Jaribio la kijeshi kumuondoa Rais wa Burundi madarakani

Baada ya kikao aungane na ndugu zake waliokimbia nchini mwake huko kigoma na wampe ukilanja wa hao wakimbizi wenzake si anapenda kuendelea kuongoza eeee' maana hakuna namna.
huko mbona mbali sana ! niko tayari kumlipia gesti keko magurumbasi ajifiche japo mwezi mmoja ili wananchi wamsahau .
 
Safi sana. Na ni mjinga saaaaana. Sasa heahima yote nje na kifwatacho ni kuporwa mali zake. Wakati angejitokea vuzuri angeendelea kuheshimika na kubaki na investment zake.
 
Tulioko Dar tutakimbilia wapi?si meli,ngalawa wala ndege zitaruka!
nadhani ueleko mzuri na salama utakuwa ni wa kusini....unachapa lapa mpaka n'twara kupitia daraja la rufiji.mbaya zaidi ni pale daraja hilo litakapo kuwa limetekwa na waasi wa chama cha magamba.hatari sana mkuu.tusiombe hii kitu itokee.:becky:
wale wa kasikazini itakuwa imekula kwao mazima,maana njia hiyo sidhani kama itaweza kuendeka.
 
Najaribu kuiangalia T-shirt aliyovaa hapa na kujiuliza kama inatokea kwa bahati mbaya au alikusudia kuinunua kutokana na maandishi yake yaliyokaririwa kutoka kwa mwananamuziki Tupac!
Kama asingelikuwa 'against the world' na kusikiliza dunia ilichokuwa inasema then akamuandaa hata 'mtu wake' na kumpa madaraka basi angepata heshima kubwa sana hata kama sio Burundi basi kwingineko duniani ikiwa ni pamoja na kurejesha heshima ya mtu mweusi. But all are now gone, imebaki story!!!
View attachment 251502

nami nakuongezea hizi......
1374639_10151638175210741_701684314_n.jpg
peter2304.jpg
fdd2304.jpg
 
5:36 Viongozi wote wa kanda ya Afrika Mashariki na kati wako Dar es Salaam kwa mwaliko wa rais Kikwete.
15:35 Rais Nkurunzinza yuko mjini Dar es Salaam Tanzania kuhudhuria mkutano wa kutafuta suluhu ya mgogoro wa kisasa uliokuwa ukiendelea Burundi.
15:30 Maelfu ya raia wa Burundi waandamana a mabarabarani mjini Bujumbura wakishangilia tangazo hilo la ''kutomtambua'' rais Nkurunzinza.
150513124232_burundirais_nkurunzinza_apinduliwa__640x360_bbc_nocredit.jpg

Raia wa Bujumbura wakishanilia tangazo la generali Niyombareh 15:20 Jenerali huyo aliyetimuliwa na Nkurunziza mwezi februari anasema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa.
15:10 Meja Generali Niyombareh amesema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya tatu ya urais wa Nkurunziza.
15:05Jenerali Niyombareh alikuwa ameandamana na viongozi wengine wa jeshi la Burundi.
15:00 taarifa zaibuka kutoka Burundi kuwa rais Nkurunzinza ameng'olewa'' madakani.
140806101022_habari_iliyotufikia_punde_640x360_bbc_nocredit.jpg

Meja Jenerali Godefroid Niyombareh amewaambia waandishi wa habari mjini Bujumubura, kuwa kumeundwa kamati maalum ya kuiokoa Burundi Ripoti kutoka Bujumbura zinasema kuwa kamanda mmoja wa kijeshi ametangaza kuwa hamtambui tena Pierre Nkurunziza kama rais wa Burundi
Meja Jenerali Godefroid Niyombareh amewaambia waandishi wa habari mjini Bujumubura, kuwa kumeundwa kamati maalum ya kuiokoa Burundi itakayotawala taifa hilo kwa kipindi cha mpwito.
Kulingana na taarifa iliyopeperushwa na redio Isanganiro, serikali ya Nkurunziza imeon'golewa madarakani.
Meja Generali Niyombareh amesema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya tatu ya urais wa Nkurunziza.
Jenerali huyo aliyetimuliwa na Nkurunziza mwezi februari anasema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa.
Kwa sasa rais Nkurunziza yuko nchini Tanzania alipokuwa anatarajiwa kujumuika na viongozi wa kanda hii ya Afrika Mashriki kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi tangu Nkurunzinza atangaze nia yake ya kuwania awamu ya tatu.
Jenerali Niyombareh alikuwa ameandamana na viongozi wengine wa jeshi la Burundi.
Meja Jenerali Godefroid Niyombareh amewaambia waandishi wa habari mjini Bujumubura, kuwa kumeundwa kamati maalum ya kuiokoa Burundi Tayari wanajeshi wameshika doria nje ya makao makuu ya runinga ya taifa.
Rais Nkurunzinza alikuwa amepuzilia mbali maombi ya kuahirisha uchaguzi huo.
Duru kutoka Burundi zinasema kuwa raia wameshajitokeza mabarabarani wakishangilia kauli hiyo ya ''Mapinduzi''

source:Burundi:Rais Nkurunzinza ''apinduliwa'' - BBC Swahili
 
Sisi watu weusi tunatia aibu sana, ulafi, uchoyo na ubonafsi. Haya majamaa pia nimajinga na mashenzi.

1. Yowel Kaguta Museven - Uganda

2. Paul Kagame - Rwanda

3. Joseph Kabila - DRC Kongo

4. Ally Bashil- Sudan

5. Robert Mugabe - Zimbabwe

6. Lipumba- cuf
7. Mbowe- cdm
 
Kumbukeni hiyo COUP D'ETAT haijaafikiwa na baadhi ya wanajeshi na maafisa wa jeshi ambao bado ni watiifu kwa Nkurunzinza, its response is not that much large as expected. It can turn to a CIVIL WAR. Mungu awaepushe kwani atakaeumia ni mwananchi wa chini.
 
Mimi huwa sielewi kabisa.Huwa inadaiwa kuwa urais ni mzigo. Ni kazi ngumu mno.

Halafu unakuta jitu limekuwa lirais kwa mihula miwili au zaidi halafu bado tu linataka kuendelea kuwa lirais.


Sasa kama urais ni mzigo inakuwaje kuna mijitu inapenda kung'ang'ania kuendelea kuwa mirais?


Ukiachia madaraka bado utatunzwa na hela za walipa kodi kwa maisha yako yote hata ukiamua kukaa tu nyumbani bila kujishughulisha na chochote tena.


Ya nini kutaka kuendelea kuwepo madarakani?
 
Back
Top Bottom