Wakuu, I salute you,
Nilileta thread nikirejea jinsi inavyowezekana Mh. Zitto Kabwe akafukuzwa ubunge wake mara mkutano wa bunge uanzao wiki ijayo utakapoahirishwa.
kwa urahisi waweza kuirejea thread hiyo hapa:
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...okuhudhuria-vikao;-hasaini-kupokea-posho.html
Mmechangia kama kawaida yetu na wengine wengi zaidi ya 1,000 wamesoma thread hii. Great.
Kumewahi kuwa na hoja kwamba waandishi wa Tanzania wanaitumia JF kama source. Baadhi ikaelezwa kuwa hili si tatizo japo wengine hawaonyeshi appreciation kwamba JF ndiyo source ya habari zao ambazo zinanunulika.
Sikushangaza thread hii kutoka kwenye magazeti. Magazeti ya leo yaani
HABARI LEO na
THE AFRICAN wametoa kama nilivyo-post humu.
HABARI LEO wametumia maneno "
mdadisi au wadadisi " kila waliponukuu . sina matatizo na hili kama tunaleta hapa thread halafu tunaitwa wadadisi, ni kweli sisi ni wadadisi na tunastahili sifa hiyo. Sasa sijui kwa nini mwandishi wa HABARI LEO asiitaje Jamii Forum kama moja ya chanzo, maana asilimia kubwa ya wanavyosema hao wadadisi wake ni kilekile nilichosema kwenye thread ile.
Pamoja na hayo sina tatizo sana na hao HABARI LEO kwa hiyo intended or inadvertent overlook. Shida yangu kuu ni jinsi
THE AFRICAN walivyoiandika.
THE AFRICAN wamekopi vilevile lakini kilichonishangaza ni wao kutoitaja kabisa
JAMII FORUM na badala yake wanataja kwamba imejadiliwa na
"WANABIDII FORUM" .
Hii maana yake nini? Maana yake ni kwamba msomaji asiyeijua JAMII au WANABIDII basi kwa kusoma gazeti hili anapata akili kwamba kumbe WANABIDII kumefurika vichwa vinavyjua kufikiri hata kama mwanzoni alikuwa anapuuzia Social media. Kwa namna moja WANABIDII imepigiwa marketing or campaign stratergy na JAMII FORUM tulioleta post hii tusiposhtuka bai sifa zetu zitaenda kusiko.
Nimeleta thread hii ili wenzagu tuione concern hii na tunaweza kupata mawazo zaidi ya kupambana na hali hii.
Sina upenzi wa kudumu wa chama chochote. Lakini ni mara nyingi JF imekuwa ikibezwa kuwa ni "
mtandao wa CHADEMA". Moderators wanajua zaidi walivyohangaika kukanusha hilo na baadhi humu mkafikia kutaja majina ya wana CCM wengi tu waliomo humu, tena long living members.
Sijui mmilikia wa HABARI LEO lakini hasa THE AFRICAN ni watu gani na wana muelekeo gani. Lakini nawasihi tuwe macho na jinsi magazeti yanavyohabarisha kuhusu JF kwa kuiponda lakini vilevile zinapotoka brilliant posts unashtukia magazeti hayoayo yanaikopi post nzima tena front paga lakini yanataja mtandao mwingine kabisa.
View attachment 46075View attachment 46077