Kwa maisha ya kijamii, HAKI na AMANI vinafungamana, vinategemeana. Ni kama KUKU na YAI. Huwezi kupata kimoja kama huna cha pili.
Huwezi kudai HAKI kama huna AMANI; na huwezi kupata AMANI kama hutendi HAKI.
Kwa WATAWALA, kudai haki ni uanaharakati. Ni uchochezi. Ni uvunjifu wa amani. Kwao wao, AMANI lazima ilindwe hata kama wataua maelfu kwa maelfu ya watu, ili watakaobakia, wakiwamo wao, waishi kwa amani.