Je, Dawa za mvuto katika mapenzi zina chimbuko la kibiblia?

Jodeo

JF-Expert Member
Mar 10, 2015
1,286
1,328
Ni matumaini yangu kwamba nyote hamjambo na kwamba Mungu anazidi kuwabariki.

Wakuu, katika kusoma vitu mbalimbali wiki hii nimekutana na simulizi moja katika biblia

(MWANZO 30:14-16).

Panasomeka hivi;

" 14 Reubeni akaenda siku za mavuno ya ngano akaona TUNGUJA kondeni, akazileta kwa Lea mamaye. Ndipo Raheli akamwambia Lea, Nipe mimi baadhi ya TUNGUJA za mwanao.
15 Naye akamwambia, Je! Ni jambo dogo kuninyang?anya mume wangu; hata wataka kuzitwaa TUNGUJA za mwanangu pia? Raheli akamwambia, Kwa hiyo atalala kwako usiku huu kwa TUNGUJA za mwanao.
16 Yakobo akaja kutoka kondeni jioni, Lea akatoka kumlaki, akasema, Lazima uje kwangu, kwa sababu nimekuajiri, kwa TUNGUJA za mwanangu; akalala kwake usiku ule"
mwisho wa kunukuu.

Sasa baada ya kukosa maana ya neno TUNGUJA ikabidi niangalie biblia ya kingereza inasema vipi kuhusu TUNGUJA.

1. Biblia ya KING JAMES ikasema TUNGUJA ni mandrakes.
042afc0dca5fc52bc481d7368a6d0c77.jpg

2. Biblia ya Contemporary English Version inasema Tunguja ni " LOVE FLOWERS"

5ca6bd090dd6f46135ef70883baf2fe0.jpg

Baada ya hapo nikarudi tena kwenye hiyo simulizi (Mwanzo 30:14-16). Nikashindwa kupata conclusion kama hizo "LOVE FLOWERS " hawa kina Leah na Rahel walizitumia kama ndumba kumvuta mume wao (YAKOBO) au kuna nini hapo? Maana baada ya Leah kupata "LOVE FLOWERS" tunaona "YAKOBO" anavutika kwenda kulala kwa Leah japo haikuwa siku ya kulala kwa LEAH!

Nachotaka mnisaidie ni je';

A) Tunguja ( Love flowers / mandrakes) zinazotajwa hapo kwenye biblia ni Kitu gani au Ni mimea gani?

B) Je, TUNGUJA (LOVE FLOWERS/mandrakes)
Ni miongoni mwa mimea inayotumika katika mambo ya mahusiano / kuleta mvuto wa kimapenzi?!

Asante.

~Jodeo~
 
Biblia inahitaji tafsiri za kiroho na si za kiakili kuielewa, si kama Abort, Atlas au Nipashe.

Biblia inahitaji msaada wa kiroho au elimu ya theolojia ili kuisoma na kuielewa.

Biblia haisomwi kwa kuchagua kile kinachokuridhisha tu au kujustify kile unachopenda kiwe hivyo utakavyo (Mwl. Christopher Mwakasege alilifundisha vizuri sana hili majuzi)

Mfano:

Wanasiasa huwa wanapenda kuchukua baadhi ya mistari inayowaridhisha na wanapenda watu waelewe vile wanavyopenda wao.

Wewe unataka tuelewe kuwa Limbwata imetajwa katika biblia au?

Ukisoma hiyo mistari kuanzia mwanzoni na kuendelea hapo ulipoishia utaelewa vizuri.
 
Biblia inahitaji tafsiri za kiroho na si za kiakili kuielewa, si kama Abort, Atlas au Nipashe.

Biblia inahitaji msaada wa kiroho au elimu ya theolojia ili kuisoma na kuielewa.

Biblia haisomwi kwa kuchagua kile kinachokuridhisha tu au kujustify kile unachopenda kiwe hivyo utakavyo (Mwl. Christopher Mwakasege alilifundisha vizuri sana hili majuzi)

Mfano:

Wanasiasa huwa wanapenda kuchukua baadhu ya mistari inayowaridhisha na wanapenda watu waelewe vile wanavyopenda wao.

Wewe unataka tuelewe kuwa Limbwata imetajwa katika biblia au?

Ukisoma hiyo mistari kuanzia mwanzoni na kuendelea hapo ulipoishia utaelewa vizuri.
Azarel, habari za limbwata umesema wewe, Mimi sijasema limbwata mahali popote. Na hata ningetaja limbwata, biblia inayo mifano mizuri ya kuigwa na mifano mibaya ya kutoigwa daima. Unachojaribu kusema ni kwamba mifano mibaya haimo katika biblia! Kitu ambacho Si kweli.

Mambo mabaya mengi yameoneshwa katika biblia ili kutuonya ( 1 wakorintho 10: 6-9), kwa hiyo hata ukipinga haiondoi ukweli kwamba yalifanyika.

Naomba unisaidie kama unaujua huo mmea tafadhali.
 
Azarel, habari za limbwata umesema wewe, Mimi sijasema limbwata mahali popote. Na hata ningetaja limbwata, biblia inayo mifano mizuri ya kuigwa na mifano mibaya na kutoigwa daima. Unachojaribu kusema ni kwamba mifano mibaya haimo katika biblia! Kitu ambacho Si kweli.

Mambo mabaya mengi yameoneshwa katika biblia ili kutuonya ( 1 wakorintho 10: 6-9), kwa hiyo hata ukipinga haiondoi ukweli kwamba yalifanyika.

Naomba unisaidie kama unaujua huo mmea tafadhali.
Kabla hatujaendelea na mjadala...Je unaijua Limbwata ni nini?

Ulishasoma habari za kuhusu limbwata?
 
Basi hiyo mbinu ndio itakuwa alitumia Ngwajima kumnasa Mrs Mbasha
 
Hizo tunguja ni mapambo ya nje tuu.....

Mwanamke anatakiwa awe na mapambo ya ndani

Soma 1 petro 3

Pale ndipo biblia inaeleza namna vitu vinavyoweza kuwavutia wanaume. Sio mapambo ya nje Ila Ni mapambo ya ndani mfano

Mwenendo wa mwanamke unatakiwa uwe Safi, na hofu.

1 petro 3:4

Kujipamba kwenu kuwe katika vitu visivyoonekana. Na visivyo haribika yani roho ya upole na utulivu...iliyo ya thamani kuu mbele za mungu.

Nakushauri soma hiyo sura yote, hamna tunguja Ila matendo na mioyo Safi hayo Ni zaidi ya limbwata
 
Kabla hatujaendelea na mjadala...Je unaijua Limbwata ni nini?

Ulishasoma habari za kuhusu limbwata?
Inaonekana wewe umeshazisoma na unazijua vema! Sasa hii thread inataka kujua TUNGUJA (LOVE FLOWERS/ mandrakes) ni kitu gani au ni mmea gani.

Habari za limbwata Anzisha thread wanaofahamu watakujuza.
 
Hizo tunguja ni mapambo ya nje tuu.....

Mwanamke anatakiwa awe na mapambo ya ndani

Soma 1 petro 3

Pale ndipo biblia inaeleza namna vitu vinavyoweza kuwavutia wanaume. Sio mapambo ya nje Ila Ni mapambo ya ndani mfano

Mwenendo wa mwanamke unatakiwa uwe Safi, na hofu.

1 petro 3:4

Kujipamba kwenu kuwe katika vitu visivyoonekana. Na visivyo haribika yani roho ya upole na utulivu...iliyo ya thamani kuu mbele za mungu.

Nakushauri soma hiyo sura yote, hamna tunguja Ila matendo na mioyo Safi hayo Ni zaidi ya limbwata
Muwe mnasoma mada mnaelewa
 
Back
Top Bottom