MchangaMweupe
New Member
- Nov 24, 2025
- 1
- 0
Utangulizi:
Maandishi haya yanawajia ndugu zangu baada ya matukio kadhaa yaliyojiri katika nchi yetu. Mwandishi ameona ikiwa ni vyema tukapata mda wa kukaa na kutafakari japo kwa njia hii ya fasihi haya yaliyojiri na pia kuhakikisha kuwa yaliyotokea yasisahaulike au kubezwa bali yawe funzo na mbegu izaayo mwanzo mpya katika nchi yetu. Wengi wetu humu ni watu ambao tuna nia za dhati kabisa na ardhi hii pendwa tunayoiita nchi yetu; tunaipenda, tunaiheshimu, na tunaiita nyumbani. Mengi yamekuwa yakijiri nasi tumeshiriki katika kuyafumbia macho, na haya haya ndiyo yametufikisha hapa tulipo. Tupo katika njia panda. Yawezekana yajayo yakawa mema kwa hii ardhi tuiitao nchi yetu au yakawa mabaya na kuturudisha katika zama za giza. Hii basi iwe rai kwetu kuwa wakati wa kunyamaza na kufumbia macho maovu na mabaya yanayotendeka katika ardhi hii, kuyapea mgongo na kudhani hayatugusi kwa namna moja au nyingine, na pia kushiriki katika kuyanufaisha, umefikia mwisho maana matokeo yake tumeyaona na yametugusa vilivyo. Haya na maandishi yajayo ni mchango wa rambirambi kutoka kwa mwandishi kuja kwenu kwa msiba huu mkubwa tulioupata. Ni ombi la dhati la mwandishi kuwa, maneno haya yakae mioyoni mwenu na kumea taswira mpya itakayo neemesha ardhi hii tuiitao nyumbani.

Shairi: Jasho
Naomba usimwambie Mama,
Hii rangi nyekundu sio damu,
Namuona kibarazani ameshika tama,
Kajitwika kanga tulionunua kule Lamu,
Mwambie hili ni jasho na maji,
Mbolea tamu kwa ardhi hii,
Sio damu inayomlilia Mpaji,
Vita ya Abili mbona haingilii,
Tafadhali nakuomba usimwambie Mama,
Majeraha yangu bado mabichi,
Walionidhuru ni zangu jama,
Wanalamba asali mtoni kijichi,
Je ni kosa kudai haki?
Je ni kosa kudai haki...?
Imeandikwa na ndugu "mhaini" (mwananchi)
SDG.