Japo umegharimiwa kwa machozi, jasho na damu, ulikuwa huru na wa haki!. Hongera CCM, CHADEMA poleni!. Mungu saidia Tz

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,468
113,583
Wanabodi,

Baada ya figisu figusu za hapa na pale za uchaguzi wa marudio wa majimbo ya Kinondoni na Siha uliohusisha kampeni kubwa za nguvu, zilizopelekea umwagaji wa damu, hivyo chaguzi hizi kuwa zimegharimiwa kwa machozi, jasho na damu, na kupotea kwa roho za Watanzania wenzetu wasio na hatia yoyote, na wengine wao, have nothing to do with politics, lakini hitimisho la jumla la uchaguzi huu, ni ulikuwa ni uchaguzi huru na wake haki, in a sense of kanuni ya "the end, justify the meas", haijalishi ushindi umepatikanaje, aliyeshinda ndie mshindi halali na ameshinda kihalali katika uchaguzi huru na wa haki!.

Aliyeshinda ameshinda kwa haki, aliyeshindwa ameshindwa kwa haki, tukubali matokeo, asiyekubali kushindwa sii mshindani!. Uchaguzi sasa umekwisha, Watanzania sasa tuendelee tuu na maisha yetu ya kawaida as if nothing happened!, ama kwa kusubiria wabunge wengine na madiwani wajitoe tuwarudishe, tuwarudishe kwa mtindo huu huu, au kusubiria uchaguzi wa mwaka 2020 utakaoirudisha rasmi, Tanzania, kuwa nchi ya chama kimoja cha siasa.

Nilibahatika ya kufanya mahojiano na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Ramadhani Kailima, yaliyofanyika ofisini kwake siku za nyuma, kuhusu chaguzi hizi za marudio, katika kipindi changu cha Habari Zaidi ya Habari na PPR, ambacho kinarushwa kupitia Vituo 6 vya TV, TBC, ITV, STAR TV, Channel Ten, Azam TV, Clouds TV na kwenye Youtube.


Hizi ni Baadhi ya Dondoo za Mahojiano Hayo.
  • Zoezi la Uchaguzi limekwenda vizuri kwa asilimia 95%, hakukuwa na kasoro yoyote kubwa kuathiri uchaguzi huo, hivyo uchaguzi umekamilika na taarifa rasmi ya NEC itatolewa punde itakapokamilika.
  • Uchaguzi huo ulikuwa ni uchaguzi huru na wa haki, licha ya kutokea mapungufu madogo madogo, lakini mapungufu kayo, hayajaathiri matokeo, hivyo matokeo halali, aliyeshinda ameshinda kihalali kwa haki, aliyeshindwa, pia ameshindwa kihalali kwa haki katika uchaguzi huru na wa haki.
  • Hakuna hata chama kimoja, kilicholalamikia rasmi jambo lolote kuhusu uchaguzi huo, kwa kujaza rasmi fomu za malalamiko mpaka sasa, Tume ya Taifa ya Uchaguzi, haijapokea malalamiko yoyote rasmi, kutoka chama chochote, au mgombea yoyote kwa mujibu wa utaratibu wa kujaza fomu za malalamiko.
  • Hakuna chama kilichojitoa rasmi, ila kama ilivyo kushiriki uchaguzi ni hiyari, vivyo hivyo vyama viko huru kujitoa wakati wowote, lakini mpaka zoezi la uchaguzi linakamilika, hakuna chama chochote, kilichojitoa rasmi kwa mujibu wa taratibu za kujitoa.
  • Mawakala wa vyama, wanapatikana kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni ikiwepo kutoa barua za utambulisho kwa watu waliokidhi vigezo, mtu ambaye hajakidhi vigezo, hawezi kuruhusiwa.
  • Barua hizo za utambulisho wa mawakala zinakabidhiwa kwa chama husika, na chama ndicho kinawapa mawakala wao.
  • Kukosekana kwa wakala wa chama chochote, hakuathiri uchaguzi, hivyo pamoja na mapungufu madogo madogo ya hapa na pale, uchaguzi ulikuwa huru na wa haki.
  • Ameelezea kuwa Tume yake kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC, ni Tume huru, inayoendesha chaguzi kwa mujibu wa sheria taratibu na kanuni, hakuna chama chochote, kimewahi kulalamikia kipengele chochote cha uchaguzi kinachonyima haki, kitakachoifanya tume hiyo isiwe tume huru.
  • Amesisitiza Tume yake haijawahi kuingiliwa na chombo chochote, wala kupokea maagizo au maelekezo kutoka kwa yeyote.
  • Tume yake haijawahi kufanya upendeleo wowote kwa chama chochote cha siasa, na malalamiko ni kawaida kwa kila anayeshindwa, hata CCM nayo pia huwa inailalamikia tume yake pale inaposhindwa.
  • Pia nimeuliza kuhusu Mkurugenzi, Mwenyekiti wa NEC na makamishna wa Tume kuteuliwa na rais ambaye pia ni mwenyekiti wa chama kimoja, wataweza vipi kutenda haki huku wakiwa ni wateule wa mshindani mmoja?, hili pia Kailima amelijibu, utamsikiliza mwenyewe.
My Take. (Maoni Yangu).
1. Tume yetu ya Uchaguzi NEC, ni Tume Huru, licha ya kuteuliwa na rais ambaye ni Mwenyekiti wa chama kimojawapo, kwa uhuru ule ule wa Mahakama zetu ambazo majaji huteuliwa na rais huyo huyo ambaye pia humteua Mtendaji Mkuu wa Bunge letu. Kama Bunge limeweza kuwa huru kwa mfumo huu, na Mahakama ni huru, hata Tume pia ni huru, ila ionekane kuwa huru, something more needs to be done kwenye Tume Hii.
2. Sheria yetu ya uchaguzi, ina mapungufu makubwa yanayohitaji kufanyiwa marekebisho ili kutoa ushindani wa haki. Tusiilaumu Tume kwa chochote kinachotokea kwa sababu Tume inatekeleza sheria zilizopo, kama ni sheria kandamizi, ni kosa la sheria na aliyezitunga na sio kosa la mtekelezaji.
3. The political game playing field is not level, we need to create a level playing field ili kupata ushindani wa haki. Hili nalo ni tatizo la kikanuni, mfano uchaguzi wa 2020, kuna mgombea mmoja anaingia kwenye kinyanganyiro na vingora, msafara, media, na wasaidizi kibao, huku budget yake is fully footed by state, ashindane na makapuku!, unategemea nini?. Tangu tumeanza uchaguzi wa vyama vingi, kuna chama dola kinashindana na vyama makapuku!.
4. Now it's high time vyama vya siasa, vianze kutake responsibilities kwa matokeo ya utendaji wa vyama vyetu kwenye chaguzi mbalimbali, kwa kukubali kushiriki uchaguzi katika mazingira haya, na tukishindwa kihalali kwenye sanduku la kura, katika uchaguzi huru na wa haki, tukubali matokeo, na sio kutafuta visingizio.
5. Lazima tufike mahali, kwa pale ambapo uchaguzi ulikuwa huru na wa haki licha ya kasoro za hapa na pale, ambazo hazitaathiri, matokeo ya jumla ya uchaguzi huo, tujifunze kukubali matokeo na kushindwa kihalali, asiyekubali kushindwa sio mshindani. Kisha turudi nyuma kujitathmini where did we go wrong. Tulipaswa kufanya nini ili kupata ushindi katika mazingira kama haya.
Conclusion.
The bitter reality kwa wapenda demokrasia wa kweli wa mfumo wa vyama vingi nchini, mimi nikiwemo, tumeshuhudia hali hii ndio uwezo wa ushindani kwa vyama vyetu vya upinzani nchini Tanzania ndio umefikia hapa baada ya miaka 26 ya vyama vingi, naweza kusema kuwa this is the peak ya upinzani Tanzania, upinzani Tanzania, ndio imefika mwisho wake sasa!. Sasa tuanze kujiuliza, jee kama hali ni hii sana, je hali itakuwaje kwa uchaguzi wa 2020?. Kama wapinzani hawatabadili mbinu na strategies, za namna ya kushindana na CCM kwenye ushindani usio sawa kupitia sanduku la kura, then, uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, kuna hatari kubwa kwa CCM, kuyarejesha majimbo yote ya uchaguzi yaliyokuwa yanashikiliwa na upinzani, hivyo kuirudisha Tanzania kuwa ni nchi rasmi ya chama kimoja cha siasa, something which is not healthy at all to true modern democracy!.

Hongereni sana CCM kwa ushindi mtamu.
Poleni sana Chadema/Ukawa kwa kupoteza majimbo, wabunge na madiwani.

Tanzania kama taifa, tujipe pole kwa gharama kubwa za chaguzi hizi, ila tuombe sana Mungu alisaidie taifa letu kama gharama hizi za uchaguzi wa kinachoitwa demokrasia ya uchaguzi huru na wa haki, zinajumuisha, machozi, jasho na damu za Watanzania, kwa kugharimiwa na damu na roho za Watanzania, hakuna namna nyingine yoyote ya fidia kwa damu za watu na roho za watu, zaidi vya karma!'
Nawatakia Jumapili Njema.

Wasalaam.

Paskali
 
Umeyaandika hayo kwa maneno
Ukiambiwa uweke matukio yote utaweza!!.. ni vizuri ukafungua uzi uandike yoteeee tuyajue unayodai..

Nilikuwa busy kweli kweli jana
Ndio nimeona CCM wameshinda kwa kishindo

Ila inajulikana chini ya JPM haiwezi kushangaza.. drama za kulialia za haswa Chadema watu wamezichoka

Wabunge wao hawana la kuonyeshea na kuringia kwa kuleta maendeleo kwa wananchi wao kupiga domo na kujaza matumbo kwa kupenda pesa tu

Hongera kwa Wabunge.. ila walifanya kazi ya kujinadi nafikiti kupita ya 2015.. eeeeeh jasho limewatoka hawatasahau uchaguzi wa jana maishani mwao eeeeeeh

Sasa watende kazi na waliyosema watafanya wayafanye kweli kweli...

Chadema acheni kulalamika hata vikamera vya kuficha hata peni au saa kweli mlishindwa kurekodi kama kweli.. mnaboa
 
Kweli upinzani ubadili mbinu. Mbinu ya kalamu na karatasi kwa wasimamizi ''wanaolipwa" na mwenyekiti wa chama cha mapolisi CCM kati hamtashinda hata kijiji maana watendaji wamepewa onyo la kupoteza ajira. Tafuteni mbinu mbadala
 
Sisi tunashukuru ndugu yetu ameshinda kwani sasa watoto wataendelea na shule vizuri, Alipojiuzuru Hali ilikuwa mbaya Sana kwenye familia, Hongera kaka fitina na majungu Ndio mbinu yetu

Bila wewe kushinda familia ingeishi vipi? Bora kumwaga damu lakini familia ifurahi,
 
Nilikuwa busy kweli kweli jana
Ndio nimeona CCM wameshinda kwa kishindo

Ila inajulikana chini ya JPM haiwezi kushangaza.. drama za kulialia za haswa Chadema watu wamezichoka

Wabunge wao hawana la kuonyeshea na kuringia kwa kuleta maendeleo kwa wananchi wao kupiga domo na kujaza matumbo kwa kupenda pesa tu

Hongera kwa Wabunge.. ila walifanya kazi ya kujinadi nafikiti kupita ya 2015.. eeeeeh jasho limewatoka hawatasahau uchaguzi wa jana maishani mwao eeeeeeh

Sasa watende kazi na waliyosema watafanya wayafanye kweli kweli...

Chadema acheni kulalamika hata vikamera vya kuficha hata peni au saa kweli mlishindwa kurekodi kama kweli.. mnaboa
ndio wakamuua na akwilina
 
Back
Top Bottom