Jay-Z kugomea wimbo wa Taifa

Super Villain

JF-Expert Member
Jan 2, 2019
9,204
2,000
Jay-Z na Beyonce ni miongoni mwa watu ambao walibaki wamekaa wakati wimbo wa taifa la Marekani ukiimbwa kwenye ufunguzi wa fainali za #SuperBowl usiku wa kuamkia leo. Tafsiri yake ni kutounga mkono vitendo vya uonevu na ukandamizwaji wa mtu mweusi.


Hii imemuamusha Mtangazaji Tomi Lahren ambaye ameandika kupitia ukurasa wake wa twitter akiuliza kama wanaweza kujaribu kutafuta Nchi nyingine ambayo itawapa uhuru na mafanikio.


Pia Mchezaji Colin Kaepernick amemdhihaki Jay-Z kwa kumwambia "Nilifikiri tumemaliza mchakato wa kupiga magoti" kama alivyowahi kusema [Jay-Z] kwenye moja ya mahojiano yake mwaka jana.


Pia ukiachana na story ya Jay-Z kugomea wimbo wa taifa usiku wa kuamkia leo, Unaukumbuka ule mstari wake kwenye wimbo wa THE APE SH*T alisema "I said no to the Super Bowl, you need me, I don't need you" - ndio, sasa Jay-Z amefafanua hili kwenye mahojiano na The New York Times.


Amesema aliipiga chini ofa hiyo ya kutumbuiza kwenye fainali za Super Bowl mwaka 2018 kutokana na waandaaji kumpa ofa ya kutumbuiza wimbo wa "Run This Town" pamoja na Rihanna. Ofa hii ya kutumbuiza pamoja na msanii wake wa Roc Nation haikumuingia kichwani Jigga na kuamua kuipiga chini. Awali ilisemekana kwamba Jay aliipiga chini ofa hiyo mwaka jana kutokana kumuunga mkono mchezaji Colin Kaepernick.

IMG_20200203_192737_035.JPG
IMG_20200203_192644_579.JPG
IMG_20200203_192717_545.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom