Je, CUF ni idara ya CCM? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, CUF ni idara ya CCM?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Papa D, Nov 16, 2010.

 1. Papa D

  Papa D JF-Expert Member

  #1
  Nov 16, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mgombea wa kiti cha unaibu spika kupitia CUF alisimama na bila woga akaidhinisha kwamba CUF ina muafaka na CCM na tayari wana dhamira ya kushirikiana, basi anajitoa na kusubiri CCM imuunge mkono kwenye ugombea wa SADC.

  Ujumbe huo umetuonyesha jibu moja kwamba; Kwa sasa CUF ni sehemu ya CCM na kwamba vyama vingine vinapojaribu kujiunga na CUF vitambue vinajiunga na CCM pia. Kwa mazingira hayo Mgombea wa naibu spika kupitia CHADEMA alitakiwa aonyeshe msimamo wa chama kuhusu matokeo ya Urais bila kujaribu kuonyesha aina yeyote ya diplomasia.


  Ningekuwa mimi ndiye Akonaay [Mgombea wa CHADEMA] ningemjibu muuliza swali wa CCM Hivi:-

  Ø Ni kweli Chama changu hakiyatambui Matokeo ya Urais yaliyotangazwa na NEC kwa kuwa si matokeo halisi ya vituoni mfano jimbo la Gairo matokeo ni Kikwete kura 239,102 na Slaa kura 174,500 lakini NEC ilitangaza kura 194,108 kwa 41,439. Hali hii ipo ktk majimbo mengi ya uchaguzi. Kutokana na hali hiyo naungana na Mgombea wa CHADEMA Dr. Wilbroad Peter Slaa Sambamba na CHADEMA katika maamuzi yao ya Kutotambua Matokeo hayo hivyo kutotambua ushindi wa ndugu Jakaya Mrisha Kikwete.

  Ø Mimi kama Naibu Spika ntaongoza kwa kufuata Kanuni za Bunge wala si kanuni za CHADEMA, CUF, TLP, NCCR-Mageuzi, CCM, Mahakama au Serikali. Kanuni za Bunge hazifungamani na taasisi nilizozitaja.

  Ø Isitoshe Kutambua au kutotambua ushindi wa Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete hakufungamani na kanuni yoyote ya kuongoza bunge hili kwani hakuna kipengele kinachomtaja mshindi wa Kura za Urais na nafasi yake katika kuongoza Bunge.
   
 2. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #2
  Nov 16, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Una mawazo mazuri sana ndugu, nimekuwa disappointed mno na CUF, hawajui kwamba CCM watawatumia kama condom kisha wakiishiwa hamu inatupwa!
   
 3. October

  October JF-Expert Member

  #3
  Nov 16, 2010
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 2,147
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Cuf inasikitisha. imepoteza uaminifu kwa watanzania
   
 4. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #4
  Nov 16, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,690
  Trophy Points: 280
  Asubuhi nilimwona Hamad Rashid Mohamed mbunge pekee wa CUF niliyekuwa namheshimu kupita maelezo, lakini leo ameweza kumaliza hadi ile heshima ya mwisho nliyokuwa nayo kwake.

  Alikuwa anahojiwa na Tom Chilala anasema eti, hawezi kuungana na CHADEMA kwa vle Zitto Kabwe alitangaza hata kabla ya Uchaguzi kuwa CHADEMA itaunda upinzani, pia CHADEMA walimpiga mgombea wa CUF Kigoma Kaskazini. Pia, hawawezi kuungana na CHADEMA kwa vile vipo vyama vyenye wabunge mmoja mmoja na CHADEMA hawaviamini ila wao wanaviamini, akasemma tena CHADEMA wana ugomvi na vyama vyote vya upinzani (isipokuwa wao) hivyo hawawezi kuungana kwa sasa labda baadae.

  Akasema pamoja na Mh. Lyatonga kuwa na afya mgogoro na anaelewa hataweza kurudi katika hali ileile ya kisiasa kama zamani lakini ni bora kujiunga nao kuliko CHADEMA.

  Mwenye akili atajua tu kuwa huu ni mkakati wa CCM wa kuudhoofisha upinzani hasa wa CHADEMA unaoundwa na vijana wenye uelewa, maono, confidence na uwezo kwa kugundua mbinu zao chafu.

  CUF = CCM= NCCR MANUNUZI= TLP = UDP=UPDP
   
 5. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #5
  Nov 16, 2010
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Mkuu naomba kuuliza ni jimbo gani hilo la Gulou? Uko mkoa gani ni mara ya kwanza kuisikia :hippie:
   
 6. C

  Chumvi1 Senior Member

  #6
  Nov 16, 2010
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 137
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  kwani ulikuwa hujui kwamba CUF kwa sasa ni sehemu ya ccm? Pole ukweli ndio huo hawa jamaa ni wanafiki si wapinzani waende zanzibar huko we chama cha muda mrefu kinapata kura laki sita na kitu.shame on you CUF
   
 7. m

  mosesk Member

  #7
  Nov 16, 2010
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni ngumu sana CUF kuungana na CHADEMA kama vile Ngamia kupita kwenye tundu la sindano. Nashangaa watu wamekuwa wakilalamika kwamba CHADEMA haitaki kuungana na vyama vingine lakini ukweli upo wazi siyo rahisi. Watu wanasahau kiuwa Zanzibar ni sehemu ya muungano kwa hiyo CUF haiwezi kuingia kwenye muafaka Zanzibar halafu wawe tofauti Bara. Na isitoshe wabunge asilimia 90 ya wabunge wa CUF wanatoka Zanzibar kuna mawaziri 7 na makamu wa Rais kutoka CUF wapo na wanafanya kazi na CCM.

  Kuna siku niliandika maoni yangu kupinga muungano wa CHADEMA na CUF na hata NCCR-M na TLP, hakuna sababu na wala kwa kufanya hivyo hakuleti nguvu yoyote kwenye vyama vya upinzani. Kwa sababu kila chama kina sera, Dira na malengo yake, huwezi kuunganisha watu ambao kwa hawana sera na dira moja.

  Labda kwa taarifa CUF na CCM ni ndugu watoto wawili baba moja ila mama mbalimbali, sasa wamerudi pamoja kuna cha ajabu hapo?. Kwa mtu anayefuatilia siasa za bongo vizuri sana kujua hilo. Watu wasishangae na wasikate tamaa, sasa hivi kazi imekuwa rahisi zaidi Chama cha upinzani wa kweli kimebaki kimoja - CHADEMA. Kwa wale wenye mapenzi mema ni vizuri kukisaidia kikakua na baadaye kikachukua madara ya DOLA.

  Wala watu wasipoteze muda kufikiri mambo ya muungano ambao hauwezi kutokea na ambao hauna tija.

  Mimi katika kusoma historia hasa ya bara la Africa katika miaka hii sijawahi kusoma ama kusikia muungano wa vyama hasa vya upinzani vilivyoungana na kuzaa matunda. Vinaweza vikaungana sawa na vikachukua dola lakini mwisho wake inakuwa vurungu na wananchi wanabaki hoi.

  Tunataka mabadiliko ya kweli na siyo ujanja ujanja wa kuungana kwa malengo ya kuchukua madaraka huku dhamira na malengo siyo kuwasaidi wananchi wa kawaida.
   
 8. akashube

  akashube JF-Expert Member

  #8
  Nov 17, 2010
  Joined: Dec 24, 2009
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Mimi ni Chady na niko vitani napambana na jitu mla watu, tuko porini tunatafutana, nimeliona jitu hili lakini lenyewe halijaniona, nina rifle yangu yenye kiona mbali, nimeweka shabaha tayari kwenye kichwa chake, hili jitu linaitwa Cicy,...tatizo ni kuwa kila nikichungulia kwenye kiona mbali simwoni Cicy bali namwona rafiki yangu Kufu. Nikitoa jicho kwenye kiona mbali namwona Cicy, nikirudisha jicho tayari ku-shoot namwona Kufu.

  Hivi mpaka dakika hiyo nimepoteza muda wa mapambano kiasi gani? Je thamani ya muda unapopata shabaha hadimu katika vita inaweza kupimwa kwa mizani gani?????

  If you want my opinion dude...JUST SHOOT THE FUCKER!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 9. Papa D

  Papa D JF-Expert Member

  #9
  Nov 18, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  ndugu susuviri!
  Nilichukua muunganiko wa herufi ili kutolea mfano tu! Sikupenda kuchukua jimbo halisi nikihofua kupoteza maana ya neno kwamba "nigekuwa mimi ndiyo akonaay" kwa lugha nyingine nimejifanya mgombea wa bunge la kufikirika katika jimbo la kufikirika!
   
 10. Papa D

  Papa D JF-Expert Member

  #10
  Nov 18, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  hofu yange kwa anayoyafanya CUF ni kujijengea utumwa ndani na himaya yake mwenyewe. Maana CCM ni mithili ya CIA wanakutumia wakishamaliza they dump you!. CCM walishaona nguzo ya CUF ni Maalim Seif na weakness ya Seif ni madaraka yaani anapenda madaraka. Mtu anayependa madaraka huhakikisha anaficha aina zote za kashfa. kwa hiyo CCm watamjengea Kashfa moja kubwa na kuwa silaha yao kwani kila wanachokitaka watamwambia akifanye na akikataa wanatishia kutangaza kashfa yake. thats will be the end of everything! INDEED kwa kukubali kuwa makamu wa kwanza wa Rais ndio ulikuwa mwanzo wa Mwisho wake na CUF kwa ujumla wake! You Guys Mark my word 2015 hatapata hata viti ishirini vya Ubunge!
   
 11. T

  The Infamous JF-Expert Member

  #11
  Nov 18, 2010
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 719
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  chama cha upinzani kwa sasa ni kimoja tu chadema..cuf wameshajitoa na wamejiunga na ccm, hata bungeni wanaisapoti ccm...mi nadhani sasa ni poa tayari tumejua mamluki wapi wanaharakati wapi
   
 12. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #12
  Nov 18, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,586
  Likes Received: 4,693
  Trophy Points: 280
  CUF wamepewa agizo na Kikwete kuwa kwa vile M/kiti na K/mkuu wa Chadema ni wakristo waiogope Chadema kama ukoma, kwa vile hawa wameolewa lazima watii amri ya mume, ukikubali kuolewa................
   
Loading...