Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,499
- 113,610
Wanabodi,
Declaration of Interest Kuhusu Uzalendo.
Naomba ku declare interest yangu kuhusu uzalendo wangu kwa nchi yangu, kwa sababu, ukiibua hoja yoyote humu, kuhusu utendaji usioridhisha wa mashirika yetu ya umma ya kizalendo, utanyooshewa vidole kwa kutuhumiwa wewe sio mzalendo. Ile siku nilipoibua mjadala huu kuhusu ATCL,
ATCL, tuache siasa kwenye usafirishaji abiria. It's not fair kuchelewesha abiria kwa dakika 45 wakiwa ndani ya ndege, kumsubiria abiria mmoja kigogo ambaye ni waziri
nilishutumiwa hadi na maziri husika kwa kukosa uzalendo, hivyo kuomba headline ibadilishwe!. Ndege ya ATCL yachelewa kuondoka ndani ya muda; watoa ufafanuzi!
Uzi huu ni uthibitisho wa uzalendo wangu, unapoona kuna uwezekano wa shirika lenu kuhujumiwa kwa ushindani usio sawia na mashirika ya nje, wazalendo wa kweli hatuwezi kunyamaza. Hivyo huu ni uzi wa kizalendo, kwanza kwa kuuliza swali tuu, jee kuna uwezekano, Shirika la Ndege la Fast Jet, linalihujumu shirika letu la Ndege la ATCL, kwa kuvamia routes za ATC na wao kupunguza bei kwa more than 50%!. Baada ya swali, pia ninatoa mapendekezo ya hatua za kuchukua, kufanya protection ya kilicho chetu.
ATCL inakwenda Kigoma mara mbili kwa wiki, kwa kutumia ndege yetu ya Bombadier -400, inayotumia Pangaboi, hivyo safari kuchukua muda wa saa 2.45, kwa nauli ya TZS 365,000 (japo tulielezwa nauli ni 165,000), lakini leo nimeona tangazo kuanza kuuzwa kwa tiketi za Fast Jet, kwenda Kigoma, ambapo safari zitaanza tarehe 1 Mwezi Machi, Fast Jet watazindua safari kati ya Dar es salaam na Kigoma kwa safari 3 kwa wiki, siku za Jumanne, Alhamis na Jumamosi kwa nauli ya Tsh 123,000. kwa kutumia ndege za kisasa aina ya Embraer E 190 ambayo ni Jet engine, safari itachukua muda saa moja tuu!.
Jee uamuzi huu wa Fast Jet, ni uamuzi tuu wa kawaida wa kibiashara, ili kuleta ushindani kwa kutoa more choices na ku provide some better a cheaper options kwa wateja wa usafiri wa anga, au una lengo la kuihujumu ATCL?, kwa kuifuata kule inakoruka, na wewe unapeleka ndege yako route ile ile, unaongeza frequency, unapunguza nauli, unatumia ndege bora Zaidi ya jet engine, wakati mwenzako ana bangaboi, unafanya direct route, kuruka kwa muda mfupi Zaidi wakati mwenzako anapitia Dodoma!, kuna mtu kweli ambaye ni time conscious na cost conscious ataendelea kupanda ATCL kwenda Kigoma, tangu siku Fast Jet, itaanza kuruka route hiyo?.
Kwa Nini Ndege Hazipangiwi Routes na TCAA Kama Mabasi Yanavyopangiwa na Sumatra, au Masafa na TCRA?.
Ukinunua dala dala, unaomba kibali Sumatra, wanakuonyesha routes zenye nafasi unachagua, kama unataka routes Fulani zenye mabasi mengi, unaambiwa hiyo route imejaa!. Vivyo hivyo kwa TCRA kwenye kugawa masafa, wengi wangetaka kutangazia DSM kwa sababu ndio kwenye wateja wengi, lakini TCRA inakulazimisha kwenda sehemu ambako redio hazijajaa!. Vivyo hivyo kwa Kampuni za simu, kulazimishwa kwenda hata sehemu kusiko na soko!. Kama ilivyo kwa regulators wengine kuwapangia players, kwa nini TCAA pia isiyapangie routes haya mashirika ya ndege ili wasigombee routes na kuuwana?, pia iwapangie nauli kama Sumatra?.
Kama ATCL inakwenda Kigoma, kwa nini Fast Jet nayo iende Kigoma tena kwa bei nusu ya ATCL?.
Kwa nini TCAA wasiilazimishe Fast Jet iende Singida, Iringa, Tanga, au route ambayo haina kabisa ndege?, kwa nini ndege zisongamane Dar, Mwanza, Kia, ect wakati Tanzania tuna routes kibao, na destinations tele hazina ndege?!.
Hostile Kick Out na Hostile Take Over ni Mbinu Chafu za Ku Create Monopoly Kwa Kuwafungasha Virago Wapinzani Wako, Kama ilivyo Inside Trading!.
Mimi licha ya kuwa ni mwanahabari wa kujitegemea, pia ni mfanyabiashara wa huduma za Radio na TV Programs production. Zikitangazwa tenda za utayarishaji wa Vipindi, washindani wako wenye akili Zaidi hufanya "inside trading", kwa ku collude na watu a ndani, kujua bajeti iliyotengwa, kisha kwenye tenda yao, wana quote bei ya chini ajabu kuliko hata bei ya soko, tenda inafunguliwa wewe bei yako inakuwa juu, unakuwa kicked out, mwenzako mwenye bei ya chini, anashinda tenda, kisha wale wanamfanyia appreciation kurekebisha viwango, na kumlipia pesa stahiki hadi ziada ili agawe cha juu as kick backs!.
Jee hiki kinachofanywa na Fast Jet sio hostile kick out of ATCL out of business kwa wao kushusha sana nauli ili ATCL akose wateja kwenye routes hizo, ajitoe kwenye hizo routes, ndipo Fast Jet waweke gharama halisi?. Mbinu hii hutumika kumuondoa mshindani wako kwenye soko kwa kuweka nauli za chini sana na kujiendesha kwa hasara kwa muda fulani, kisha akiisha fungasha na kuondoka, ndipo wewe utawale soko na kutoza nauli halisi?!.
Hostile take over ni kama kile kitu kilichofanyika kwa kwenye ile vita ya bia, (the beer war), kati ya KBL na TBL, Kenya walishusha bei ya bia zao zinazokuja Tanzania, na kuuzwa kwa bei ya chini kuliko bia za TBL, ilifikia mahali watu wa mikoa ya Arusha na Moshi kunywa zaidi Tusker kuliko Ndovu, vita hii ikamalizwa kwa makubaliano ya wakubwa, kuuziana viwanda juu kwa juu, matokeo yake kiwanda cha Kibo, kikafungwa!.
Jee bei hii ya tiketi ya Fast Jet ya Dar-Kigoma, TZS 123,000/= is it realistic, au wameshusha ili kuiua ATCL?.
Nini Kifanyike Kuinusuru ATCL na Ushindani Usio Sawia.
ATCL ni ndege yetu, inahitaji upendo wetu na protection yetu, kama tunavyozipenda familia zetu, ukiisha oa au kuolewa lazima umpende mkeo, hata kama utakutana na mwanamke mrembo vipi, au mke umpende mumeo, hata kama utakutana na mwanaume mwingine tajiri vipi!.
Huu ndio uzalendo wa kweli!, hivyo namalizia kwa lile lile swali la msingi, tukiona kama ATCL inakabiliwa na ushindani usio sawia, jee tutumie utashi wa kisiasa kuinusuru ATCL yetu, au tuachie tuu huu ushindani uendelee, na kuilazimisha ATCL lazima ihimili ushindani huu na kusaidiwa ili isishindwe. Najua ATCL inaendeshwa kwa hasara kwa kubebwa na serikali, bila kuisaidia ATCL kwa a political will, serikali itaendelea kuibeba hadi lini?. Watanzania sasa ndio tunabidi tuibebe ATCL kwa uzalendo, au mnataka tuiache tuu ijifie after spending all that much?.
Jumatatu Njema.
Paskali

- A Political Will, Kulazimisha Twiga Aendelee Kuchanja Mbuga!. Kwa vile ATCL ni ndege yetu, lazima tufike mahali. nchi yetu ichukue maamuzi ya kisiasa ya kuinusu ATCL dhidi ya ushindani usio sawia kutoka ndege za mashirika ya kipepari na kibeberu, hata kama uamuzi huo utakuwa unakwenga against free trade, ikiwemo kuandika waraka kwa taasisi zote za umma, wizara, idara na Wakala za serikali, kwa safari zote za kikazi, lazima kwanza waitumie ATCL, hata kama ni ghali zaidi na inakwenda pole pole kuliko jet engines, lakini fedha za umma kwenye usafiri wa ndani, lazima kwanza ziende ATCL, kama hawana route hiyo ndipo wapande ndege nyingine!. Hili linawezekana, mimi nimefanya kazi na Waingereza chini ya FCO, watu wote wanaolipiwa usafiri na serikali ya UK. lazima kwanza wapande BA, hata kama nauli ya BA ni juu na ghali kuliko ndege nyingine, ikiwa BA hawana route hiyo ndipo wapande ndege za mashirika nyingine.
- Tutumie Protectionism Kuchukua Protective Measures Kulinda ATCL. Hapa ni kuhakikisha ATCL inalindwa kibiashara kwa namna nyonyote ikiwemo some exclusive routes, na kuitumia TCAA kufanya restrictive measures kuzuia routes za ATCL kuingiliwa, na kuitumia Fair Competition kuzuia mashirika mengine yasishushe bei below average to make a business sense ili tuu kuwaua washindani wako wa kibiashara. Ikibidi ATCL ipewe some monopoly fulani hadi I stabilize kibiashara na kutawala soko. Hili liliwahi kufanyika kulinda viwanda vya ndani dhidi ya cheap imported products.
- Kuandaa Kampeni za Uzalendo Watanzania Wazalendo Tupande ATCL!, hii ni kampeni maalum ya kujenga upya moyo wa uzalendo kwa wasafiri wa ndege wa Tanzania, kujitolea kupenda kupanda ndege za ATCL kwa kuhimiza penda chako, jenga chako, kama Watanzania wote, tutapanda ATCL hivyo hivyo ilivyo despite all the odds, baada ya miaka michache, ATCL nayo itakuwa na uwezo wa kununua jet, na kufanya safari za haraka, na hizi pangaboi za Bombadia zitakuwa ni za group routes kusafirisha makundi ya wanafunzi na wanavyuo kwenye group trips.
- ATCL Isibweteke!. I know ATCL is making losses na serikali inaibeba ndio maana inazuia taarifa ya ukaguzi isiwekwe public. Hata kama serikali itachukua hatua za kuibeba ATCL kwa kila aina ya mbeleko, Uongozi na Menejment ya ATCL inawajibu wa kutobweteka na mbeleko ya serikali, bali nayo ijibebe kuhakikisha inatoa huduma bora na za ushindani, isije kufika mahali anayekubeba akachoka. sisi tunaoamua kupanda ndege za ATCL, pia tusafiri huku tunapata raha kwa huduma nzuri, na sio tusafiri na ATCL kwa sababu tuu ya uzalendo lakini watu tunasafiri huku tunakereka, tunanuna na tumekunja nyuso!.
- Tuisalie ATCL Ifanikiwe. Kwa kadri ndege zetu zinavyozidi kuchelewa kuachiliwa, ndivyo washindani wa ATCL wanavyozidi kuipiga bao, kwa kujiimarisha!, hivyo natoa wito kwa Watanzania wote wazalendo wenzangu, pia tutumie nguvu ya sala, kuombea ndege zatu ziachiliwe, ATCL ipeleke ndege kila kona.
- Hili ni la kwangu binafsi, kwa routes za Mwanza, kama ATCL kila siku kwenye route hiyo, itampangia rubani mmoja mdada mweupe kama shombe shombe , najua hajaolewa!, na kumtangaza huyu rubani Binti ndie rubani wa kudumu wa ndege za ATCL kwa route ya Mwanza!. Ndege ikiwa njiani kwenye mazingira tulivu, aweke auto pilot na kutoka cockpit kuja kusalimia abiria!, nawahakikishia ndege ya ATCL route ya Mwanza, kila siku itajaza abiria mijibaba ya Kisukuma, hata wale Wasukuma wanaosafiri kwa mabasi, wakijua wanaendeshwa na rubani mwanadada Cheupe!, watadunduliza na kuhakikisha wanapanda ndege za ATCL tuu, na hata ikitokea Fast Jet na Precision hata wakaweka nauli ya bure, bado ATCL ndio itajaza kwanza abiria wa Mwanza, halafu wengine ndio watafuatia!.