Je hii ni lazima Ben?

mharakati

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
1,271
391
Mkapa (rais wa awamu ya tatu), baada ya kustaafu alijijengea nyumba ya thamani isiyopungua bil4-5 kwa thamani ya sasa huko Masaki mwisho kutoka kwenye akaunti za taifa kama zawadi ya kustaafu...sasa ili kuondoa aibu na kufuatwa fuatwa amelazimisha kua hiyo itakua ni package ya kila Rais wa Tanzania kutumia tujisenti twetu walipa kodi kumzawadia Rais mstaafu mahekalu haya.

tatizo siyo kwamba Rais haitaji nyumba, la, tatizo ni gharama na anasa zisizo na msingi kwa taifa maskini kuwazawadia hawa wakubwa haya mahekalu wakati tayari wana makazi yao mazuri tu kwa viwango vyetu vya kitanzania au hata kama Rais anastaafu akiwa hana nyumba ya heshima basi ajengewe nyumba ya kuishi na siyo hoteli ya kifahari inayogharimu serikali mamilioni kuihudumia tena...Hatujui na mengine yapi yamepitishwa kwa wasstaafu, lakini hii inaonyesha kutokua na uzalendo kwa hali ya juu kabisa.

Kwa wale wasiojua lile hekalu la Mkapa na anasa iliyopo mle ndani...nyumba ina level 3, na ukubwa au upana wa 70 m2 au acre moja nzima kutoka upande mmoja wa nyumba hadi mwingine...finishing na furniture ilichukua $2 mil**. Katika anasa zilizopo kuna reli ya kuwekea taulo bafuni ya mbunifu maalum wa mabafu ya anasa inayohifadhi joto (taulo zizishike baridi)..na vikolo kolo vingine visivyokua na umuhimu kwa matumizi ya hapa Tanzania.

kwa spidi hii marais wanaokuja watakua wanajenga mahekalu ya thamani sasa sawa sawa na bajeti za taasisi, idara, na hata wizara zetu..Mwinyi ameshaandaliwa kiwanja maeneo hayo hayo na inasemekana bajeti haijatosha kuanza ujenzi, na Jk naye atakuja na lake, n.k

Mungu endelea kuipenda Tanganyika yetu,

Mharakati,




** wahusika wa mradi wenyewe ni source**
 
We ndio umeona hiyo reli ya taulo ndio kitu kikubwa? Kwanza ulifata nini bafuni kwake?
 
Back
Top Bottom