Japo mwaka 2025 unaisha usikate tamaa

Japo mwaka 2025 unaisha usikate tamaa

Nrangoo

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2017
Posts
3,422
Reaction score
5,479
Habari wakuu..

Awali ya yote nimshukuru Mungu Kwa wakati huu aliotujalia na vilevile nitoe pole kwetu sote Watanganyika kwa madhila yaliyotokea wakati wa uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, kila mmoja ameathirika kwa namna moja ama nyingine lakini zaidi kwa familia zilizopoteza wapendwa wao, Mungu azilaze roho zao mahali pema peponi AAMIN.

Ndugu zangu lengo la Uzi huu ni kuendelea kuwatia moyo Vijana wenzangu ambao bado hawajafikia malengo au matarajio Yao katika maisha , wapo wanaotafuta kazi, Wanaotaka kuoa/kuelewa/ kujenga n.k

Nipende kuwaambia kufanikiwa kupo kikubwa wasikate tamaa, mambo ya msingi ya kufanya ni kulinda afya zao za mwili na afya ya akili huku wakiendelea kuweka juhudi kwenye kile kidogo wanachokifanya. Kamwe wasikubali kukatishwa tamaa ingali wako hai.


Mimi nimepitia Msoto hivyo ninaelewa vyema ninachokizungumza , nimekuwa mtaani Kwa zaidi ya miaka kumi baada ya masomo bila shughuli yoyote inyoeleweka , nimepitia masimango ya kutokuwa na shughuli rasmi , nimedhalilika na kudharauliwa Sana, wakati mwingine hata kutengwa kwenye baadhi ya mambo ya kijamii Kwa Sababu Tu kutokuwa na kipato.

Ama hakika nyakati ngumu hazidumu ndugu zangu.

Mwaka 2025 umekuwa mwaka wa Neema Sana Kwa Upande wangu, Kwani nimeweza kupata KAZI nzuri inayoniwezesha kumudu mahitaji yangu muhimu , kusaidia familia na kuweka akiba .

Mwaka 2025 nimeweza kuoa mwanamke aliyekuwa ananipenda nikiwa sina chochote.

Mwaka 2025 nimefanikiwa Kununua kiwanja eneo zuri Tu, mwakani panapo majaliwa nitaanza rasmi Ujenzi.

Kwa Mimi ambaye sikuwa na pa kuanzia popote naona haya kama mafanikio makubwa mno, najua kuna waliofanikiwa pakubwa zaidi lakini kwa haya ya kwangu Mimi ni makubwa.

Namshukuru Sana Mungu , ama kweli nyakati ngumu hazidumu. Tukutane 2026.
 
Malengo ni utumwa

Mimi siweki malengo na sitaki malengo ni UTUMWA
Naishi na ninaenjoy life sina mkataba na maisha!
 
Maisha safi tu, Jf hakuna mlalahoi labda uendeshe hiyo semina mitaani.
 
Back
Top Bottom