Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,154
- 144,681
Wadau, kama mnakumumbuka sakata la makinikia lilitingisha nchi kwa kiasi kikubwa sana na hii ni kutokana na jinsi sakata lenyewe lilivyoshughulikiwa na serikali sambamba na matumizi makubwa ya media kutangaza matukio husika kuanzia matukio ya kutangaza matokeo ya kamati mbili za Raisi, kutangaza ujio wa Boss wa Barrck na ahadi ya kishika uchumba bila kusahau live coverage ya kuwatunuku nishani wajumbe wa kamati za makinika kwa kazi nzuri waliyofanya (kazi iliyoitwa ya kizalendo).
Hata hivyo, majuzi Mbunge wa Kigoma Mjini, Mhe Zitto kabwe ametoboa siri kuwa kuna kesi inaendelea kati ya serikali ya Tanzania na kampuni ya Acacia ambapo wanatudai zaidi ya trilioni 4 na mpaka leo hii serikali haijakanusha madai haya hivyo sisi wengine tumeani ni kweli maana Zitto alitaja mpaka namba ya kesi.
Sasa wadau, kwa nguvu kubwa ile iliotumika mpaka na kutoa nishani kwa wajumbe wa zile kamati mbili alafu ghafla tunaangukia pua huko London kuwa kilichofanyika hakikuwa kitu sahihi, tutakuwa tayari kupokea aibu hii bila kufanya any sort of damage control?
Je, kujitoa huku kabla ya hukumu kutolewa sio hatua ya kujihami kwa kuwaaminisha watu mapema kuwa hizo mahakama hazitendi haki na hivyo hatui hii ni kama kuwaanda watu kisaikolojia kuwa maamuzi yatakayotolewa sio ya haki?
Je, hii si damage control ya mapema?
Na je, hatua hii sio kutaka kujaribu ku-influence uamuzi wa mahakama juu ya kesi hii na zingine tunazosikia zipo(kutafuta huruma)?
Na je, ikitokea tumeshinda( ingawa matumaini ni madogo kulingana na maelezo ya Zitto aliedai kuona ripoti ya kesi hiyo) tutasemaje?