Je CCM imetoa rushwa nchi nzima? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je CCM imetoa rushwa nchi nzima?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by QUALITY, Oct 12, 2010.

 1. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #1
  Oct 12, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  JE RUSHWA NI NINI?
  Mwaka huu, takukuru walitoa bango ambalo nilibahatika kulisoma limetoa tafsiri ya Rushwa katika uchaguzi kama ifuaatavyo.
  1. utoaji wa fedha
  2. Utoaji wa T-shirt
  3. Vitu vya thamani

  Ambavyo vinaweza kumshawishi mpiga kura ampigie kura mgombea. Je CCM wanapotoa T-shirt nchi nzima, ni rushwa au siyo Rushwa? Kama ni rushwa, kwani TAKUKURU hawachukui hatua madhubuti na kutamka wazi kuwa CCM imetoa rushwa nchi nzima na kwa hiyo iondolewe katika kampeni?

  Tafakari, chukua hatua.
   
 2. J

  Jafar JF-Expert Member

  #2
  Oct 12, 2010
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Waliniletea Kofia , T-Shirt, Kitenge na ki-bendera - sharti ni kuwa ukivipokea lazima uende kwenye mkutano wa JK. Nikawaambia enendeni na zawadi zenu mshindwe na mnyong'onyee. Nikagundua kumbe umati ule sio wote ni CCM bali ni njia ya kupata T-Shirt, Kofia na Vitenge.

  Kama kweli wanakubalika mbona gharama kubwa ya kampeni??????????????? wanamshawishi nani wakati wanakubalika ??
   
 3. akashube

  akashube JF-Expert Member

  #3
  Oct 12, 2010
  Joined: Dec 24, 2009
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Pia ukumbuke JK anatumia 'Iddi Amin Economic Theory' akiamini kuwa 'all the resources in the country are for CCM and that budget concerns are only when it comes to free education. CCM can spend as extravagantly as satanically possible and no constraints at all'.

  Matumizi yanayokubalika kwa CCM na ambayo hayaathiri bajeti kwa mtazamo wa CCM ni

  1) rushwa kubwakubwa na ndogo ndogo, tshirts, pilau, khanga, usafiri wa fuso, d/coaster kwenda mikutanoni, elfu kumi nyumba kwa nyumba, vibali hewa vya biashara, kulindiwa unga usimwagwe(kazi), ukuu wa wilaya( Nape Nnauye), viti maalum, kofia ishirini za uongozi....n.k naweza jaza kurasa bilioni. YOTE ILI MURADI TU CCM ISHINDE.

  2) mafunzo ya kijeshi yasiyo ya lazima; mfano kuliandaa jeshi JWTZ kupambana na wapiga kura badala ya kulinda mipaka, kununua vifaru na ndege za kivita ili vitumike manzese, mwanjelwa, kirumba, tambuka reli, mianzini, soweto, kariakoo, igogo, hamugembe na kwingineko ambako wananchi hawadanganyiki.

  3) Rais kusafiri na ujumbe wa watu 100 kwenye mikutano ambapo nchi kubwa marais wao wanakwenda na ujumbe wa watu 6,


  Serikali ya CCM ina uwezo wa kutoa rushwa Afrika nzima, lakini bajeti yao haitoshi kusomesha hata mtoto mmoja wa masikini bure, na watetezi wao humu wanadai watoto wa maskini wamejitakia kuwa hivyo kwa kuwa wamebweteka wanasubiri kusaidiwa. Kweli CCM ni Chama Cha Mashetani.
   
 4. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #4
  Oct 12, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,377
  Likes Received: 3,140
  Trophy Points: 280
  Watz wanakula pilau na kunywesha pombe za kienyeji na ccm kila baada ya miaka mitano
   
 5. akashube

  akashube JF-Expert Member

  #5
  Oct 12, 2010
  Joined: Dec 24, 2009
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Halafu rushwa haina risiti, sijui mkaguzi mkuu baada ya uchaguzi atakagua nini.
   
 6. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #6
  Oct 12, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Kama furana,kofia na vtenge walipewa, bule basi hiyo ni rushwa kabisa!kwa kuwa navyofahamu mimi baadhi ya vitu hivi, vinauzwa pale Ofisi za CCM -Lumumba!
   
Loading...