Hatimaye siku zinazidi kujongea kufikia siku ya uchaguzi mkuu Oct 31, ni siku takribani 11 zimesalia kwa waTanzania kwenda kutumia haki yao ya kikatiba kuchagua viongozi wao katika ngazi mbali mbali kuwaongoza, kuanzia udiwani, uwakilishi(znz),ubunge na urais
Kama kawaida kambeni zinaendelea kwa utulivu wa hali ya juu ukiondoa rabsha ndogo ndogo za hapa na pale ambazo ni zakawaida
Mtazamo wangu upo zaidi upande wa bara na hasa vyama hivi viwili vinavyoonyesha kukinzana kwa hali ya juu CCM na CHADEMA
CCM kwa upande wao wanaendelea na kampeni zao za nguvu za lala salama kwani sasa hatusikii tena siasa za maji taka za kushambuliana binafsi kama ilivyokuwa mwanzo
Kwa upande wa CHADEMA nao wanaendelea na kambeni zao majukwaani kwa bidii zote lakini kwa wakati huo wanapandikiza chembe chembe mbaya sana akilini mwa wananchi kwa kujitahidi kuwaaminisha kile wanacho fikiri kitawasaidia wao bila kujali maslai ya taifa.
Kumekuwepo na juhudi kubwa sana inayoendeshwa na CHADEMA kuwafanya wananchi waamini kuwa CHADEMA inaonewa, na mbaya zaidi inapangwa kuwa NILAZIMA KURA ZITAIBIWA ili kuipoka ushindi na kuipa CCM, rejea post yangu ya awali -chadema-na-mbinu-ya-lawama-kupata-huruma.
Naliandika hili hapa JF kwakuwa member wengi humu wamekuwa wakiandika habari za uchochezi kwa kuzusha habari zisizo na kichwa wala miguu, kwa kudai kuwa CCM imekuwa ikifanya hujuma mbali mbali dhidi ya chadema.
Kama ni mfuatiliaji mzuri wa post nyingi zinazo anzishwa na kupata wachangiaji wengi kwa muda huu basi ni zile ambazo zina lengo la kuonyesha kuwa Tayari CHADEMA wameshinda na CCM inajaribu kupoka ushindi huo
Post hizo zimekuwa zikitoa taarifa mbali mbali kwamba CCM inatumia kila namna ku poka ushindi wa Chadema. Habari kama za karatasi za kura Tunduma, Serikali kuingia mkataba na nchi fulani kusidia kuchakachua matokeo, kutokubali na kukosoa kila maelekezo yanayo tolewa na tume,kama idadi ya wapiga kura,idadi ya wapiga kura kwa kila kituo, na madai ya kutaka kuahirisha uchaguzi na mengineyo mengi kama hayo.
Tuhuma hizo zinaweza kuwa na athari kubwa kwa watu kwa kuziamini kuwa ni za kweli
Je madai kama haya yanamuandaaje mwananchi pindi matokeo yatakapo toka?
Katika chaguzi kuna kushinda na kushindwa na hii ndio siasa, lakini sasa CHADEMA wanatuaminisha kuwa ushindi kwao ni lazima na hii haina mjadala kwao,na uchaguzi huu utakuwa huru na haki tu pale wao watakaposhinda, vichwani mwao wameondoa kabisa ile dhana nzima ya kushinda au kushindwa, na hivi ndivyo wanataka mwananchi aelewe hivyo
Hatari iliyopo ni pale matokeo yatakapo toka na kuwa tofauti na mwananchi huyu alivyo aminishwa na kuandaliwa kuwa ushindi ni lazima kwa CHADEMA, bila kujali kama imeshindwa kwa mujibu wa kura halali zilizo pigwa
Kwenda kwenye uchaguzi ilihali ukiwa tayari na mentality ya kushindwa na kuanza kutumia nguvu ya umma kujihalalishia ushindi kabla ya uchaguzi nia tabia hatarishi kwa usalama wa amani ya nchi yetu, na unapaswa kuepukwa
Tabia ya kuwafanya watu wajiandae na ushindi bila kujali uhalisia wa kura ni namna moja ya ujinga wa kutaka kujipatia usicho stahili bila kujali kuwa panaweza kutokea machafuko ambayo yataathiri badala ya kujenga
Kwa maana nyingine CHADEMA inawaandaa wananchi kuwa pindi matokeo yatakapo toka na CHADEMA kushindwa basi wananchi wasikubaliane na matokeo, na sote twajua nini maana yake ikitokea hivyo. machafuko kudai haki
CHADEMA wanapaswa kufahamu kuwa pamoja na mambo yote wanayo ituhumu CCM kuiharibu nchi hii kwa ufisadi nk, kuwa hicho sio kibali cha wao kushinda uchaguzi hata kidogo, demokrasia itabaki pale pale kuwa wananchi ndio watakao amua
Na itakuwa kosa kubwa sana kama CHADEMA watadhania ufisadi ndio mtaji wao pekee wa kuwaingiza ikulu bila kuzingatia nguvu ya CCM, CCM ni organization kubwa yenye mtandao mkubwa sana hasa vijijini, CCM ni tofauti na vyama vya nchi nyingi vilivyoshindwa kirahisi na upinzani kama KANU nk
Issue ni kuwa je CHADEMA walifanya nini na wanafanya nini kuikabili ngome ya CCM na kuwashawishi wananchi wawaamini ili kuwapa kura badala ya kuwapa CCM?
Jibu ni baada ya Oct 31
Paulss