Tatu
JF-Expert Member
- Oct 6, 2006
- 1,140
- 370
Katika harakati zangu katika mtandao wa Google Play wa kutafuta dawa ya baadhi ya watu ambao ni wadaiwa sugu na wamekuwa wakinipiga chenga kwa ahadi za uongo kila kukicha, nimefanikiwa kupata app inayoitwa YOMM iliyotengenezwa na kampuni ya ZaidiSoft. Hii app inamuwezesha mtumiaji kuweka kumbukumbu ya madeni anayodai au anayodaiwa na malipo katika madeni hayo.
Kilichonifurahisha zaidi kuhusu hii app ni kwamba, kama mtu asipolipa deni, unaweza KUMUANIKA kwa maana ya kwamba mtumiaji yeyote anaweza kufanya search kwa jina au location na kujua kama mtu fulani ana deni. Kwa hiyo kama una hii app halafu rafiki, ndugu, mwanafunzi au mfanyakazi mwenza, au mtu yeyote anataka kukopa hela, unaweza ku-search kabla hujafanya uamuzi wa kumpa au la.
App ni kwa watumiaji wa simu za Android (sina uhakika kwa watumiaji wa iPhone au BlackBerry) na ipo kwa Kingereza. Natumaini itakuwa ya msaada kwako na wale wenye biashara ya kukopesha mikopo midogo midogo kwa watu. Hii app itakuwa dawa ya matapeli na wale wanaopenda kuwarusha watu.