Je, hii inaweza kuwa laana?

kibaravumba

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
6,635
7,005
Nilimaliza kidato cha nne na kufaulu kiwango cha div 2 na kuchaguliwa kuendelea na A level ambako sikufanikiwa kufanya vizuri kwa sababu ya ukosefu wa walimu na umaskini mkubwa ulionikosesha hata fursa ya kusoma tuition ambayo iliwasaidia wote waliofanya vizuri kipindi hicho.

Nilipata nafasi ya chuo kimoja kikubwa hapa nchini kwa kozi diploma ya afya.Nilifanikiwa kuipata GPA 4.Tangu mwaka 2007 nimekuwa nikiomba nafasi ya kujiendeleza kwa kozi yangu lakini sijawahi kupata.2011 nilipata kozi tofauti na fani yangu lakini nilishindwa kusoma kwa kuwa niliambiwa siwezi kupata mkopo.

Mwaka huu nimeomba tena na nilifurahi walivyosema GPA lazima iwe kuanzia 3.5 maana nikajua nafasi inaweza kuwa kubwa ya kufanikiwa.Lakini La!haikuwa hivyo.Cha kushangaza zaidi nilivyona wamepunguza cut points hadi GPA ya 3 lakini mimi nina nne sijapata!Hat hivyo Mungu ni mwema nimeamua nisubiri kozi nyingine tofauti na fani yangu ili nitimize ndoto yangu ya kupata shahada ya kwanza kupitia chuo kikuu huria.

Je, wakuu hii inaweza kuwa laana? Kuna watu wamewahi kupatwa na aina hii ya bahati mbaya?
 
Kuna watu mna mioyo fragile kama kioo aisee, hamuwezi kukabili changamoto ndogo ndogo za maisha.

Yaani issue ndogo kama hiyo ndo unasema ni laana?....umejijengea mentality mbovu sana Mkuu.

Kuna mtu alimaliza Muccobs 2004 hadi leo hana kazi.

Kuna mwingine alimaliza MD Muhimbili 2000 akafariki wiki na nusu baada ya mahafali.

Maadam wewe ni mzima, jiulize kwa nini unaitaka hiyo degree? Maana ukishapata hiyo degree ukaja kukosa kazi ndio utaamini kuwa una laana kweli.

Surviving has never been an easy task!
 
Hizo ni changamoto tu za maisha kinachotakiwa usikate tamaa katika maisha.Endelea kupambana Mungu ni mwema kila siku ipo siku utatimiza ndoto yako
 
Kama mtu ujawah kutana na changamoto kubwa kubwa unaeza dhan kwamba umelogwa au n.laana but n vitu vya kawaida ukichukua hatua fulan unaeza tatua tatizo lako vizur tuu na malengo yako yakatimia
 
Back
Top Bottom