Je bunge letu limejaa wajinga?

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2013
Posts
12,151
Reaction score
44,072
Kuna kipindi Spika Ndugai iliwahi kusema mule bungeni kuna wavuta bangi balaa, na akashauri ikiwezekana hatua madhubiti zifanyike ili kunusuru ile hali. Bunge likazizima kwa makofi ikiwa ishara kuunga mkono hoja ile.

Juzi juzi, Mbunge Waitara akatoa pendekezo la kuomba ofisi ya spika ifanye haraka kuleta mashine mahsusi wa kuwapima ushoga kwa wabunge. Bunge likazizima kwa makofi ikiwa ishara kuunga mkono hoja!

Siku ya leo, Spika Tulia ameibuka na kusema kuwa, mijadala kadhaa iliyofanyika siku chache zilizopita ndani ya bunge ilikuwa na makosa makubwa ya kikanuni na kisheria na bunge halihusiki nayo. Wabunge na kiti cha spika kilichohusika katika kipindi hicho, kwa kutokujua (umbumbumbu) walifanya hayo kimakosa na Spika akaonya hayo mambo yasiendelee na yasije yakajitokeza tena. Baada ya Spika kusema hayo, wabunge wakapiga makofi kuachiria kuunga mkono hoja!

Nimebaki nimejiuliza haya;
1. Kwenye pendekezo la kudhibiti uvutaji bangi miongoni mwa wabunge, bunge liliunga mkono hoja kwa makofi mengi!

2. Kwenye pendekezo la kuletwa mashine maalum ya kupima ushoga kwa wabunge wote, bunge liliunga mkono hoja kwa makofi mengi!

3. Kwenye pendekezo la kudhibiti umbumbumbu (ujinga) miongoni mwa wabunge, bunge liliunga mkono hoja kwa makofi mengi!
 
Hapana, wana akili timamu na wanajua wanachokifanya kuwa si halali, si chema ila wanatetea ajira zao na kujikomba kupata teuzi.

Ikitokea CCM ikaondoka madarakani, na wao CCM wakatekwa, wakauawa, wakapotezwa unadhani watasema ni sawa maana yalikuwa yanafanyika CCM tukiwa madarakani. Wataandamana kupinga kuua, kutekwa etc etc,
 
Mwashambwa akiona hayo makofi anabubujikwa machozi🤣🤣🤣
 
Bunge la " hongera na pongezi"
Muda wa kuchangia hoja anapigiwa kengele.....hopeless!
 
Yangu ni ndio yapi maoni yako?
 
Icho ni kikao cha chama fisiem TU.
KAZI ni kipimo cha utu
 
Humo yamejaa ma Kenge Maji, wameamua kutoa profile zao kwa sababu ni aibu. Mtu Elimu ya Sekondari anasoma zaidi ya miaka 13 unategemea kichwani atakuwa mzima kweli???!!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…