Nafikiri anavaa kama pambo tu. Kama ingekuwa ni alama ya ukuu, au ufalme basi angevaa Rais wa nchi kama ambavyo Zuma au marais wa Haiti wamevaa. Sasa yeye first lady ni mkuu wa nani/ni kiongozi wa nani? Hatukuwahi kumchagua yeye kuwa kiongozi wetu. Hata hivyo sikuwahi kumwona mama Mkapa amevaa. Kama kweli inamaanisha hivyo basi huyu naye ni limbukeni. Maana ukuu wa mtu hautambulishwi kwa mavazi bali kwa kazi nzuri anayoifanya.