Mazoezi ya kijeshi ya JWTZ yazua taharuki Dar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mazoezi ya kijeshi ya JWTZ yazua taharuki Dar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by OSOKONI, Aug 11, 2012.

 1. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #1
  Aug 11, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,809
  Likes Received: 3,893
  Trophy Points: 280
  Milio mizito ya mizinga, ngurumo za vifaru vyatikisa
  Msemaji wa jeshi : Ni mazoezi ya kawaida kabisa


  Mazoezi ya kijeshi yaliyofanywa usiku wa manane kuamkia jana na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), yalizua taharuki kubwa miongoni mwa wananchi wanaoishi jirani na kambi ya Vifaru ya Kiluvya nje kidogo ya jiji la Dar e s Salaam.

  Mazoezi hayo yanayoonekana kufanywa kwa udharura, yameleta wasiwasi mkubwa kwa wananchi kutokana na vishindo vikubwa vilivyo kuwa vikisikika mithili ya radi huku mingurumo ya vifaru ikisikika kwa nguvu.

  Wakati mazoezi hayo yakifanyika, mvua ilikuwa ikinyesha na umeme katika makazi ya watu ulikatika na kuzidi kusababisha hofu kubwa.

  Askari wa kambi hiyo walifanya mazoezi ya kushitukiza usiku wa kuamkia jana ikiwa ni pamoja na kuzijaribu zana zao nzito kama vile mabomu na mizinga ya kurushwa kwa vifaru huku ikitoa milio mizito.

  Vishindo hivyo vya majaribio ya silaha hizo nzito vilisababisha wananchi wanaoishi jirani na kambi hiyo wakiwemo wa Kiluvya, Kibamba na maeneo ya Mbezi, kupatwa na taharuki huku wakikumbushwa milipuko ya mabomu ya kambi za Mbagala na Gongo la Mboto yaliyosababisha vifo vya watu wengi na uharibifu mkubwa wa mali.

  Wakazi wengi wa maeneo hayo walilazimika kutoka nje ya nyumba zao na familia zao huku wakiwa hawajui hatma yao huku wengine wakizungumza kwa tahadhari wakiwa wamefunga nyumba zao na kukaa maeneo ya wazi huku wakifanya mawasiliano na ndugu zao walio nje ya maeneo hayo.

  Akizungumza na gazeti hili jana, Msemaji wa JWTZ , Kanali Kapambala Mgawe, alisema mazoezi hayo ni ya kawaida kabisa.

  “Huwa yakifanyika tunatoa taarifa, haya ya jana taarifa zilitolewa kwa wananchi wale wa jirani sana lakini kwa kuwa mazoezi yenyewe yalifanyika usiku, kelele zilisikika mbali sana tofauti kama mazoezi yangefanyika mchana,” alisema.

  Wasiwasi mkubwa uliwakumba wananchi kufuatia kauli za serikali bungeni dhidi ya chokochoko zinazofanywa na nchi jirani ya Malawi ya kugombea mpaka katika ziwa Nyasa.

  Pamoja na serikali kusisitiza kuwa jeshi limejiandaa kwa lolote litakalotokea nchini Malawi, Kanali Mgawe alisema mazoezi hayo hayahusiani na chokochoko za Malawi.

  Mwanzoni mwa wiki hii, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, aliionya Serikali ya Malawi juu ya utata wa mpaka uliopo katika Ziwa Nyasa kati ya Tanzania na nchi hiyo na kusisitiza kuwa Serikali ya Malawi hairuhusiwi kutumia eneo la mpaka unaogombaniwa hadi mwafaka utakapopatikana.

  Alisema tatizo hilo ni la muda mrefu ambapo Malawi wanadai Ziwa lote Kaskazini ya Msumbiji kuelekea Ruvuma na Mbeya ni mali yao kwa mujibu wa Mkataba wa Heligoland uliowekwa saini Julai mwaka 1890.

  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama, Edward Lowassa, naye alitoa msimamo wa kamati yake na kusisitiza kuwa JWTZ wako tayari kwa lolote ingawa aliomba Mungu kuepusha kutokea kwa vita na badala yake suala hilo liamuliwe kwa njia ya kidiplomasia.

  Msimamo huo wa serikali umekuja baada Serikali ya Malawi kutoa kandarasi kwa kampuni kadhaa za kigeni zinazoendesha utafiti wa mafuta na gesi katika eneo la ziwa Nyasa linalogombaniwa na pande hizo mbili.

  Ndege za kuangaza katika mipaka ya baharini zimeripotiwa kuzunguka mara kwa mara katika eneo la ziwa hilo kwa kile Tanzania inachokiita ukiukwaji wa makubaliano ya pande zote mbili.

  Wakati Serikali ya Tanzania ikiweka tishio hilo, serikali ya Malawi kupitia Waziri wake wa Mambo ya Ndani na Usalama wa Ndani, Uladi Mussa alisema Watanzania hawana mamlaka ya kuzuia utafiti wa mafuta uliokuwa ukiendelea katika ziwa hilo na kwamba shinikizo la Tanzania likiendelea watalazimika kwenda katika mahakama ya kimataifa.
   
 2. D

  Dopas JF-Expert Member

  #2
  Aug 11, 2012
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Safi saana kufanya mazoezi... msg sent to joy banda.. ingefaa mazoezi awamu ya pili yafanyikie mpakani kabisaaaa..
   
 3. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #3
  Aug 11, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Sio mara ya kwanza jeshi kufanya mazoezi, waandishi wanalazimisha habari!
  Kiluvya ni kikosi cha mizinga na mazoezi na routine yao.
   
 4. JOYCE PAUL

  JOYCE PAUL JF-Expert Member

  #4
  Aug 11, 2012
  Joined: Jan 8, 2010
  Messages: 1,007
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  kujiweka fiti ni muhimu kuwe hakuna vita au kuna vita.....watanzNI tuache woga...
   
 5. Aleyn

  Aleyn JF-Expert Member

  #5
  Aug 11, 2012
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 10,229
  Likes Received: 13,681
  Trophy Points: 280
  Huyu Wazir wao Ulad Mussa anajikuta kiburi sana.
   
 6. SALOK

  SALOK JF-Expert Member

  #6
  Aug 11, 2012
  Joined: Sep 20, 2011
  Messages: 2,683
  Likes Received: 879
  Trophy Points: 280
  POINT muhimu!
   
 7. Crucial Man

  Crucial Man JF-Expert Member

  #7
  Aug 11, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 3,277
  Likes Received: 470
  Trophy Points: 180
  Wakafanye mazoeri ziwa nyasa,na maeneo ya mipakani,wamalawi watafyanta wenyewe.
   
 8. i

  ivungwe New Member

  #8
  Aug 11, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Majirani wa hii kambi hii hatukalala kabisa na hatukuwa na taarifa yoyote!...muuungurumo na mtetemo was too much!
   
 9. Mjuni Lwambo

  Mjuni Lwambo JF-Expert Member

  #9
  Aug 11, 2012
  Joined: Apr 25, 2012
  Messages: 5,505
  Likes Received: 721
  Trophy Points: 280
  Kamanda mgawe ongeza ratiba ya mazoezi, we need a strong army kama kwa dogo kim un.
   
 10. mndwadage

  mndwadage JF-Expert Member

  #10
  Aug 11, 2012
  Joined: Jul 15, 2012
  Messages: 345
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ilipendeza Malawi wanavyorusha ndege mpakani sisi tuwe tunafanya mazoezi ya mizinga chini mpakani, wakiuliza tunawaambia mazoezi ya kawaida.!
   
 11. Tuyuku

  Tuyuku JF-Expert Member

  #11
  Aug 11, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 3,149
  Likes Received: 1,407
  Trophy Points: 280
  Safi sana. Sasa na Ngerengere wajaribu vifaa na ndege za kivita. Halafu kambi za mikoa ya Mbeya na Ruvuma wajaribu vifaa
   
 12. Jiwe Linaloishi

  Jiwe Linaloishi JF-Expert Member

  #12
  Aug 11, 2012
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 3,736
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Jamani mazoezi sawa hatukatai lakini taarifa ni muhimu sana jana mmekatisha game kibao za watu usiku si unajua hiki kipindi cha kipupwe dar ndio kipindi cha kupanda na kufanya palizi na hasa kulinda heshma ya ndoa
   
Loading...