Je, Bunge litamfukuza Zitto kwa "kutokuhudhuria" vikao; hasaini kupokea posho!? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, Bunge litamfukuza Zitto kwa "kutokuhudhuria" vikao; hasaini kupokea posho!?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by SubiriJibu, Jan 23, 2012.

 1. S

  SubiriJibu JF-Expert Member

  #1
  Jan 23, 2012
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 1,131
  Likes Received: 779
  Trophy Points: 280
  Wakuu,

  Wala sina mpango wa kubadili headline kwa sababu wanaokumbuka akiwemo Zittto mwenyewe wanajua kuwa niko sahihi kabisa!

  Sakata la kufukuzwa Zitto Kabwe linaanzia kwa msimamo wake binafsi aliouanzisha bungeni. Yeye hakutaka kuzama zaidi kwenye malumbano ya kwamba ama posho ni sahihi au si sahihi. Zitto aliamua kukataa kuchukua posho ile.

  Mtego uliotaka kumnasa Zitto ni ule utaratibu kwamba attendance form ndiyo inayotumika kulipa wabunge posho zao (seating allowances).

  Bado hili halikuwa kikwazo kwa Zitto na mwishowe akaamua kuacha kusaini kabisa forms hizo ili kukwepa kuingizwa katika list ya wachukua posho.

  Spika Anne Makinda alikuja na kauli kwamba kwa attendance form ndiyo ushahidi wa mhudhurio ya mbunge basi Zitto akikosekana mara tatu basi atakuwa amejifukuza ubunge kwa mujibu wa Katiba ya nchi.

  Ni kweli Katiba ya nchi Ibara ya 71(1)(c) inasema hivi:

  Mbunge atakoma kuwa Mbunge na ataacha kiti chake katika Bunge ikiwa Mbunge atakosa kuhudhuria vikao vya Mikutano ya Bunge Mitatu mfululizo bila ya ruhusa ya Spika

  Sijasikia Anne Makinda au bunge zima likisema limeacha kutimiza mpango wa kumfukuza Zitto ubunge. Hivyo, binafsi nimekuwa nikifanya countdown na hatimaye muda uumefika.

  Zitto alianza kuacha kusaini mahudhurio kwenye Session/Mkutano wa NNE. Mkutano wa SITA unaanza Tuesday, January 31, 2012. Matokeo yake ni nini?

  Matokeo yake ni kwamba siku bunge linaahirishwa basi Zitto Kabwe atakuwa amekamilisha MIKUTANO MITATU huku karatasi ya mahudhuriao haionyeshi jina lake!

  Kama alivyoeleza Spika, basi Spika huyohuyo Anne Makinda itabidi atimize kauli yake kutekeleza kifungu cha katiba kinachomtaka Zitto afukuzwe ubunge.

  Sijajua bunge linaloanza wiki ijayo litaisha lini. Lakini tunatarajia kuwa saa ya kuliahirisha yaani kuuahirisha MKUTANO WA SITA basi ndiyo saa ya kutangaziwa pia kufukuzwa kwa Zitto kabwe ubunge wake.

  Hatuhitaji kujua Makinda atatumia ushahidi gani wakati yeye mwenyewe alinukuliwa akifafanua kuwa kutosaini attendance form kunamfanya Zitto mbunge yeyote akabiliwe na adhabu ya kufukuzwa ubunge.

  Nafahamu kuwa kuna thread humu Zitto mwenyewe alieleza kwamba process ya kumfukuza anataka aone itakuwaje, kwa sababu ni kweli attendance forms hajazi lakini TV zinamuonyesha yumo bungeni, hansard zinamuonyesha anashiriki vikao.

  Je, wadau mna la kuongeza?

  Wasalaam.
   
 2. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #2
  Jan 23, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Ukweli haujifichi Tutajua karibuni.....
   
 3. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #3
  Jan 23, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Tunasubiri "Sarakasi za maneno!"
   
 4. M

  Makamuzi JF-Expert Member

  #4
  Jan 23, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 1,157
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Mwanzoni nlidhan umekurupuka kama MS,kumbe uko right,ni uchambuz mzuri wenye kujenga hoja,well done!
   
 5. Mpui Lyazumbi

  Mpui Lyazumbi JF-Expert Member

  #5
  Jan 23, 2012
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,853
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Namuonaga Zitto anachangia sana kwenye vikao/mikutano ya bunge.
   
 6. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #6
  Jan 23, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mbona Zitto alishalisemea hili. Alisema karatasi pekee siyo inayoonyesha kuwa mtu amehudhuria bungeni. Kuna hansard ambazo huandika matukio ya bungeni na hivyo anajitahidi kuchangia mara nyingi ili awemo kwenye hansard. Hapa zitto atakuwa amekizunguka hicho kifungu cha katiba.
   
 7. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #7
  Jan 23, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  umetumwa kutubeep? kabla hatujaenda mbali aulizwa spika na zitto tutapata majibu sahihi badala ya hisia. Tafsiri za kisheria ni pana kwa kila sentensi
   
 8. nice 2

  nice 2 JF-Expert Member

  #8
  Jan 23, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 746
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mkuu uliyeleta mada endelea ku 'subiri jibu', maana umejitahidi kweli kweli kuandika.
   
 9. mgodi

  mgodi JF-Expert Member

  #9
  Jan 23, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,309
  Likes Received: 974
  Trophy Points: 280
  Mama naye mbona anawakomalia wabunge wachukuwe posho hata kama hawataki, tatizo liko wapi kama wengine hawataki.. nilisikia hata mh january nae hataki posho! yeye vp anasaini kwny daftari? na kwa upande wa cdm ni mh zitto peke yake ndiye hasaini kwny daftari?
   
 10. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #10
  Jan 23, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  umetumwa kumtengenezea kesi Makinda ili aonekane anataka kupunguza upinzani bungeni, kama ni kweli sheria na kanuni zitachukua mkondo wake na Zitto kama hakujua hili basi hayuko smart enough kumalizwa kirahisi hivyo. chadema ina wanasheria kama Lissu, Safari na marando kama hawakumpa ushauri wa kulaumiwa sio Spika
   
 11. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #11
  Jan 23, 2012
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Hansard zitawaaibisha. Karatasi la mahudhurio si ushahidi pekee kuwa mbunge kahudhuria vikao. This will shake the intergrity of the Speaker and National Assembly/Perliament as a whole
   
 12. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #12
  Jan 23, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  suala la posho kama limekaa kisheria linatakiwa kumalizwa kisheria sio kisiasa, ukichanganya sheria na siasa ni hatari
   
 13. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #13
  Jan 23, 2012
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Ansard zitawaaibisha. Karatasi la mahudhurio si ushahidi pekee kuwa mbunge kahudhuria vikao.
  This will shake the intergrity of the Speaker and National Assembly/Perliament as a whole
   
 14. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #14
  Jan 23, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  mmmhh mabwaku mbona mambo haya hayaeleweki vizuri..
   
 15. M

  Mgaza jm Member

  #15
  Jan 23, 2012
  Joined: Oct 27, 2011
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sidhani kama orodha ya malipo bungeni tu ndio kigezo cha kujulikana kama upo?
  kwakua Zitto ni mtu makini tayari anajibu la hilo
   
 16. Mkondakaiye

  Mkondakaiye JF-Expert Member

  #16
  Jan 23, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 839
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Makinda kama anataka kuhakikisha kuwa mapenzi ya watanzania yako kwa ccm au upinzani ajaribu kufanya hicho kitu.
   
 17. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #17
  Jan 23, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Ivi msimamo wa shibuda ukoje hadi sasa kuhusu posho.bado anataka ziongezwe hadi laki tano au ameridhika. na je vp msimamo wa cdm kuhusu huyu jamaa.atapigwa chini au ndio nipotezee kiaina.
   
 18. Third Eye

  Third Eye JF-Expert Member

  #18
  Jan 23, 2012
  Joined: Jan 8, 2012
  Messages: 332
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  Eh roho yangu ungoje burudani pale mjengoni, mama Makinda akiwa kanuna pale kati anatamani kumfukuza Zitto ila hansard zinambana, Lisu anazunguka zunguka kwenye kiti mdogo mdogo, awesome view
   
 19. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #19
  Jan 23, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0

  Hili sio suala la makinda,ni ishu ya kisheria.
   
 20. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #20
  Jan 23, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,768
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  mbona wote mnaochangia sijawahi kuona majina yenu!???
   
Loading...