Je,ataweza kujiunga na mafunzo ya ualimu msingi ngazi ya astashahada?.

kalma

Member
May 27, 2017
18
45
Nawasalimu wakuu nakuwatakia amani na salama kutoka kwa yule mnae mwamini.

Kama mnavyojua,mwishoni mwa wiki iliyopita NACTE ilifungua dirisha kwa waombaji katika kada za ualimu na afya.
Nikasoma (entry requirements) za karibu kila Chuo kwa ngazi ya cheti nikaona "vipaumbele kutolewa kwa waombaji waliofaulu masomo ya hesabu,biolojia,kemia,fizikia,sayansi ya uhandisi,kiswahili na kiingereza".Hapo nikaanza kushindwa kuelewa.

Niende kwenye lengo kuu.
Kifupi Nina kijana mwenye matokeo yafuatayo;
Civics-C
History-B
Kiswahili-C
Geography-D
English-A
Biology-B
Chemistry-F
B/math-F

Kijana huyu alifanya mtihani kama "private candidate".Kijana huyu,hajapata nafasi ya kujiunga na kidato cha tano awamu ya kwanza,lakini hata katika orodha ya awamu ya pili (kwa wale watakaopangiwa hayumo)

Swali,je kijana huyo ataweza pata nafasi katika mafunzo ya ualimu ukizingatia kapata F katika masomo ya hesabu na kemia?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom