Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 427
- 666
Baada ya Bunge la Ulaya (EU) kujadili masuala mbalimbali yanayohusu ukiukwaji wa haki za Binadamu Nchini Tanzania ikiwemo mashtaka yanayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu na kutoa azimio kuwa aachiwe huru bila masharti
Suala hilo lilijadiwa jana Mei 7, 2025, ambapo Wabunge mbalimbali wametoa wito wakieleza haki itendeke katika shauri hilo na kulinda uhuru wa Kisiasa, usalama wa Waandishi wa Habari, Watetezi wa Haki za Binadamu ili kuendeleza ushirikiano uliopo baina ya Bunge hilo na Tanzania.
Akizungumzia suala hilo katika jicho la kidiplomasia, Mkufuzi wa masuala ya Diplomasia ambaye pia ni mchambuzi wa masuala ya siasa, Deus Kibamba ameeleza masuala mbalimbali kuhusu suala hilo.
----------------------
Bunge la Ulaya wapi linapata wapi nguvu ya kujadili suala hilo ikiwa Tanzania ni Taifa huru?
Anajibu "Dunia imekubaliana kwamba kuna baadhi ya mambo lazima kila Nchi iyafuate (Universal Standard), ambapo jumuiya ya kimataifa imekubaliana kusiwepo Mtu anayezikiuka."
"Kati ya hizo 'standard' ni pamoja na haki ya kuishi, kwa mfano hawezi kujitokeza Mtu kwamba hawa ni watu wangu nawaongoza hata nikiwachinja kwani inawakela nini, hiyo hairuhusiwi huwezi kufanya hivyo na Dunia haitakuacha."
Kibamba anasema kwamba Tanzania ni miongoni mwa Nchi mwanachama wa Jumuiya ya Kimataifa na imesani Tamko hilo kwamba wataheshimu.
"Mfano Tanzania ni moja kati ya Nchi zilizosaini kwamba itaheshimu tamko la Kidunia la Haki za Binadamu (Universal Declaration of Human Rights -UDHR)."amesema Kibamba
Anasema kwamba Nchi zilizosaini tamko hilo zinalazimika kuheshimu haki zilizotajwa, ambapo ameongeza kwamba haki nyingine muhimu iliyotajwa ni kwamba Mtu akituhumiwa kutenda kosa mchakato wa kumshtaki na uendeshaji wa mashtaka uwe wa haki.
Anaongeza "Lingine ambalo lipo kwenye Tamko hilo ni kwamba Mtu asifunguliwe mashtaka kwa kubabikizwa kutokana na maoni yake ya kisiasa (hiyo ipo kwenye haki za kisiasa)"
Je, Tanzania katika hili imeingiliwa na Bunge EU?
Anaeleza "Ni wajibu wa Jumuiya ya Kimataifa kuweza kulinda haki hizo Kidunia na Umoja wa Ulaya umetengeneza utaratibu wa ulinzi wa haki hizo za binadamu bila kujali zinakiukwa ndani ya Ulaya au nje ya Ulaya, wao wameweka utaratibu kwamba kuhusu haki za binadamu yeyote atakayezikiuka Duniani tutashughulika naye"
Amesema kwamba kila Nchi huru inaweza kufanya mambo yake bila kuingiliwa lakini kutekeleza mambo hayo haitakiwi kukanyaga haki za watu wake waziwazi. Amesema kwamba ikifanyika hivyo wadau wa Kimataifa kulingana taratibu mbalimbali ambazo Nchi imesaini hawawezi kunyamaza.
Kufuatia sakata ambalo lilijadiliwa hapo jana amesema uenda limekuja baada Umoja wa Ulaya kutokana na Intelijensia yao kufuatilia matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini, amesema kwamba wamekuwa wakifanya hivyo ndani ya Umoja wa Ulaya na nje ya Jumuiya hiyo inapotokea kuna mambo wanaona hayapo sawa.
Anasema baada ya kubaini kupitia Intelijensia zao na kujadili masuala hayo uanza kuchukua hatua kulingana na mazingira na hali ilivyo, anasema wanaweza kuanza kwa kulaani, wakafika hadi kuweka vikwazo lakini anasema kwamba wanaweza kutoa taarifa kwenye Jumuiya ya Kimataifa kwenye mambo ambayo wanaona yanakiukwa kama haki.
Nini kinaweza kutokea hatua zisipochukuliwa na nani anaweza kuathirika zaidi?
Kibamba anasema Tanzania na EU wanao ushirikiano mzuri kwenye mambo mengi ambayo yana tija na yanayogusa jamii katika sekta mbalimbali, akitolea mfano misaada.
"Ukiacha Marekani ambayo ilikuwa inatoa misaada zaidi kupitia USAID mtoaji wa misaada kwa Nchi zetu hizi za kiafrika ikiwemo Tanzania ni Umoja w Ulaya"anasema Kibamba
Amesema kwa Umoja wa Ulaya umekuwa na utaratibu wa kuwezesha mafunzo pamoja na kuwajengea uwezo watanzania kwenye idara na sekta mbalimbali, lakini anasema kwamba ushirikiano huo unaenda mbali zaidi hadi kwenye masuala ya Kiusalama na kiuchumi.
Anasema, "kama inaweza kufikia hatua ya Tanzania kuwekewa vikwazo na Umoja wa Ulaya, Tanzania linaweza kuwa jambo hatari Kiuchumi", ametolea mfano bidhaa zinazotoka kwenye Nchi za Umoja wa Ulaya kuzuia zisifike Tanzania au badhaa za Tanzania zisiende kwenye Nchi za Umoja wa Ulaya, amesema kulingana na mazingira yalivyo Tanzania inaweza kuathirika zaidi.
Nini kimepelekea kufika hatua hiyo? (Tanzania kujadiliwa juu ya ukiukwaji wa haki za binadamu ndani ya Bunge la EU)
Anasema kwamba kukosekana kwa 'Utawala bora' uenda ndicho sababu kubwa ambayo imepelekea kufika hatua hiyo, anasema kwamba licha ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kuanza vyema kwa kuitangazia Dunia na kuchukua hatua mbalimbali za kuleta uhuru na uzingatiaji wa haki nyingine ikiwemo za kisiasa, anadai kwa kipindi cha hivi karibuni yamejitokeza matukio ambayo yanaviashiria vya ukiukwaji wa utawala bora.
"Rais Samia Suluhu Hassan alianza vizuri akaja na 4R watu na Dunia ikampongeza lakini sasa kile kikundi kinachotaka kutawala bila kukosolewa kimerudi"anasema
Anasema kwamba Rais Samia aliuambia umma kwamba anaenda kuliponya Taifa ikiwemo kujibu kiu ya kuzingatia utawala bora na haki za binadamu, lakini anadai kwamba kwa sasa inaonekana kuna watu wasio na dhamira njema uenda wamechangia kumtoa kwenye reli ambayo awali alianza nayo.
Nini kifanyike sasa?
Ili kuhakikisha hali inakuwa shwari na kuepuka mazingira ya Tanzania kutokuwa sehemu ya mijadala ya kutuhumiwa kukiuka haki za binadamu ameshauri kuanzishwa kwa Baraza la ushauri la Taifa ambalo litapewa nguvu ya kisheria ili ushauri wao upewe nguvu, anasema kwa sasa kuna wazee wastaafu Serikalini wamekuwa wakiangaika kushauri lakini anadai bado hakuna mazingira rafiki ya kufikisha ujumbe wao na kupewa uzito stahiki.
"Tuanzishe Baraza la ushauri la Taifa ili wazee kama wakina Warioba na Butiku, Mongela, Msekwa wawe na uwezo wa kisheria kuweza kuitisha hilo Baraza kama hali haiendi vizuri"anasema Kibamba