Je, D Knob alimaanisha nini?

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,015
9,883
NDANI YA MISTARI
BAD MAN - D KNOB FT CANNIBAL

Mtumishi wa Bwana, Innocent Sahani aka kinundu kichafu "Dirty Knob" kwa kifupi D KNOB akiwa na Mla nyama kutoka Mombasani waliangusha dude hili lililoishika Afrika Mashariki lakini kuna mstari mmoja umenifanya niwashirikishe;

D anaifungua stanza ya pili kwa kusema;
"KAMA NINGEKUWA MIMI, NISINGEKUWA MSHKAJI NA MIMI" Dakika ya kwanza, sekunde sifuri.

Nimekuwa na tafsiri mbili hapa;
Mosi, kama yeye angekuwa mtu mwingine basi asingekuwa na urafiki na D Knob. Kwa maana hii, anaona D Knob ana tabia ambazo haziwafai watu mpaka wakafanya urafiki au ushirika naye.

Maana ya pili ni kwamba, anamwambia mtu ambaye ana USHKAJI na NGWEA kwamba kama angekuwa yeye, basi asingekuwa na USHKAJI na NGWEA kwa sababu NGWEA alikuwa anajiita AKA MIMI.

Lakini kumbukumbu zangu zinaonesha kwamba D aliwahi kulumbana na Fid Q tu kimistari na siyo msanii mwingine, sembuse Ngwea!!!
Je D alimaanisha nini?

LUAH ( LENGO, UWEZO, AKILI, HISIA)
 
Nahisi alimaanisha hiyo tafsiri ya Kwanza uliyoitoa

Kuna watu waga Wana msemo unaosema kuwa "kuwa mtu ambae unataka kukutana nae"

Yani kama unataka kukutana na watu wazuri basi anza wewe Kwanza kuwa mtu mzuri ili ufanye mfano wa watu watakaokuja katika maisha yako

Kwahiyo hapo D Knob alimaanisha kuwa yeye sio aina ya mtu ambae anatamani kukutana nae

Kifupi ni kwamba yeye sio Kariba ya mtu ambae sie tunamjua, yeye ni mtu tofauti na ambavyo anaonekana kuwa
 
Anatutisha

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Una mawenge yako tu ndio maana unajipa majibu. Hapo amemaanisha kuwa yeye ni mtu noma sana so wa kuogopwa na kukaliwa mbali.

Kwa kifupi ndio maana wimbo kwenye chorus una kiitikio kinasema "i am a bad man".

Acha overthinking kijana.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom