je hii ni halali?

wazo lilikuwepo cha ajabu kipi mbona kuna makamu wa rais mmoja hapa bongo alikufa bila kujenga tulipanga mwaka jana ndio tununue hicho kiwanja mwaka huu tuanze uenzi yeye achukue mkopo tununue kiwanja mimi nichukue tuanze ujenzi tatizo jina lake kwenye hati kwa kiwanja cha kwanza ndani ya ndoa ,sure natakiwa kurudisha ukichwa wa mwanmme
 
kwa maana hiyo mwanamke yeye kaumbiwa shida tu ndo mwenye kustahili kutimliwa na kubaki bila chochote? Hata mlalamike saivi wote 2napambana kuvitafta bana
haikatazwi mwanamke kumiliki mali mbona gari lina jina lake wala halinitishi mi hata daladala ntapanda incase sina hela ya mafuta au likiwa bovu,nyumba ni sensitive issue tena nyumba ya kwanza ndani ya ndoa pale ndio unapopatia usingizi wako tatizo sio kununua tatizo sjui dhamira yake
 
Unajua hapa Jf na kwingineko kuna katabia ka kuvindicate dada zetu wa Kichagga hasa pale mambo yanapokuwa ndivyo sivyo.

Sijapenda daana kuhusisha umiliki wake wa kiwanja na kabila lake....wakati unamuoa hukujua kabila lake? Ulilazimishwa mkuu? Suala la kuandika jina lake angeweza kufanya mwanamke yeyote anayejitambua and honestly sioni tatizo hapo zaidi ya ww kutokujiamini.

Ila hili la kusema eti kwa vile katokea KNjaro ndo linanipa shida kidogo apa....huko ndani mnaishije mnapeana unyumba kweli?

Cc Asprin Heaven on Earth gfsonwin Ablessed neggirl Smile RR miss chagga Munkari DEMBA
 
Last edited by a moderator:
eti mwanaume kumiliki ki2 sio shida ila mwanamke kumiliki inakuwa gumzo! Huo unyanyasaji wa kijinsia bana wote tuna haki za kumiliki

cha mume cha wote cha mke cha mke
 
Usichangie chochote kwenye ujenzi, nunua kiwanja chako, anza ujenzi wa nyumba yako.
Nina mafano hai katika hili. huwa napita naiangalia hiyo nyumba roho inaniuma sana ila nilishasamehe
Ila usithubutu
 
Kaa chini uongee na mkeo....period!!!

 

hapo kwa hawa kazi ipo hata me bado sijaingia lakini najua ndoa ni maelewano kwa kweli na kama ni kununua kiwanja lazima majibna ya mama baba na mtoto
 
We chalii yangu ni ---- kinoma yaani...
Mwanaume unakalisha matak@ nyumbani hadi mkeo ananunua kiwanja????
Kisha unakuja mbele ya wanaume wenzio kulalamika kwamba mkeo kakuzidi ujanja!!!
Halafu unalaumu kabila la mkeo!
Ulitaka anunue kiwanja kisha aandike jina la nani kama wewe umelala??


Huyu hakuoa....nadhani aliozeshwa!!!

 

umeongea vema mine. hebu ashirikiane na mkewe wajenge nyumba kwa maslahi ya watoto. hii aliyoonyesha hapa ni tabia ya kibinafsi tu
 

Kaizer asante kwa kuniita. Mleta mada atutake radhi wadada wa kichaga lolz!

Kwa style hii anaonyesha wazi hana imani na mkewe, but nachofikiri ni vyema wao kuzungumza kabla huo ujenzi haujaanza, sio kuhusiana na kiwanja tu bali kuhusiana na mali za familia zitakazonunuliwa na yeyote kati yao yatumike majina yao yote au iweje! To me, dada yangu huyo kama alijua nyumba ni ya familia alipaswa aandike majina yote. Huo ndio mtazamo wangu.

Baadhi ya wanaume ni watu wa kujishuku sana usipokuwa makini na vitu hivi jamaa anaanza kujishtukia.
 
Last edited by a moderator:
Miaka 5 yote hamjaaminiana? Kwanza inawezekana yeye anakuamini, wewe tu humuamini. Angalia maana siku si nyingi utaanza kuwaza kama hao watoto wawili ni wako...

daaa... maisha ya kuviziana, utafikiri mko siasani ..hehe heeee
 
kumbuka huo mkopo tulishauriana yeyey achukue mwaka jana anunue kiwanja na mimi nichukue mwaka huu tuanze ujenzi umenipata,dhamana ni kazi zetu

kama mlikubaliana kukopa, natumaini hata kwenye kutafuta kiwanja ulishiriki.. kama hukushiriki what happened??
Nachokiona hapa, kuna shida katika mahusiano yenu na ndio iliyopelekea kuvunjika kwa ushirikishwaji.
 
kama mlikubaliana kukopa, natumaini hata kwenye kutafuta kiwanja ulishiriki.. kama hukushiriki what happened??
Nachokiona hapa, kuna shida katika mahusiano yenu na ndio iliyopelekea kuvunjika kwa ushirikishwaji.
tulishirikiana process zote isipokuwa hatukujadili jina gani litumike alipotoka bank akapitia kwa mwanasheria akadraft mkataba wenye jina lake na muuzaji,
 
we unafikiri kuishi na dada wa kichaga ni kama kuishi na mwanamke wa kizaramo au kimakonde sifagilii ukabila ila wanawake wa kichaga wengi wamesoma na wanatiming kali wanaona mbali either in a positive or negative way so akili zaidi inahitajika kuishi nao
 
Nahisi hata hao watoto sio wako kaka, kapime DNA kabisaaaaa kungali mapema!!
 
Usichangie chochote kwenye ujenzi, nunua kiwanja chako, anza ujenzi wa nyumba yako.
Nina mafano hai katika hili. huwa napita naiangalia hiyo nyumba roho inaniuma sana ila nilishasamehe
Ila usithubutu
Hebu tupe mfano mmoja na wengine waelewe unachoongea maana wengine wanamuona zoba
 
tulishirikiana process zote isipokuwa hatukujadili jina gani litumike alipotoka bank akapitia kwa mwanasheria akadraft mkataba wenye jina lake na muuzaji,

dii.....
 

1. Asante kwa kutupa sifa ya kusoma
2. Pole shemeji yangu, kila kitu kina faida na hasara zake, ungeoa bogaz ingekuwa balaa lingine. NOA kichwa ujue jinsi gani ya kuishi nae kwa AKILI. Ni jukumu lako kuishi na Mkeo kwa Akili.
3. HUONI KAMA HIYO NI CHANGAMOTO Kwako? kakufungua akili sasa.. mmeoana mna 5 years, bila bila... Though nahisi huenda hajui kama kakosea, ni vyema kuzungumza nae pia. Kila la kheri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…