mwl.lukiko
Member
- May 2, 2013
- 26
- 7
Leo ni siku yangu ya tatu hapa nchini Kenya, ni asubuhi tulivu kabisa, jua likiwa limechomoza taratibu na kwa uzuri kama mielezi ya lebanoni, hakika tunauona uzuri wa Bwana. Napita huku na kule hapa KABARAK UNIVERSITY katika shughuli zangu zilizonileta hapa, lakini pia nikijaribu kwa makini sana kutafiti juu ya itikadi na mitazamo ya watu hawa kuhusu msitakabali wa EAC lakini pia wa Afrika kwa ujumla. Jana nili-post status hapa nikizungumzia jinsi wakenya wanavyotudharau kuhusu matumizi ya ardhi yetu huko TZ. Nashukuru kwamba wadau mliamka na kuchangia kwa nguvu sana.
Leo nataka nilete kwenu jambo jingine nililoligundua katika utafiti wangu huu usiorasmi. Hili ni kuhusu Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai yaani ICC. Mkenya mmoja akaniuliza "hivi unalionaje suala la Afrika na ICC?" Kabla sijamjibu nikataka kwanza kujua yeye anamawazo gani. Alichoniambia akasema "ICC inatuonea sana Afrika, hebu sasa angali wanamshitaki rais wetu na Naibu wake, huu si ni uonevu, inabidi Afrika ijiondoe ICC". Mwisho wa kunukuu.
Sikutaka kuendelea na mazungumzo zaidi na mtu huyu, maana mtazamo wangu ni tofauti kabisa na wa kwake. Ni kweli kwamba ICC inaonekana sana kujishughulisha na kesi nyingi kutoka Afrika, lakini swali langu ni je, hao waaafrika wanaopelekwa huko wameonewa? Kabla hatuja zungumza kuwa Afrika inaonewa na ICC tujiulize kwanza hawa watu wanaoshitakiwa huko je wanasitahili au wameonewa? Afrika kama Afrika haiwezi kuonewa na ICC ndio maana si kila mtu katika Afrika anapelekwa The Hague. Tujiulize hivi makosa haya ambayo watu hawa wanashitakiwa nayo, ni makosa ya namna gani na yanahitaji adhabu gani. Nafikiri ambao wanalalamika kuwa Afrika inaonewa na ICC watakuwa hawajui maumivu wanayoyapata waathirika wa vitendo hivyo vya kinyama na mauaji yanayofanyika katika kutekeleza uhalifu huo.
Laiti kama ungepata nafasi ya kuzungumza na waathirika wa vitendo hivyo na kuwaambia eti Afrika ijitoe ICC, wangekukata ulimi ili usiseme tena maneno hayo. Hebu tujiulize hivi kinachotufanya Afrika tutake kujiondoa ICC ni nini kama sio nia ya kutaka kuukumbatia uovu na uasi. Ni nchi gani Afrika ambayo iko tayari kuwachukulia hatua wahalifu wa makosa haya kwenye nchi zao. Nitatoa mfano wa Rwanda na Kenya.
Rwanda mwaka 1994 baada ya mauaji ya kimbali ililiomba baraza la usalama la umoja wa mataifa kuanzisha kwa mahakama maalumu ya ku-deal na uhalifu wa kivita na mauaji ya kimbali yalifanyika nchini humo miaka hiyo. Baadae Rwanda yenyewe tena ikapinga kuanzishwa kwa mahakama hiyo na kunawakati hata walimzuia Mwendesha mashitaka wa ICTR visa ya kuingia Rwanda kufanya uchunguzi.
Kenya, baada ya vurugu zilizofanywa mwaka 2007 baada ya Uchaguzi mkuu nchini humo waliunda tume ya kuchunguza uhalifu huo. Miongoni mwa mapendekezo ya tume hiyo ilikuwa ni kutaka kenya ianzishe makama maalumu ya kushughulikia uhalifu huo. Kenya haikufanya hivo. Mwendesha mashitaka wa ICC alitoa muda wa mwaka mmoja ili Kenya ianzishe mahakama hiyo lakini Kenya haikufanya hivo. Kisha ICC kwenye ambacho kinaitwa "the prosecutor acting proporio motu" ilianzisha uchunguzi na kisha kushitakiwa kwa Kenyatta, Rutto na wenzao. Hawa wawili ambao sasa ni viongozi wa juu wa Kenya walishitakiwa kabla hawaja kwenye nafasi walizonazo sasa kwa hiyo hata immunity ya viongozi haikuwa juu yao. sasa ni kwa nini leo eti kwa sababu wameingia madarakani wanataka sheria iwaache?
Sisi wengine nao tunaingizwa kwenye mtego wa kutaka kuteta eti mahakama ya ICC iwaache kwanza. Mi binafsi nalipongeza baraza la usalama la umoja wa mataifa kwa kukataa ombi la AU la kutaka kesi za Kenyatta na Rutto ziahirishwe kwa mwaka mmoja. Hivi kama AU ingekuwa na uchungu hivo na waafrika si ingeomba kesi zote zilizoko ICC zinazohusu waafrika ziahirishwe? Kwa nini waombe za hawa wawili tu.
Najua siko kwenye vyombo vya maamuzi lakini kama mtanzania halisi napenda kuishauri serikali yangu isikurupuke juu ya jambo hili. Tujiulize kwanza nini siri ya kutaka kuizuia ICC kuwachukulia hatua wahalifu hawa? Ni nini faida za tukijiondoa au tukibaki na kuiacha ICC iendelee na kazi zake? Au ni ulize swali hivi wakati nchi za Afrika zinasaini sheria ya uanzishwaji wa ICC yaani ROME STATUTE zilikuwa zinategema nini?
Rais wangu, JK na watanzania wenzangu hebu tujiulize kwa nini hili vuguvugu la Afrika na ICC limekuja tu baada na Kenyatta na Rutto kuwa madarakani? Je, ni kwa sababu yao hata na sisi tunataka kuingia mkenge huu? Hapana mimi niaamini Tz kama nchi iliyokomaa katika demokrasia ya kweli na ukomavu wa kisheria. Tuiache sheria ichukue mkondo wake. Tuwaache ICC wafanye kazi ya kama watu hawa wakikutwa hawana makosa wataachiwa huru ila tusijiingize kwenye mtego wa kulinda watu ambao ukweli wa vitendo vyao waote tunaujua.
MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU NIBARIKI NA MIMI. ASANTENI KWA KUNISIKILIZA