Jasho La Mkulima | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jasho La Mkulima

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Augustine Moshi, Aug 20, 2006.

 1. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #1
  Aug 20, 2006
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 316
  Trophy Points: 180
  Serikali Iache Kudhalilish Wakulima.

  Wakulima wadogo wanapata taabu sana. Kuna wazee miaka 65 au zaidi bado ni wakulima wa jembe la mkono. Hawawezi kung'atuka kwani hawana pensheni.

  Sasa katika umri huo, mzee anachohitaji sio mahindi ya ugali tu, bali sukari ya chai na hata fedha za kinywaji. Wenyewe hudai wakijaribu kunywa maji ya bomba huwa hayapiti kabisa.

  Wakulima huwa wanaishiwa sana. Sasa akilima mahindi yakifika wakati wa kuliwa mabichi, huamua auze kiasi ili apate fedha za sukari, kwani hajanywa chai miezi, na koo limekauka kabisa. Fikiria anavyoudhika kunapotokea kijana mdogo, DC ambaye amejua kutoa kamasi mwenyewe juzi tu, anamwambia "Huna ruhusa kuuza mahinda mabichi"! Kwani ni mahindi ya serikali?

  Sasa mahindi yakivunwa, wakulima hula mengine, kiasi huuza kupata fedha, na mengine hutengenezea viburuduisho kama kimpumu na kiamble. Sasa ka DC tena kanakuja na vimgambo vyake kanasema hakuna ruhusa kutengenezea mahindi kinywaji. Ni mahindi ya serikali? Kwani wakulima ni watoto wadogo wasiojua wanachohitaji ni nini? Serikali inawadhalilisha wakulima kwa hatua hizi za uonevu. Ni lini wakulima wa Tanzania watapata UHURU?

  Mkulima ana haki ya kulima zao lolote analotaka (mradi lisiwe kitu kama zao la bhangi amabalo limekatazwa na Bunge), kuuza mazao yake wakati wowote anaopenda na kwa yoyote amtakaye, na kutumia yaliyobaki kwa namna yoyote anayopenda, ikiwa ni pamoja na kuyanywa pombe kama akijisikia kufanya hivyo. Ni yake, ana uhuru nayo.

  Serikali iache kuwakandamiza wakulima kwa kuwanyima uhuru wao wa kisheria wa kujiamulia mambo yao wenyewe. Ma DC waache tabia chafu ya kutunga na kutekeleza sheria zao wenyewe, na sheria yoyote itungwayo na serikali za mitaa isipingane na uhuru wa msingi wa kila mtu, ambao uko kwenye katiba.

  Augustine Moshi
   
 2. DZUDZUKU

  DZUDZUKU JF-Expert Member

  #2
  Sep 25, 2016
  Joined: Nov 8, 2012
  Messages: 3,474
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
   
Loading...