Je haya maovu Halmashauri ya Maswa yana baraka toka Serikali Kuu?

MKWANO

JF-Expert Member
Jul 19, 2014
221
153
Halmashauri ya Wilaya Maswa
(1) kuto walipa watumishi Malipo ya Likizo hasa idara ya Elimu, huku watumishi katika halmashauri zingine kama Nyamagana wakipewa fedha wiki moja kabla ya kuanza likizo.

(2) Walimu kulazimishwa kuchangia TSH 5000 kwa ajili ya Madawati licha ya kukatwa kodi kila mwezi.

(3) kuamlisha watumishi wote kupeleka Passport size halmashauri kabla ya Tarehe 30 mwezi huu bila kujali kuwa kuna baadhi ya watumishi hasa idara ya Elimu wako likizo.

Je haya yanabaraka ya serikali kuu? au ndo mwendelezo wa ubabe kwa wanyonge?

NANI ANAJALI .
 
Nyie walimu Mmezidi kulialia. Hivi mnawaogopa sana hao maafisa elimu wenu kwanini msiwafuate muambie haya mnayoyaandika humu msitake tukubali nyie ni vilaz, mnafikiri nyie tu ndio watumishi.
 
NANI ANAJALI?

HAKUNA ANAYE JALI, MAANA KILA KIONGOZI HAIJALISHI ANA CHEO GANI NI MTUNGA SERA NA SHERIA, hata sheria walizotunga wenyewe wanapishana nazo na kutekeleza ilani zao.
 
Nyie walimu Mmezidi kulialia. Hivi mnawaogopa sana hao maafisa elimu wenu kwanini msiwafuate muambie haya mnayoyaandika humu msitake tukubali nyie ni vilaz, mnafikiri nyie tu ndio watumishi.

kwa bahati mbaya mimi sio mwalimu ndugu, ila ni roho ya huruma tu kwa hawa ndugu zangu walimu. pia ndo maana nimetaja halimashauri ya Nyamagana kama reference.
 
Halmashauri ya Wilaya Maswa
(1) kuto walipa watumishi Malipo ya Likizo hasa idara ya Elimu, huku watumishi katika halmashauri zingine kama Nyamagana wakipewa fedha wiki moja kabla ya kuanza likizo.

(2) Walimu kulazimishwa kuchangia TSH 5000 kwa ajili ya Madawati licha ya kukatwa kodi kila mwezi.

(3) kuamlisha watumishi wote kupeleka Passport size halmashauri kabla ya Tarehe 30 mwezi huu bila kujali kuwa kuna baadhi ya watumishi hasa idara ya Elimu wako likizo.

Je haya yanabaraka ya serikali kuu? au ndo mwendelezo wa ubabe kwa wanyonge?

NANI ANAJALI .
Acha wakomeshwe tu huko usukumani ndio waliimba sana lile sebene letu
 
Hayo yapo kwa kila Halmashauru ndugu...
Tena halmashauri zingine ni zaidi ya hayo uliyo yataja hapo juu.
 
Suala la kulazimishwa kuchangia kitu chochote halikubaliki. Wawe wabunifu basi hao watendaji. Kwani ukigoma kuchangia atakufanyaje?

Zaidi walimu naona kama nao wamekuwa wakifurahia hizi hali. Yaani kitu kidogo tu, WALIMU!!! Amkeni bana acheni kulialia kama watoto. Sasa kama nyie ndo mnaozalisha watoto wenye fikra na maono chanya kwa Taifa na kila siku wanasikia mnalialia tuuuuuu, hapo mnataka wao wafanyeje sasa wakinyimwa haki zao?

Yawezekana ni kwa sababu ya unyonge wa walimu ndiyo sababu kizazi hiki kimekuwa DORMANT eh!!!
 
Back
Top Bottom