Je CCJ wamechezewa rafu au ni uzembe wao?

Chapakazi

JF-Expert Member
Apr 19, 2009
2,874
310
Ningependa kuanzisha hii thread kwa ajili ya kuangalia kwa undani huu uhakiki wa CCJ!
Gazeti la Rai...tarehe 2 June 2010
Msajili kuanza rasmi kuihakiki CCJ kesho
Mwandishi Wetu Juni 2, 2010
HALI ya mkanganyiko imezidi kujitokeza serikalini kuhusu uhakiki wa wanachama wa Chama Cha Jamii (CCJ) kinachohitaji usajili wa kudumu; huku viongozi ofisi ya Waziri Mkuu wakisema uhakiki hauwezekani kwa sasa, lakini sasa imebainika ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa imekubali kuanza uhakiki kesho, Alhamisi, wiki hii. Taarifa ambazo Raia Mwema imezipata Mei 31, mwaka huu, zinasema kuwa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa inayoongozwa na John Tendwa, ilifanya mazungumzo na viongozi wa CCJ, saa nane mchana, katika ofisi hizo na kupendekeza kuwa uhakiki uanze kesho Alhamisi ya Juni 3, kwa Jiji la Dar es Salaam na kuendelea katika mikoa ya Pwani na Mjini Magharibi, ikiwa ni awamu ya kwanza.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotufikia mapema wiki hii, mkoani Pwani uhakiki wa wanachama wa CCJ utafanyika Juni 4, mwaka huu, wakati mkoa wa mjini Magharibi, Unguja uhakiki utafanyika Juni 9, mwaka huu.
Tayari uongozi wa CCJ umemwandikia barua Msajili wa Vyama Vya Siasa ili kukubaliana na uamuzi huo. Barua hiyo imeandikwa Mei 31, mwaka huu.
Kabla ya kukubalika kufanyika kwa uhakiki huo, Tendwa aliwahi kueleza kuwa hana bajeti kwa ajili ya uhakiki wa wanachama wa chama hicho na kwamba kwa sasa ofisi yake imewekeza muda na rasilimali zaidi katika suala la Uchaguzi Mkuu, na hasa kusimamia Sheria mpya ya Gharama za Uchaguzi.
Lakini pamoja na Tendwa kueleza hivyo, hivi karibuni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Philip Marmo naye alieleza kuwa uhakiki huo hautawezekana kutokana na kutokuwapo kwa fedha na kwamba ni suala lililojitokeza baada ya bajeti kupangwa.
CCJ awali kilikuwa kikihusishwa na baadhi ya vigogo waliomo katka CCM ambao wamechoshwa na hali ya mambo nchini kutokwenda sawia na hivyo kuamua kujitoa na kuanzisha vuguvugu jipya la siasa za kusaka maendeleo kwa kasi zaidi.
Hata hivyo, vigogo mbalimbali waliokuwa wakihusishwa na chama hicho kwa nyakati tofauti walikana hadharani huku taarifa nyingine za ziada zikieleza kuwa waliendelea kuwa na mawasiliano ya karibu na chama hicho.
Mmoja wa viongozi aliyetoka CCM na kujiunga na CCJ ni aliyekuwa Mbunge wa Kishapu, Fred Mpendazoe, ambaye alijivua ubunge, sambamba na uanachama wa CCM, akisema chama hicho kimepoteza dira na hajutii kujitoa.
Mpendazoe kwa sasa anatajwa kuwa msemaji wa CCJ chenye makao yake makuu kwa sasa eneo la Mwananyamala, jijini Dar es Salaam.
Fact ya kwanza:

  • CCJ hawakushtukizwa katika uhakiki

Uhakiki CCJ vurugu tupu -
PAMOJA na juhudi za Chama Cha Jamii (CCJ) kulazimisha kupewa usajili wa kudumu, jitihada hizo zinaonekana kugonga mwamba baada ya kazi ya uhakiki wa wanachama wake kugubikwa na vurugu mkoani Dar es Salaam, huku uongozi ukitangaza kusitisha kazi hiyo.

Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa anayeendesha kazi ya uhakiki huo pamoja na watendaji wake wawili, jana alisema kuwa kazi hiyo itaendelea leo na kesho katika mikoa ya Pwani na Morogoro, na kama wanachama hao hawataonekana ‘mchezo umekwisha.'

Kazi hiyo ya uhakiki imeingiwa na dosari baada ya Msajili Tendwa kusema kwa wanachama wa CCJ kwa Mkoa wa Dar es Salaam, ni 13 tu ndio halali baada ya uhakiki kati ya watu 26 waliokuwa na kadi za uanachama. Msajili alipewa fomu yenye majina 247 na watu waliojitokeza jana si zaidi ya 110.

Ili chama kipate usajili wa muda, mojawapo ya masharti ni kuwa na wanachama 2,000 kwa mikoa 10 ya Tanzania na kati ya hiyo, miwili ni lazima iwe ya Tanzania Zanzibar.

Viongozi wa CCJ wamekuwa wakilazimisha kupewa usajili wa kudumu na Msajili wa Vyama huku wakisema idadi ya wanachama kwa nchi nzima inafikia 20,000 na kufikia hatua ya kumtaka Tendwa kutamka kiwango cha fedha anachohitaji kwa ajili ya kukamilisha kazi hiyo ya uhakiki.

Tamko la Tendwa alilitoa jana katika viwanja vya Mwembeyanga wilayani Temeke, ambako ndiko kazi ya uhakiki ilikokuwa ikifanyika na baada ya uhakiki, wanachama walianzisha fujo zilizoambatana na kelele huku wakisukumana baina yao na viongozi kwa kutoelewa kilichokuwa kikiendelea.

Tendwa alipoingia Mwembeyanga, wanachama wa CCJ walionekana wakiwa katika makundi huku wengine wakiendelea na kazi ya kuandikisha wanachama wapya na kuwapa kadi ambazo walitakiwa kuzihakiki mbele ya Msajili.

Kazi ilianza kwa kila mwanachama kupita mbele ya Msajili aliyekuwa ameongozana na watendaji wake wawili ili kusoma majina yaliyokuwa kwenye fomu na mwingine kurekodi majina yaliyohakikiwa.

Wakati kazi hiyo ikiendelea, Msajili alibaini kuwepo kwa wanachama wengine wakiwa na jinsi ya kike huku wakionesha kadi ya mwanamume, tena wakiwa ni wakazi wa eneo jingine.

Akizungumza, Tendwa alisema jambo la kushangaza wakati wa uhakiki, viongozi wakuu wa CCJ, Mwenyekiti Richard Kiyabo na Katibu Mkuu Renatus Muabhi walifika bila kuwa na kadi zao na majina yao kutoonekana katika fomu za kujiandikisha; jambo ambalo alidai ni udanganyifu wa kidemokrasia.

"Nimewasamehe viongozi hao kwa kutofika na kadi zao kwa kuwa ni waanzilishi wa chama, lakini pia ninashangazwa na majina ya kadi 26 kutokuwepo katika orodha ya fomu kati ya majina 247 niliyoletewa," alisema Tendwa.

Tendwa alimtaja mwanamke aliyetambuliwa kwa jina la Joyce mkazi wa Kibonde Maji, Mbagala, aliyefika na kadi iliyokuwa na jina la John Mwamba mkazi wa Mwananyamala akidai kuwa ni kadi yake aliyopewa baada ya kujiandikisha huku Anzurunely Lisas na Sospeter Chomala, walipewa kadi katika muda wa uhakiki; jambo ambalo Msajili aliliona ni ubabaishaji wa chama hicho.

Wanachama wengine kama Halima Mohamed mkazi wa Mwananyamala, alibeba kadi hiyo huku akisema ni mkazi wa Mbagala na Joyce Pastory alibeba kadi ikidai anaishi Mbagala, lakini katika fomu imeandikwa kuwa anatokea Yombo Vituka.


Aidha, Mwenyekiti wa CCJ, Kiyabo akizungumza kwa jazba, alisema kazi hiyo imehujumiwa hivyo kusitisha uhakiki kwa mikoa yote hadi hapo watakapokuwepo waangalizi wa kimataifa na vyama vya hiari kwa madai Msajili ana nia ya kutosajili chama hicho.

"Hatuwezi kuendelea, tunahitaji vyama vya hiari na waangalizi wa kimataifa wawepo katika kazi ya uhakiki ili kujenga heshima kwa nchi na kwa chama chetu, tunakosa imani na Msajili," alidai Kiyabo.

Hata hivyo, akijibu hoja ya kusitisha uhakiki, Tendwa alisema amesitisha kwa Mkoa wa Dar es Salaam na kwamba leo ataendelea na kazi hiyo kwa Mkoa wa Pwani katika Wilaya ya Kibaha eneo la Picha ya Ndege na kesho atakuwa Ifakara, Morogoro na kwamba wasipoonekana ‘mchezo umekwisha.'

"Hatufanyi uhakiki mara mbili, ni mara moja tu, tutaenda katika maeneo yaliyopangwa na wasipofika mchezo umekwisha," alisema Tendwa.

Alisema hafanyi hivyo kwa kuwa awali aliwapa viongozi wa CCJ miezi sita kuanzia Machi 2, mwaka huu wa kujiandaa ili wapatiwe usajili wa kudumu, lakini kabla ya muda huo kumalizika, mwezi uliopita, walifika kwake na kudai wako tayari kwa uhakiki na Dar es Salaam pekee, kuna wanachama 7,000.

Katibu Mkuu wa CCJ, Muabhi alisema tatizo la kadi limetokana na wizi wa fomu 50 aliofanyiwa Mwenyekiti wa chama hicho eneo la Kariakoo mapema Machi mwaka huu.
Fact ya pili:

  • CCJ hawakuwa tayari kuhakiki majina!
To consider:

  • CCJ ilikuwa haina wafuasi wa kutosha????
  • Nani mwongo hapa - Kati ya CCJ na Tendwa?
Point ya Zitto:
"Nadhani tatizo ni CCJ kwa kiasi kikubwa......
Majina ya kuhakikishwa huletwa na Chama chenyewe. Sasa hata huyo mwenyekiti wa CCJ hakuwa na kadi ili ahakikiwe anasema eti alipoteza wakati amenigwa pale Kariakoo (angeweza kuchukua kadi nyingine kwa mujibu wa taratibu za chama chao kwa kadi zinazopotea madhali alitoa taarifa polisi). Huyo Katibu Mkuu wao pia hakuweza kuhakikiwa. Hata wangehakiki watu wote pale Mwembe Yanga bado wasingefika 200! Huoni kuwa tatizo ni CCJ?

Kitu kimoja katika siasa za Tanzania, unapokuwa mpinzani unapaswa kuwa makini sana sana. CCJ wlaikwenda kuzindua chama MwembeYanga. Mpendazoe alikwenda kuchukulia kadi mwembe yanga. MwembeYanga ni TEMEKE na Temeke eneo la CUF. Kwa vyovyote vile kama CCJ hawakushirikiana na CUF (na ninaamini hivyo maana walijiona wao ndio wakombozi na kazi nyingine iliyofanywa na vyama vya upinzani toka mwaka 1992 ni bure) basi CUF ilipandikiza watu katika uanachama na ndio hayo yamewakuta. Hiyo ni Dar mtaona kwingine.

I have an experience with this. Mwaka 2007 CHADEMA tuliweka Mgombea Ubunge katika Jimbo la Tunduru baada ya Akukweti kufariki. Tunduru ni CUF strong hold lakini CHADEMA 'tuliamini' kuwa tunaweza kufanya mabadiliko. CUF walilalamika sana na hatukuwasikiliza. Wakaweka mtego. Kila kata tuliyokwenda wanachama wa CUF ndio walitupokea, wakachukua kadi za CHADEMA na kuunda uongozi na timu za kampeni. Tukafanya kampeni kabambe kabisa with a modern information system (ambayo pia tulitumia Tarime na chaguzi nyingine zote na hivyo kuwa chama cha kwanza kupata matokeo mapema kama tunashinda tunazuia wizi wa CCM).

Uchaguzi ukafika. Watu wakapiga kura. Tukapata kura 2000 tu. Kumbe watu wote tuliokuwa tunafanya nao kazi ni CUF na hawa 2000 kwa kweli ndio haswa walikuwa wafuasi wa CHADEMA kule Tunduru.

This is how CUF safeguard ngome zao. CCJ inaweza kuwa Hoax kama alivyosema Tendwa."
Point ya Mwanakijiji:
tatizo liko kwa Msajili.. na watu hawataki kuona tatizo hilo kwa sababu wanapenda kweli tatizo lingekuwa kwa CCJ.

Nilikesha jana kufuatilia suala hili kutoka pande zote na jaribio la msajili ni "kufanya uhakiki hewa" wakati tayari ameshafikia uamuzi. Hili ndilo lilikuwa lengo la kutoa kauli tofauti kati yake na Marmo (ambaye msajili yuko chini yake) ndani ya masaa 24. Lengo lilikuwa ni kuwachanganya wananchi na hivyo kutokutoa muda kwa CCJ kuwaandaa wananchi na kuelewana mfumo.

a. Msajili alisema hana fedha za kufanya uhakiki.. hakuna mtu anauliza hizi za sasa zimetoka wapi?
b. Walisema uhakiki hautafanyika na kuwa CCJ haitashiriki uchaguzi .. sasa wanafanya uhakiki ili kiwe nini?

Wengi humu mnaposikia "uhakiki" hata hamuulizi umefanywaje hadi kuzua malalamishi. Mnachukulia tu kuwa watu wamelalamika bure.

Nimefafanua sehemu nyingine labda nirudie hapa:

Msajili alitakiwa kufanya uhakiki wa wanachama 200 wa mkoa wa Dar.. kaenda Mwembeyanga na kukuta kuna wanachama wa kutoka matawi mbalimbali ya mkoa wa Dar. Yeye kachukua orodha ya watu wa maeneo ya Mwembeyanga na ni HAO TU ndio alioataka kuwahakiki. Wanachama wa CCJ kutoka sehemu nyingine wamekataliwa kwa sababu majina yao hayakuwepo kwenye "orodha ya mwembeyanga".. Hakutaka kuchukua orodha ya sehemu nyingine za Dar kulinganisha! Sasa anapotangaza kuwa watu hawapo kwenye orodha au majina yao hayaonekani ni kweli - in the wrong orodha.

Hii ndio sababu ya uongozi wa CCJ kutaka zoezi lisitishwe kwani "uhakiki wa mkoa" unapofanyika kama uhakiki wa kitu kimoja kunapoteza kabisa dhana nzima ya uhakiki. Cha kuudhi kama kawaida vyombo vya habari vimerudia tu kile kilichoripotiwa na Msajili baada ya kwenda kuuliza maswali ya muhimu kujua nini hasa kimetokea.
Kilichonivunja mbavu: (kimesemwa na Zitto)
Hujanielewa na kwa kuwa umeshahukumu wala siakusaidia kuelewa. Hapa nimeonesha jinsi vyama makini kama CUF vinavyolinda ngome zao. Niseme tu kuwa, to me CCJ was a threat to CHADEMA and other opposition parties. I better get rid of it. We dont need an emerging party every new election. We need existing parties to consolidate. To me i go for CHADEMA, CUF and NCCR-M and the civil society. New parties? i dont have that luxury
kazi tunayo....hahahhaha
 
Back
Top Bottom