Jaribio la kuiba silaha JWTZ Bohari kuu Gongo la Mboto

Huyo jamaa aliyetaka kwenda kuiba jeshini ana akili timamu kweli?

Wanajeshi always ndiyo huwa chanzo,wanawadharau sana polisi! Kuna mshkaji wangu mmoja hivi ni mjeda anasema anatoa saluti kwa IGP tu lakini wengine hatambui vyeo vyao! Halafu cha ajabu jamaa mwenyewe ana nyota mbili tu kamaliza chuo kikuu hata miaka mi3 hana.Sijui wanafundishwa huko monduli kuwadharau wenzao?
 
Jamaa si walikuwa mitaani, hao majambazi walikosea step gani?

Azipa 14:01 Yesterday

Hakuna kitu hapa! Mimi naona nchi haina usalama kabisa. Siku moja kabla tulishaonywa kwamba waislam wataandamana baada ya sala ya Ijumaa.

Usalama wa Taifa wangeweza kumwagwa kwenye hot spots

Lingine mbona kwenye kifo cha Mwangosi inasemekana FFU walisafirishwa usiku usiku kwenda kuungana na wenzao Iringa?

Matumizi ya wanajeshi dhidi ya raia ni jambo ambalo halikubaliki. Na Mwamunyange ajue alichofanya hapo ni kutoa somo kwamba nchi hii kupinduliwa ni rahisi sana kama maandamano yanaweza kusababisha so much panic.

Wanajeshi wanauza sura mjini bila hata silaha. Na wasingeweza kuwa na silaha kwasababu zoezi zima halikuwa legitimate
 
Mhh hii sasa kali jambazi akaibe kwenye kambi ya jeshi??? Kuna namna hapo sio bure.
 
Siku zote nasema POLISI watumie taaluma yao vizuri. Kuwachelewesha hawa jamaa itatafsirika kuwa Polisi walihusika katika jaribio hilo.
JWTZ v/s Polisi:

Nimefahamishwa kuwa, askari walioavalia sare za JWTZ walishuka kwenye lori lao na ‘kumlabua’ askari aliyekuwa akiongoza magari kwenye eneo la Ubungo, Dar es Salaam kwa kuwachelewesha kwenye foleni kwa muda mrefu.

Taarifa kutoka chanzo kingine cha habari zikaongeza kusema kuwa Wanajeshi waliohusika ‘kulabua’ walikamatwa baadaye katika eneo la Ilala na sasa wapo rumande.

Jaribio la kupora silaha:

Kwa mujibu wa
GPL, mtu mmoja anaedaiwa kuwa ni jambazi wakiwa na wenzake waliingia katika kambi ya JWTZ 511 KJ bohari kuu ya kijeshi iliyopo Gongo-la-Mboto jijini Dar es Salaam kwa lengo la kupora silaha. Kulizuka purukushani baina ya majambazi hayo, askari waliokuwa ulinzi ndani ya kambi hiyo na raia, purukushani ambayo ilimtoa uhai jambazi mmoja.
 
Siku zote nasema POLISI watumie taaluma yao vizuri. Kuwachelewesha hawa jamaa itatafsirika kuwa Polisi walihusika katika jaribio hilo.
mkuu Thanda tunaambiwa hao wanajeshi wapo rumande je.walikamatwa na nani hadi kupelekwa rumande.? Wakati tunaambiwa polisi hana uwezo wa kumkamata mwanajeshi.?
 
Last edited by a moderator:
Majambazi wameenda kuiba silaha kwenye bohari ya jeshi?
Labda walikuwa wanajeshi!

yaani sehemu ya kijeshi inavamiwa mabwaku aisee yaani kwenye ulinzi kumbe shuduu tupu kweli tz ni zaidi uijuavyo...
 
mkuu Thanda tunaambiwa hao wanajeshi wapo rumande je.walikamatwa na nani hadi kupelekwa rumande.? Wakati tunaambiwa polisi hana uwezo wa kumkamata mwanajeshi.?
Polisi hana uwezo wa kuingia ndani ya Kambi ya Jeshi... Kumkamata ni haki yake kwani nje ya kambi ni uraiani na uraiani ni sehemu ya Polisi Mkuu ushawahi kuitizama ile movie ya First Blood Rambo alitiwa kuzuizini japo ni Mjeshi sababu alikuwa eneo lenye utawala wa kiraia...
 
nahis siku moja jeshi la polisi na la wananchi watapigana tena itakuwa kama moto wa petroli

mkuu usiombe hayoo wewe kwamacho yako hautaona bali utahadithiwa tuu ata ile juzi PALE KARIAKOO..JESHI WANGESHUKA HATA FFU.. USINGE WAONA MTAANI PALE OTE WANGETIMULIWA KAMA PAKA SHUME..WANGEBAKI JESHI TU...UKIONA WM/JESHI ANAKAMTWA NA KUFUNGULIWA MASHITAKA BASI UJUE NNCHI NI MZURI NA AMANI UPO SANA MWAKA 1964...NI MASAA 6 TU ILIKUA VITUO VYOTE VYA POLCE MILANGO ILIFUNGWA
 
mkuu Thanda tunaambiwa hao wanajeshi wapo rumande je.walikamatwa na nani hadi kupelekwa rumande.? Wakati tunaambiwa polisi hana uwezo wa kumkamata mwanajeshi.?
Suala la kuwapo remand (rumande) sina ukakika nalo..na kama wapo huko, ni kwa sababu ya kufanya makosa ya jinai. Kumpiga mtu hadharani, tena mwenye dhamana katika utumishi wa umma.idawa hakuna aliye juu ya sheria.Nilishasema kuwa Polisi ni usalama wa raia na mali zao(hii ni kauli-mbiu ya jumla ingawa bado kuna majukumu mengine (nisishughulike nayo kwa sasa). Uvunjifu wa amani ulifanyika uraiani...mlinzi wa hao raia ni nani. Nikupe kisa cha kweli ambacho nimewahi kukishuhudia kwa macho yangu mwenyewe KULE Arusha miaka ya hivi karibuni. Naamini wadau walioko kule ARUSHA mtanisahihisha kama nakosea kulikuwa na vita kati ya TPDF na POLISI. Na kama ni uasi kuhusu majeshi haya mawilii ungeanzia kule. Ni enzi za MKAPA na Bro MAHITA OMAR(IGP) Walikamatwa askari wanne kwa kosa la kuwapiga raia "wasio na hatia" waka
wa remanded kwa siku moja wenzao wakaja kuwatoa kwa kufuata taratibu zinazostahili, ila polisi wakasema haiwezekani ni lazima wafikishwe mahakamani. TPDF wakasema wapewe "wahalifu" wao watawafikisha katika mahakama ya kijeshi...POLISI wakagoma.Kilichofuata ni wale askari wakarudi kikosini kwao, Hawa walikuwa wanatoka kikosi cha "askari wa nchi kavu"/infantry toka 39KJ, mkuu wa kikosi wakati huo siwezi mkumbuka akawaita vijana wake na kutaka kujua ukweli ulivyo. Kumbe waliopigwa walikuwa ni madereva na makondakta wa daladala. Habari zikafika SOFA...kikosi cha service, 313KJ, kikosi 303KV wakashauriana wafanye nini ilhali wale vijana hawajapelekwa mahakamani.

Wakakubaliana kuwa hakuna daladala yeyote itakayofanya kazi kuanzia muda walioupanga wao, wakaingia mjini wakateka hizo daladala....zilikuwa zinafanya kazi ila wao walikuwa wanapanda na kushuka na kutandika dereva au kondakta yeyote, pili wakaenda central polisi wakiwa na silaha na kutoa amri ya watu wao kuachiwa, na bado polisi yeyote aliyekutwa mjini au hata wakle wa benki walipigwa.....technique iliyotumika ilikuwa ya ajabu sana. walifanya hivyo kwa wiki moja na bado majeshi ya ulinzi yalijipanga kutoa adabu kwa jeshi la polisi....mji ulichafuka waahidi kuipindua Arusha kwa Muda mfupi. Majeshi yakaanza kuungana ikafuatia 831JKT ya Oljoro wakaungana na kaka zao. Kambi zikiwa zinalindwa vizuri tu na bado kichapo kwa wiki nzima... Utatuzi wa mgogoro huo MKAPA alimwamuru Mkuu wa TPDF na IGP wakutane kwa dharura. wakaenda kukutania MONDULI wote na kujadili hali ilivyo na kupatanishwa haraka. Likatoka onyo kali la kuwakaripia vijana wasitumie nguvu na ujuzi wao vibaya.

Kuanzia siku hiyo ikatoka amri jeshini kuwa askari wote walioko na wale watakaokuwa wanasoma pale Tannzania Military Academy (TMA) wakiwa na shughuli zao weekend na kama wanataka kufika mjini, mavazi yao rasmi ni suti na tai....yaani wavae kibalozi.....wadau wa ARUSHA nadhani mtakuwa mnaikumbuka hii story.

Nimalizie kwa kusema "sheria ni msumeno". Ila usiombe MUTINY ITOKEE.....IKITANGAZWA STATE OF IMERGENCY, VITUO VYOTE VYA POLISI VITAFUNGWA KWA MUDA USIOJULIKANA.
 
Polisi hana uwezo wa kuingia ndani ya Kambi ya Jeshi... Kumkamata ni haki yake kwani nje ya kambi ni uraiani na uraiani ni sehemu ya Polisi Mkuu ushawahi kuitizama ile movie ya First Blood Rambo alitiwa kuzuizini japo ni Mjeshi sababu alikuwa eneo lenye utawala wa kiraia...
ILA MKUU DUDUWASHA, binafsi namkubali IDAWA, ni mkomavu wa fikra mwenye kutaka kujua mambo au inawezekana yeye mwenyewe ni mmoja kati ya askari polisi mwenye changamoto za ukweli na ndio maana mimi sitaacha kumjibu mtu mstaarabu kama IDAWA. uZURI WA jf NI kwamba kila mtu ana ufahamu wake na au ana kitu cha ziada kama wewe ambaye umemjibu vizuri tu...Ninyi ni watu muhimu katika utoaji michango humu JF......tuendeleeni hivyo hivyo, tueleweshane kwa kwa kufanya hivi, jamii itaelewa umuhimu wetu.
 
JWTZ v/s Polisi: Nimefahamishwa kuwa, askari walioavalia sare za JWTZ walishuka kwenye lori lao na kumlabua askari aliyekuwa akiongoza magari kwenye eneo la Ubungo, Dar es Salaam kwa kuwachelewesha kwenye foleni kwa muda mrefu. Taarifa kutoka chanzo kingine cha habari zikaongeza kusema kuwa Wanajeshi waliohusika kulabua walikamatwa baadaye katika eneo la Ilala na sasa wapo rumande.



Jaribio la kupora silaha: Kwa mujibu wa

GPL, mtu mmoja anaedaiwa kuwa ni jambazi wakiwa na wenzake waliingia katika kambi ya JWTZ 511 KJ bohari kuu ya kijeshi iliyopo Gongo-la-Mboto jijini Dar es Salaam kwa lengo la kupora silaha. Kulizuka purukushani baina ya majambazi hayo, askari waliokuwa ulinzi ndani ya kambi hiyo na raia, purukushani ambayo ilimtoa uhai jambazi mmoja
.

Mzee Mwanakijiji je haya matukio yanaweza kuwa na uhusiano na hofu yako!

mzee-mwanakijiji
Jua litakapotua na Giza litakapoingia...mwelekeo wa Tanzania utaamuliwa leo. Natumaini wapo watu ambao watasimama pamoja kupinga. Watu wema wa tanzania wapo wapi? Utafika wakati wale wenye kuamin katika udugu na umoja watoke na kusimama pamoja. Wasikubali kuiachia nchi ivurugwe hivi kwa uzembe wa wawatawala. Sijui usiku hu utapitaje..I dread the thought
 
Wabongo, wabongo, wabongo!!! Teknolojia ya kisasa ya mataa ya kuongoza magari ipo tele - mataa yanakuwa programmed kufuatana na hali halisi ya trafiki kwa wakati husika. Haya ya kusema askari wanaokoa sana jahazi ni fikra za karne ya ishirini kam sio karne ya 19. Serikali ya jiji au hata ya taifa (kwa vile Dar inaonekana kama ndio Tanzania yote) inao uwezo wa kifedha wa kuinunua teknolojia hiyo kama wahusika wangekuwa wanatumia vichwa vyao badala ya kutumia 'meya wa jiji'!!:sad:

Nilitegemea wasomi wa UDSM wangeweza kutatua tatizo hilo lkitaalamu (computerized) lakini muda ndio hautoshi wakitoka darasani wanaenda kujipikia au wanawahi kwa mama ntilie, kazi kweli kweli
 
Hao askari wa ubungo wanakera mno! Natamani kila siku wale kichapo!

Yaani wale wazee wa favor huwa wanakera mbaya sio siri ni kuchapwa makofi tu....
Mbaya zaidi ile junction pale ina mashimo kiasi kwamba magari yanaslow down na kusababisha flow rate kuwa ndogo.
 
Kama ni kweli sasa hali inatisha. Jeshini ni miongoni mwa maeneo ambayo huheshimiwa na kuogopwa sana.
 
Back
Top Bottom