Je, asili ya binadamu na hatima yake ni ipi?

Pure_sapiens

JF-Expert Member
Dec 25, 2016
2,202
2,035
Habari ndugu zangu wana jf.Kutokana na maendeleo ya binadamu Katika nyanja za sayansi na teknolojia kumekuwa na juhudi mbalimbali Katika kutafuta asli ya binadamu na hatima yake hapa duniani.Kumekuwa na tafiti mbalimbali zimekwisha fanyika na zingine zinaendelea kufanyika kuhusu asli ya kiumbe huyu.Kuna nadharia mbalimbali zinazoeleza asli na hatima ya binadamu.Nadharia hizo zimejikita Katika makundi matatu;Makundi hayo ni-Nadharia ya kihistoria,nadharia ya kisayansi,na nadharia ya kiimani/dini
1;Nadharia ya kihistoria,nadharia hii inasema binadamu ametokana na jamii ya sokwe(Zinjanthropus).Binadamu huyo wa kwanza asili yake ni sokwe ambaye alikuwa anatembea kwa miguu na mikono.
2;Nadharia ya kisayansi,nadharia hii inaeleza asli ya binadamu ni majini.Yani kiumbe cha kwanza kilitoka majini akabadilika na kuwa binadamu.
3;Nadharia ya kiimani/dini,nadharia hii inasema binadamu asili yake imetokana na udongo,binadamu ameumbwa na Mungu.Lakini Katika nadharia hii zinapishana kulingana na dini husika.Kila dini inaeleza kulingana na mapokeo yake.
Lakini nadharia zote zinashindwa kupata muafaka kuhusu asili ya binadamu na hatima yake.Watalaamu hawa wameshindwa kukaa meza moja na kuja na kauli moja kuhusu asili na hatima ya binadamu ni nini hapa duniani.
Kuna maswali mengi lakini ambayo yanazuwa utata zaidi ni je binadamu asili yake ni ipi?Akifa binadamu anakwenda wapi? anapozikwa inakuwa ndo mwisho wake?
Je kwa mtazamo wako asili na hatima ya binadamu ni ipi? Karibuni wandugu
 
Hmm! Wanachokifanya na nisawa na kuanza kujichunguza kutaka kujua kama baba uliyenaye ni baba yako mzazi au alisingiziwa...
 
Hmm! Wanachokifanya na nisawa na kuanza kujichunguza kutaka kujua kama baba uliyenaye ni baba yako mzazi au alisingiziwa...
Kuna ubaya gani kuanza kuchunguza asili yako.Mi nadhani ni jambo la msingi kufahamu kuwa umetoka wapi na unaenda wapi
 
Kuna ubaya gani kuanza kuchunguza asili yako.Mi nadhani ni jambo la msingi kufahamu kuwa umetoka wapi na unaenda wapi
Ni kweli hakuna ubaya, lakini ukizidi sana utakuwa unatafuta mengine, ambayo yanaweza kukuumiza zaidi...
 
That is the challenge. Lakini mimi naweza kusema kwamba hatma ya binadamu ni pale anapokufa. Maana tangu binadamu waanze kufa hatujawahi kuona wakirudi. Samahani maana hili jibu/mtazamo wangu ni very simplistic lakini ukweli ni kwamba...when we die that is the end of us. Unless tupate ushahidi tofauti.
 
Je itakuwa vipi kwa wale ambao wamezulumiwa haki we unadhani ndo itakuwa basi.Kama tukifa ndo inakuwa mwisho wetu sasa roho zinaenda wapi
 
Back
Top Bottom