Je DPP anatumika kuibeba CCM?

Je DPP anatumika kuibeba CCM?

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Posts
15,842
Reaction score
31,076
Kwa mazingira ya kesi ya Mkurugenzi wa Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare, namna DPP alivyomfikisha mahakamani Kisutu, akifunguliwa mashitaka ya ugaidi na baadaye kesi hiyo kufutwa kwa amri ya huyo huyo DPP na baadaye tena Polisi kumkamata tena na kumfungulia mashitaka yaleyale, bila kubadilisha hata kipengele kimoja, inaacha maswali mengi yanayokosa majibu, kama kweli hii ni kesi ya kawaida au ni kesi ya kubambikika, inayotokana na amri za watawala!!

Maswali mengi yanayokosa majibu ni kama, kwa vipi tokea sheria ya ugaidi, ipitishwe nchini mwaka 2002, kwa shinikizo la Marekani, baada ya mashambulizi ya balozi zake mbili, za Nairobi na Dar-es-salaam, mwaka 1998, na lile shambulizi la kutisha la twin towers, jijini New York, ambalo lilipewa jina la september eleven disaster, hakujawahi kufunguliwa mashitaka yoyote ya ugaidi hapa nchini na kwa maana hiyo, kiongozi huyo wa Chadema, ndiyo anakuwa mtu wa kwanza hapa nchini kufunguliwa mashitaka ya ugaidi!!

Sasa tuangalie makosa yanayolengwa kuwa ya ugaidi ni makosa ya aina gani. Ninavyofahamu mimi tafsiri ya ugaidi ni mtu au kikundi cha watu kinapotekeleza kitendo cha uhalifu unaoweza kusababisha maafa makubwa ya watu na mali, ambapo vitendo hivyo vinatokana na chuki za kisiasa au za kidini.

Sasa hebu tuangalie huyu mlengwa wa tukio hili la 'kufikirika' la ugaidi, Denis Msaki, ana nafasi gani kubwa ya kisiasa au kidini hadi awe mlengwa mkuu wa tukio la kigaidi. Katika utafiti wangu, huyo jamaa, ukiacha kazi yake ya uandishi wa habari hana nafasi yoyote kubwa ya kidini wala ia kisiasa.

Hebu tujiulize jambo jingine, sote tunafahamu kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ibara ya 13[1] inakataza kabisa ubaguzi wa aina yoyote wa kisheria inapofikia wakati wa kufungulia mashitaka watu. Sasa tunakumbuka ni mwaka jana tu mwezi wa sita, ambapo Dr Ulimboka alitekwa na kupelekwa kwenye misitu ya Mabwepande ambako aliteswa sana, hadi kutolewa kucha na meno kwa koleo bila kutumia ganzi. Mbona katika tukio hilo, ambalo yeye mwenyewe aliyetekwa anamtaja kwa jina, mtu anayefahamika kama Ramadhan Ighondu, anayefanya kazi Ikulu, ni kwa nini basi Polisi pamoja na DPP wao, hadi leo hawajamfungulia mashitaka huyo jamaa ya ugaidi??!!

Vile vile kwenye kesi huyo kuna mtuhumiwa mmoja ambaye waTZ tunamtambua kwa jina la mtuhumiwa chizi wa Kenya wa Kova, ni kwa nini mtuhumiwa huyo feki wa Kova hakufunguliwa mashitaka ya ugaidi??!!

Kwa mazingira hayo, pamoja na mimi kuijua sheria kwa kiwango kidogo sana ukilinganisha na DPP wetu Feleshi, inamshangaza kila mtu, namna alivyoiendesha kesi ya Lwakatare, watu wengi wakijiuliza, kama ni kweli ametumia taaluma yake ya sheria au amefanya hayo kwa maagizo ya wakubwa wa chama tawala pale Lumumba??!!

Wote bado tunakumbuka jinsi mwezi Desemba mwaka jinsi Mwigulu Nchemba alivyoibuka Star TV na kudai kuwa ana mkanda ambao unaonyesha viongozi wa Chadema wakifanya mipango ya mauaji. Sasa lazima tuwaulize Polisi wetu, je umakini wao upo wapi kama anatokea mtu anadai ana mkanda wa mauaji, halafu wao wamekaa kimya na baada ya miezi mitatu kupita ndiyo wanamkamata mtu na kumfungulia mashitaka ya 'kufikirika' ya ugaidi!!

Ni dhahiri kutokana na maelezo niliyotoa, ni ushahidi usio na mashaka kuwa huu mkanda alioshitakiwa nao Lwakatare, ndiyo mkanda huo huo alioongelea Mwigulu Nchemba, kwani huo mkanda wa Lwakatare tunaelezwa kuwa ulichukuliwa kwenye tarehe za mwishoni mwa Desemba.

Kwa mazingira yanayoonekana hapa, hii kesi ya Lwakatare ni mpango mchafu ulioandaliwa na POLICCM, TISS na CCM yao kwa lengo la kuiangamiza Chadema, sasa kinachoshangaza ni kwa vipi mtu aliyebobea kwenye sheria, kama bwana Feleshi naye anatupungizwa kwenye huo mchezo mchafu wa kisiasa. Ni vyema bwana Feleshi akajitafakari upya ili kazi yake asiingize ushabiki wa kisiasa na kama atapuuzia ushauri wangu basi awe tayari wakati wowoie kuanzia sasa kuondoka ofisi hiyo kwa aibu kubwa!!!
 
Katika kesi iliyofunguliwa majuzi mahakamani Kisutu, ambapo Mkurugenzi wa usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare, alifunguliwa mashitaka ya ugaidi, inaacha maswali mengi yanayokosa majibu.

Jambo la kwanza linaloshangaza ni kuwa hapa kwenye mahakama za nchini kwetu, hii ni kesi ya kwanza kabisa ya ugaidi kufunguliwa, tokea sheria hiyo ipitishwe mwaka 2002, baada ya shinikizo kubwa toka Marekani, baada ya mashambulizi ya balozi zake jijini Nairobi na Dar-es-salaam, mwaka 1998, na lile shambulizi lililotikisa dunia linaloitwa september eleven, ambapio majengo yanayoitwa twin towers, yalishambuliwa jijini New York, Marekani.

Jambo lingine linaloshangaza ni namna kesi hiyo ilivyofunguliwa chapu chapu na kufutwa chapu chapu na kufunguliwa iena chapu chapu, bila kubadilisha kipengele chochote cha mashitaka!!!

Ninavyofahamu mimi shambulizi la ugaidi, ni shambulizi linalofanywa na mtu au kikundi cha watu, yanayoweza kusababisha maafa makubwa ya watu na mali, ambapo mashambulizi hayo huwa yana malengo ya kisiasa au kidini.

Tukiangalia huyo mlengwa wa shambulizi hilo la 'kufikirika' Denis Msaki, simuoni kama ana nafasi yoyote kubwa kisiasa au kidini hadi awe mlengwa wa shambulizi la kigaidi.

Lakini vile vile kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, ya mwaka 1977, ambayo ndiyo sheria mama, ibara ya 13[1] inakataza ubaguzi wa aina yoyote ile unapotekeza sheria za nchi yetu.

Sasa hebu tulitupie macho tukio la utekwaji nyara lililomtokea Dr Ulimboka. mwaka jana, mwezi wa 6. Inafahamiika wazi kuwa Dr Ulimboka alimtaja kwa jina mtu mmoja anayeitwa Ramadhan Ighondu, kuwa ndiye aliyekuwa kinara wa lile tukio la kutisha la kutekwa kwake hadi kupelekwa kwenye misitu ya Mabwepande, ambapo alipigwa sana na kuteswa hadi kung'olewa kucha na meno kwa koleo bila kutumia ganzi na hatimaye, watekaji wake hao wakamtelekeza kwenye misitu hiyo ya Mabwepande, hadi alipookotwa na msamaria mwema. Sasa swali linakuja, ni kwa nini hadi hivi leo, huyo mtu anayeitwa Ramadhan Ighondu, anayesemekana anafanya kazi Ikulu, hajakamatwa na kufunguliwa mashitaka ya ugaidi??!!

Swali lingine ambalo wananchi tunajiuliza, yupo mtuhumiwa mmoja ambaye anafahamika zaidi kama Mkenya chizi, mtuhumiwa wa Kova. Je kwa nini huyo mtuhumiwa wa Kova, ambaye ndiye Polisi wanataka kutulazimisha tuamini kuwa ndiye aliyemyemteka Ulimboka. Ni kwa nini mtuhumiwa huyo naye hajafunguliwa mashitaka ya ugaidi, kama kweli vyombo vyetu vya dola vinatekeleza vyema ibara ya 13[1] ya Katiba tetu??!!

Vile vile watanzania bado tunakumbuka maelezo aliyotupa Mkurugenzi wa Takukuru, Edward Hosea, kuwa alishakamilisha uchunguzi wa tuhuma za rushwa ambayo ilikuwa inamkabili Andrew Chenge, ambaye alifanya dili ya kutuletea radar 'bomu' ambayo yeye na wenzake serikalini waliinunua kutoka kampuni ya BAE systems ya Uingereza, ambayo ililetwa kwa ajili ya kuongoza ndege, lakini wataalamu wa mambo ya anga wanasema kutokana na ubovu wa radar hiyo, siku moja ingeweza kusababisha maafa makubwa sana ya kuanguka kwa ndege, kwenye uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere, Dar-es-salaam, swali tunalomuuliza bwana Feleshi, ni kwa nini hadi leo ameshindwa kumfungulia mashitaka ya ugaidi mzee wa vijisenti,Andrew Chenge, ambapo faili lake alishakabidhiwa na Hosea, na kosa lake lingeweza kusababisha maafa makubwa sana ya watu na mali??!!

Kutokana na maelezo niliyoyatoa hapo juu, ni dhahiri kuwa kuna kila dalili kuwa DPP wetu bwana Feleshi, upo uwezekano mkubwa kuwa anapewa maagizo na wakubwa wa Lumumba, namna ya utendaji kazi wake, ambapo ni kinyume sana na taaluma ya sheria inavyotaka, na ni jambo la dhahiri kuwa kama majukumu yake ataendelea kuyaendesha kwa ukereketwa wake kwa chama tawala, basi siku si nyingi toka sasa, ataondoka ofisini kwake, kwa aibu kubwa, kwani ni lazima akumbuke ule msemo maarufu, unaosema, MWISHO WA UBAYA AIBU!!!!!
 
Kwa mazingira ya kesi ya Mkurugenzi wa Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare, namna DPP alivyomfikisha mahakamani Kisutu, akifunguliwa mashitaka ya ugaidi na baadaye kesi hiyo kufutwa kwa amri ya huyo huyo DPP na baadaye tena Polisi kumkamata tena na kumfungulia mashitaka yaleyale, bila kubadilisha hata kipengele kimoja, inaacha maswali mengi yanayokosa majibu, kama kweli hii ni kesi ya kawaida au ni kesi ya kubambikika, inayotokana na amri za watawala!!

Maswali mengi yanayokosa majibu ni kama, kwa vipi tokea sheria ya ugaidi, ipitishwe nchini mwaka 2002, kwa shinikizo la Marekani, baada ya mashambulizi ya balozi zake mbili, za Nairobi na Dar-es-salaam, mwaka 1998, na lile shambulizi la kutisha la twin towers, jijini New York, ambalo lilipewa jina la september eleven disaster, hakujawahi kufunguliwa mashitaka yoyote ya ugaidi hapa nchini na kwa maana hiyo, kiongozi huyo wa Chadema, ndiyo anakuwa mtu wa kwanza hapa nchini kufunguliwa mashitaka ya ugaidi!!

Sasa tuangalie makosa yanayolengwa kuwa ya ugaidi ni makosa ya aina gani. Ninavyofahamu mimi tafsiri ya ugaidi ni mtu au kikundi cha watu kinapotekeleza kitendo cha uhalifu unaoweza kusababisha maafa makubwa ya watu na mali, ambapo vitendo hivyo vinatokana na chuki za kisiasa au za kidini.

Sasa hebu tuangalie huyu mlengwa wa tukio hili la 'kufikirika' la ugaidi, Denis Msaki, ana nafasi gani kubwa ya kisiasa au kidini hadi awe mlengwa mkuu wa tukio la kigaidi. Katika utafiti wangu, huyo jamaa, ukiacha kazi yake ya uandishi wa habari hana nafasi yoyote kubwa ya kidini wala ia kisiasa.

Hebu tujiulize jambo jingine, sote tunafahamu kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ibara ya 13[1] inakataza kabisa ubaguzi wa aina yoyote wa kisheria inapofikia wakati wa kufungulia mashitaka watu. Sasa tunakumbuka ni mwaka jana tu mwezi wa sita, ambapo Dr Ulimboka alitekwa na kupelekwa kwenye misitu ya Mabwepande ambako aliteswa sana, hadi kutolewa kucha na meno kwa koleo bila kutumia ganzi. Mbona katika tukio hilo, ambalo yeye mwenyewe aliyetekwa anamtaja kwa jina, mtu anayefahamika kama Ramadhan Ighondu, anayefanya kazi Ikulu, ni kwa nini basi Polisi pamoja na DPP wao, hadi leo hawajamfungulia mashitaka huyo jamaa ya ugaidi??!!

Vile vile kwenye kesi huyo kuna mtuhumiwa mmoja ambaye waTZ tunamtambua kwa jina la mtuhumiwa chizi wa Kenya wa Kova, ni kwa nini mtuhumiwa huyo feki wa Kova hakufunguliwa mashitaka ya ugaidi??!!

Kwa mazingira hayo, pamoja na mimi kuijua sheria kwa kiwango kidogo sana ukilinganisha na DPP wetu Feleshi, inamshangaza kila mtu, namna alivyoiendesha kesi ya Lwakatare, watu wengi wakijiuliza, kama ni kweli ametumia taaluma yake ya sheria au amefanya hayo kwa maagizo ya wakubwa wa chama tawala pale Lumumba??!!

Wote bado tunakumbuka jinsi mwezi Desemba mwaka jinsi Mwigulu Nchemba alivyoibuka Star TV na kudai kuwa ana mkanda ambao unaonyesha viongozi wa Chadema wakifanya mipango ya mauaji. Sasa lazima tuwaulize Polisi wetu, je umakini wao upo wapi kama anatokea mtu anadai ana mkanda wa mauaji, halafu wao wamekaa kimya na baada ya miezi mitatu kupita ndiyo wanamkamata mtu na kumfungulia mashitaka ya 'kufikirika' ya ugaidi!!

Ni dhahiri kutokana na maelezo niliyotoa, ni ushahidi usio na mashaka kuwa huu mkanda alioshitakiwa nao Lwakatare, ndiyo mkanda huo huo alioongelea Mwigulu Nchemba, kwani huo mkanda wa Lwakatare tunaelezwa kuwa ulichukuliwa kwenye tarehe za mwishoni mwa Desemba.

Kwa mazingira yanayoonekana hapa, hii kesi ya Lwakatare ni mpango mchafu ulioandaliwa na POLICCM, TISS na CCM yao kwa lengo la kuiangamiza Chadema, sasa kinachoshangaza ni kwa vipi mtu aliyebobea kwenye sheria, kama bwana Feleshi naye anatupungizwa kwenye huo mchezo mchafu wa kisiasa. Ni vyema bwana Feleshi akajitafakari upya ili kazi yake asiingize ushabiki wa kisiasa na kama atapuuzia ushauri wangu basi awe tayari wakati wowoie kuanzia sasa kuondoka ofisi hiyo kwa aibu kubwa!!!

Hongera kwa mawazo mazuri, hii nchi ni ile ya mfalme juha. HIvyo haya ni sahihi kutokea na wanafalsafa kufanya mambo kama haya. Kama kuna Mtu anayeweza kukumbuka vizuri "naomba atukumbushe wakati ule fastjet anaingia kuna kamanda mmoja monduli alijiuzulu kwa kuogopa ya Babu Sea baada ya kukumbuka enzi hizo fat-j akiwa chini yake alifuata sheria na kutaka kumwadhibu baada ya kuitwa na Mwalimu magogoni" Hivyo huenda na huyu anataka kuja kuvaa kiatu kama hicho.
 
Back
Top Bottom