Je, baadhi ya miradi inayofanyika Dodoma ni kinyume cha malengo ya kuufanya kuwa mji wa kiSerikali?

Je, baadhi ya miradi inayofanyika Dodoma ni kinyume cha malengo ya kuufanya kuwa mji wa kiSerikali?

Keynez

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2007
Posts
3,621
Reaction score
6,510
Mara kwa mara nimekuwa nasikia baadhi ya miradi inayofanywa na serikali huko Dodoma, nabaki kujiuliza kwamba mbona yanaenda kinyume na malengo yaliyokusudiwa ya kujenga mji wa kiserikali?

Jana nilisoma mahali kwamba wanajenga viwanja vikubwa vya mchezo wa golf na lengo ni kupafanya Dodoma kuwa kitovu cha utalii wa michezo. Hivi viwanja vya Kawe, Lugalo na Gymkhana vimeleta utalii kiasi gani mpaka sasa? Hivi kupeleka mradi huo Dodoma ni wazo sahihi kweli na ni kipaumbele cha mji huo kwa sasa na hata kwa siku zijazo?

Miradi mingine unaona ina nia ya kukuza population ya Dodoma kwa kasi na kuwa na mji wenye hekaheka nyingi mfano wa Dar es Salaam jambo ambalo nadhani ni kinyume na malengo ya kuhamishia ofisi za serikali huko.

NB. Nilianza kuona kuna shida kwenye maono ya viongozi kwa kitendo cha kujenga Ikulu Dodoma ambayo ni copy and paste ya Ikulu ya Dar es Salaam. Nadhani fikra hizo ndiyo wanaendelea nazo katika miradi mingine.
 
Ni SAWA
Kama wakipewa vijana wetu wasomi kuifanya hiyo project, waka design viwanja vya golf vikawa na hadhi ya kimataifa itakuwa ni jambo la kujivunua kama Taifa.

Najua unazungumzia priority,
 
Ni SAWA
Kama wakipewa vijana wetu wasomi kuifanya hiyo project, waka design viwanja vya golf vikawa na hadhi ya kimataifa itakuwa ni jambo la kujivunua kama Taifa.

Najua unazungumzia priority,
Jeshi ndiyo linajenga na pia wanajenga miundombinu mingine ya michezo. Hii haikutakiwa kupelekwa Dodoma.
 
Labda mtoa mada alitaka pajengwe flyover tu ndo aamini kua malengo ya serikali yanatimia
 
Jeshi ndiyo linajenga na pia wanajenga miundombinu mingine ya michezo. Hii haikutakiwa kupelekwa Dodoma.
Sema hili swala la kuwaichia jeshi pekee sio sawa, itapoteza ushiriki wa jamii kwenye michezo ya golf.

Mkuu, Dodoma mji wa serikali , kwenye swala la mipango miji ni muhimu kuwepo na sehemu za michezo ya aina mbalimabli, kwa ajili ya kuzalisha utalii,burudani etc..
 
Ilitakiwa kwanza tufahamishwe mji wa kiserikali unakuwaje Ninavyo jua mimi hamna kitu kama mji wa kiserikali. Hata Washington DC sio mji wa kiserikali. Tatizo letu ni kuwa tunapenda mno kutanguliza buzz words. Maneno kama Geneva ya Afrika!

Amandla...
 
Kimsingi Washington DC ilianzishwa kama mji wa kiserikali na una vigezo na mambo mengine ambayo yanautofautisha na miji mingine.
 
Sema hili swala la kuwaichia jeshi pekee sio sawa, itapoteza ushiriki wa jamii kwenye michezo ya golf.

Mkuu, Dodoma mji wa serikali , kwenye swala la mipango miji ni muhimu kuwepo na sehemu za michezo ya aina mbalimabli, kwa ajili ya kuzalisha utalii,burudani etc..
Na wewe unarudia story za utalii. Viwanja vya golf vya Kawe na Lugalo vimeleta kiasi gani cha utalii?
 
Na wewe unarudia story za utalii. Viwanja vya golf vya Kawe na Lugalo vimeleta kiasi gani cha utalii?
Na ndio maana mwazoni nimekataa hivi viwanja kumilikiwa na jeshi, Dubai, Saudi Arabia na Nchi nyingi za Emirates Wana host michezo ya golf.

Ni swala la Nchi ya Tanzania kuamua TU, golf, swimming, etc itatumika kuzalisha utalii na ajira
 
Bado unazunguka tu. Viwanja vilivyopo mpaka sasa ambavyo vimekuwepo kwa miaka vimeingiza kiasi gani cha utalii hadi udhani kuwa hivyo vya Dodoma vitafanya hivyo?
 
Naona mmekosa hoja ila mikono ilikuwa inawasha kucomment chochote.
Sasa kiongozi kuuliza kwa nini hutaki hivo vitu viende Dodoma ni jambo baya hadi useme mikono imetuwasha kucomment?
 
Sasa kiongozi kuuliza kwa nini hutaki hivo vitu viende Dodoma ni jambo baya hadi useme mikono imetuwasha kucomment?
Ukiwauliza wachumi watakwambia siku zote rasilimali zipo "limited".

Hivi watu wenye akili timamu wakikaa wakasema tunajenga mji wa kiserikali Dodoma huku tukiwa na "limited resources", vipaumbele vya hiyo project vinaweza kujumuisha viwanja vya golf?
 
Back
Top Bottom