults wakae peke yao kwenye nyumba....anything can happen...
 
Aaah jamani tuwaachie wao wamekubaliana lakini na wakati mwingine mie naona herai nusu shari kuliko shari kamili............wanandoa wanahitaji mtoto kwa sasa; that is their focus...........there is a price to pay...............shem amekuja kukaba loaf ili kama itatokea uwepo msaada wa haraka..........hili likikubaliwa na likaeleweka halina ubaya lets be honest............uwepo wa shemeji unaweza kumzuia jamaa kujipindua na madem huko nje!

Mie naona inaleta amani kidogo kwa mke aliyeko Dodoma kuliko angmwachia uhuru wa moja kwa moja mumewe! Hebu tuangali pande zote za shilingi.
 
Nimekuwa nikijiuliza swali hili kwani mume hawezii kukaa peke yake lakini sishangai imekuwa kasumba kwa watanzania pindi mke akiwa hayupo basi yule mume lazima aletewe mtu ili aweze kumsaidia na mara nyingi unakuta anayeletwa ni mdogo mtu wa mke wa mwanaume na baadae ndio hapo mambo ya infidelity yanapokuja
 
Aaah jamani tuwaachie wao wamekubaliana lakini na wakati mwingine mie naona herai nusu shari kuliko shari kamili............wanandoa wanahitaji mtoto kwa sasa; that is their focus...........there is a price to pay...............shem amekuja kukaba loaf ili kama itatokea uwepo msaada wa haraka..........hili likikubaliwa na likaeleweka halina ubaya lets be honest............uwepo wa shemeji unaweza kumzuia jamaa kujipindua na madem huko nje!

Mie naona inaleta amani kidogo kwa mke aliyeko Dodoma kuliko angmwachia uhuru wa moja kwa moja mumewe! Hebu tuangali pande zote za shilingi.

Na akijirusha na shemejiye akampachika mimba soo likipamba moto utasikia kauli zifuatazo..... "Ina maana haukuona wanawake wengine hadi umeamua kumpachika mimba mdogo wangu"
 
This is a Family matter...
Na wewe una mambo yako ya kifamilia ya kuyamaliza mwenyewe.
Habari wadau wa JF

Kuna jirani yetu ambaye tunakaa naye same compound alizaa watoto wawili bahati mbaya wote wakafariki kabla hawajafikisha hata umri wa miezi sita na wote walifariki kwa ugonjwa wa animonia sasa baada ya kushika mimba ya tatu ikawa imeamriwa huyu dada aende akakae kwa mama mkwe wake Dodoma ili apate uangalizi mzuri mume wa huyu dada yupo hapa Dar baada ya huyu dada kuondoka kwenda kwa mama mkwe akaletwa mdogo wake huyo dada ili aje kukaa hapo kwa mumewe na ni takribani mwaka mmoja sasa tokea yupo hapo, huyu mdogo wake amekuwa akimpikia na akimfulia nguo mume wa dada yake, Je kwa muda wa mwaka mmoja aliokaa hapo na mume wa dada yake huyu binti atakuwa anajisikiaje? Na je ni sawa kumuacha mumeo kwa muda wa mwaka mmoja ukaenda kukaa kwa mama mkwe na huku nyuma ukimuacha mumeo na mdogo wako wa kike nyumbani? Isije ikatokea kisa kama alichotuhadithia FirstLady cha Pain Over My Sister's Pregnancy For My Husband, Je hii ni sawa?
 
Tusubiri baada ya muda utasikia mimba,maana kukaa na mtu mwaka huku akifanya shughuli zote za ndani si mchezo.
Jamani watanzania tuache tabia hizi.
 
Aaah jamani tuwaachie wao wamekubaliana lakini na wakati mwingine mie naona herai nusu shari kuliko shari kamili............wanandoa wanahitaji mtoto kwa sasa; that is their focus...........there is a price to pay...............shem amekuja kukaba loaf ili kama itatokea uwepo msaada wa haraka..........hili likikubaliwa na likaeleweka halina ubaya lets be honest............uwepo wa shemeji unaweza kumzuia jamaa kujipindua na madem huko nje!

Mie naona inaleta amani kidogo kwa mke aliyeko Dodoma kuliko angmwachia uhuru wa moja kwa moja mumewe! Hebu tuangali pande zote za shilingi.
usiniambie haifai kabisa mwanaume kuoa au kulala na dada wawili ...ni fitna kubwa sana kwenye family... jamani hivi mungu alileta Prophets na vitabu vya nini? si kututoa ujinga? we are human beings we have values...unlike animals....

na kama huyu dada anaweza kumtizama mume I think she can take care of her sister as well.... both of them can stay with the husband.... and it is his duty to take care of his wife as well...sio kumpeleka kwa wazazi...
 
sasa jukumu la kutunza mume wake kamuachia mdogo wake au?

kuna watu wengine wanajitafutia matatizo kisha wanaanza kulalamika.

kama kuna ulazima mama mkwe ndio angeletwa akakaa nao hapo akamsadia kutizama mtoto. mtu unaondoka kwa mumeo mwaka mzima unategemeaje? huduma zake binafsi amalizie wapi?
 
Gaijin huduma gani tena mama wa watu mgonjwa? khaa? mie naona it is all his fault...he should b a man and take care of his wife...si anataka watoto? avumilie na subira ni nzuri...
 
noname mama mgonjwa mwaka mzima?

huyo mama alikuwa kama anaenda kuzaa kwa mkwe ende ...mtoto akikuwa ndani ya miezi mitatu arudi.

sasa hatarudi mpaka kuwe hakuna possibility ya watoto kufa? watajuaje wao? wanamipango na ziraili?

mama haumwi noname......................wanataka tu kuhakikisha watoto hawapati ugonjwa wakafa ATI.

arudi atunze mume, na hata kama anaumwa, arudi atunzwe na mumewe
 
si dada mtu kamwamini mdogo wake mwacheni,kwanza hamna shida maana nina mifano ya mtu na dada yake kuolewa na mtu mmoja:mad2:
 
noname mama mgonjwa mwaka mzima?

huyo mama alikuwa kama anaenda kuzaa kwa mkwe ende ...mtoto akikuwa ndani ya miezi mitatu arudi.

sasa hatarudi mpaka kuwe hakuna possibility ya watoto kufa? watajuaje wao? wanamipango na ziraili?

mama haumwi noname......................wanataka tu kuhakikisha watoto hawapati ugonjwa wakafa ATI.

arudi atunze mume, na hata kama anaumwa, arudi atunzwe na mumewe
haha labda wanamipango na ziraili ... kumbe ndio wanaamini hivyo..kazi kweli kweli... basi i am with you on that....
 
Pesa kutoka mfuko mmoja wa suruali imehamishiwa mfuko mwingine wa suruali hiyo hiyo. Haiko maneno.
 
mimi hata niwe mgonjwa siendi kwa mama mkwe, labda niende kwa mamangu!!!!!
 
Hivi kwani pneumonia ndo ikabidi ahamishe makao ndo suluhisho kweli? ilikuwa advise ya daktari? na je, mwaka mmoja bado tu anaogopa kuwa atapata pneumonia au walishindwa kumpa matibabu stahiki? isije ikawa kuna tatizo jingine kwenye hiyo familia?
 
Ina maana wanaume hawawezi kukaa na shemeji zao wa kike, lazima wawamendee...!?
 
Huyo mwanaume kashindwa kujipikia,kufua nk? Eishh maji yakishamwagika ndo watu wanakimbilia kuzoa!!..
 
Back
Top Bottom