Japo kazi ya upinzani ni kupinga, lakini sio kupinga kila kitu. Kwenye maslahi ya taifa, tutangulize utaifa, tuwe wamoja, wakweli na tusipotoshe

Pasco sometimes unachekesha sana! Hivi kuna haja ya kumuunga mkono yeyote anaye sema hadharani kuwa 'lazima yulituze vyema jeshi la polisi kwa vile linafanya Nazi nzuri kwa maslahi mapana ya ccm"?
Unadhani maneno yale yalikuwa ya bahati mbaya? No, alikusudia na Waziri wa sheria juzi kasema tamko LA rais ni sheria.
Watu tujifunze basi juu ya kauli zetu, kwenye AFCON wapenzi wa Mpira Tanzania walipata furaha ya ajabu kuingia zile fainali baada ya miaka 39. Miaka hiyo inamaana zaidi ya nusu ya Watanzania hawakuwepo 1980 kwani walikuwa hawajazaliwa ikiwepo wachezaji wote waliokuwa kule Misri.
Lakini neno moja tuu LA Makonda kwamba Stars inatekeleza Sera za ccm mliona upepo ulivyo badilika! Watanzania wengi wakafikia kuombea kwa uwazi Stars ifungwe.
Why? Ni kauli na matendo ya viongozi ndio yanazalisha upinzani.
Kwa taarifa yako upinzani wa sasa sio Chadema ama CUF au ACT, ni Watanzania wenyewe wakiwamo wana CCM kama tunavyo shuhudia sasa. Hapati usingizi sio kwa sababu ya Mbowe au Zito pekee bali Makamba, Kinana au JK na wengine wavaa kijani.
 
Mkuu, Pascal,
Kwa makala hizi nadhani umesha-qualify uteuzi hata wa ukuu wa wilaya au ukurugenzi siku nafasi itakpopatikana. Ila kwenye CV yako baadhi ya vipengele havijakaa sawa. Naviainisha JAPO VIWILI AU VITATU hapa chini pamoja na ushauri.

Kwanza kazi za ukuu siku hizi ni za kusifia/kupiga mkwala/kuhujumu/kutukana(angalau hata kidogo japo siyo hulka yako)/kujibu mapigo/nk. Kwenye kipengele hiki unaonekana bado hujafanikiwa sana. Nikushauri hizi makala achana nazo. Watu hawana muda wa kusoma mambo maguumu na mareeeefu hivi. Jaribu kuitisha vi-press conference, uwe unajirekodi na kurusha YouTube, hata kwa dakika 5 tu hivi, watu wakusikie unajibu mapigo, wasikie sauti yako, wasikie msimamo wako walau hata kwa dakika chache tu.

Pili, mzee ni mtu wa headlines. Fanya jitihada zozote ziwazo nawe uingizwe kwenye font fedi, zinazobamba na kuvutia wasomaji au wale wanaosafisha macho kwenye vibanda. Hata kwa kuhonga wahariri ikibidi. Wewe ingia font fedi hata kwa kutukana mtu fulani hivi mkubwa. Mfano, nikuhakikishie tu kuwa siku ikisomeka "Mayala, Membe/Zitto hapatoshi" kisha pawekwe picha zenu kama mabondia, ukuu wa wilaya unaukwaa kesho yake tu.

Tatu na mwisho, jitahidi ujipambanue kuwa una chuki za dhati na wapinzani, hasa hasa viongozi wa chadema. Usitake kuwa mstaarabu na kuogopa kuwachana live viongozi wa upinzani. Usidhani kuwa watu wanataka hoja. Hoja alikufa nazo Nyerere. Watu wa kizazi hiki wapo interested na vioja na high dramas.

CHEZA NA WAKATI MKUU/
 
Wanabodi
Huu ni muswada wa makala ya gazeti.
Nimepata fursa kuendeleza zile makala zangu za "Kwa Maslahi Ya Taifa", ambazo ni makala elimishi katika nyanja za kisiasa, kiuchumi na kijamii kwa lengo la kulisaidia taifa letu lisonge mbele. Makala ya leo inazumzia
kazi ya vyama vya upinzani ni kupinga, lakini sio kupinga tuu kila kitu, kunapotokea jambo kubwa lenye maslahi ya taifa, hapa Watanzania wote tunapaswa kuungana na kuwa kitu kimoja, wakiwemo wapinzani, kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa kwa kuwa wakweli, tusipotoshe bali tulisaidie taifa letu kwa michango ya kujenga na kusaidia, na ikitokea serikali iliyoko madarakani inakosea katika jambo la maslahi kwa taifa, serikali inakosolewa constructively kwa kupewa mapendekezo mbadala na sio kwa kubebwa, kutukanwa na kusakamwa.

Rais Magufuli na serikali yake ya awamu ya tano alipoingia tuu madarakani, alitangaza vita nyingi nyingi ikiwemo vita ya dhidi ya rushwa, ufisadi na ubadhirifu kwa tumbua tumbua. Vita dhidi ya ujinga kwa kutoa elimu bure, kuongeza mikopo ya elimu ya juu na kujenga mashule na kuongeza waalimu. Vita dhidi ya maradhi kwa kuongeza bajeti ya afya, kujenga vituo vya afya, zahanati, mahospitali, upatikanaji na usambazaji wa madawa na kuongeza watumishi wa afya. Vita dhidi ya uvivu na uzururaji kwa falsafa yake ya hapa kazi tuu kwa kusisitiza kila mtu afanye kazi. Hata tangazo la kupiga marufuku mikutano ya siasa na maandamano, lengo lake ni zuri, uchaguzi umepita, watu wasikalie tuu kupiga siasa na uzururaji wa maandamano na badala yake watu wafanye kazi.

Kati ya vita zote ambazo Rais Magufuli na serikali yake ameitangaza, vita ngumu ni vita ya kiuchumi ili kupambana na adui umasikini, hii ndio vita kubwa zaidi na ngumu zaidi kuliko vita zote. Rais Magufuli ameigawanya vita hii katika maeneo tofauti tofauti ikiwemo, kujenga Tanzania ya Viwanda, kujenga miondombinu wezeshi, ndio maana tunashuhudia ndege za ATCL zinapaa duniani kote, meli zinajengwa, miradi mikubwa ya reli ya SGR, mabarabara, flyovers, umeme wa Stigler nakadhalika.

Hii vita dhidi ya kulinda rasilimali za taifa ndio vita ngumu kuliko vita zote kwa sababu inahusisha na kupambana na maadui wenye nguvu wakiwemo mabepari wakubwa, makabaila na mabeberu kupitia mashirika makubwa ya kimataifa.
Katika kupambana na vita kwa sekta ya madini, rais Magufuli akasitisha usafirishaji wa mchanga wa dhahabu kwa jina la makinikia, mchanga huo ni wa kampuni ya Acacia ambayo ni kampuni tanzu ya Barrick ya Canada. Tukatunga sheria mpya ya madini kuwa kuanzia sasa, TanzaniaTanzania itamiliki asilimia 16% ya rasilimali zote za ardhini. Hatua hii Tanzania kama nchi tukapata misukosuko ya kutingishwa tulegeze msimamo, ikiwemo ndege zetu kuzuiwa huko Canada, tukapambana hadi ndege zikatoka.

Katika kuutatua mgogoro wa makinikia serikali yetu ikafanya mazungumzo na Barrick yaliyodumu kwa zaidi ya miaka miwili ambapo ni wiki iliyopita tuu ndipo mgogoro huu umemalizika rasmi kwa Barrick kushika hatumu za Acacia hivyo sasa makubaliano yatasainiwa wakati wowote.Mazungumzo haya yalikuwa siri na mkataba pia ulikuwa siri lakini kufuatia wenzetu wazungu kuwa wazi zaidi, katika mauziano ya Barrick na Acacia, mkataba huu ukawekwa wazi na kuzua mijadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii ukiwemo mtandao unaoongoza kwa mijadala, mtandao wa Jamii Forums.

Katika kuujadili mkataba huo baadhi ya wanasiasa wa kambi ya upinzani waki utumia mkataba huo kujipatia umaarufu na kujijenga kisiasa kwa kutumia baadhi ya hoja za ukweli, kuchanganya na uongo na hata kutumia upotoshaji wa makusudi kama kuaminisha watu kuwa huu mkataba tayari umeisha sainiwa kitu ambacho sii kweli bali ni upotoshaji wa makusudi au wa bahati mbaya kutokana na kutokutafsiri vizuri lugha ya Malikia.

Wapenzi wasomaji wangu kwa vile mkataba huu ni wa lugha ya Kiingereza, nitalazimika kutumia baadhi ya maneno ya Kiingereza kwa ajili ya uhalisia

Mhe. Zitto alipoona ile Draft Agreement ikielezwa kuwa imekuwa initialed, akaibuka na upotoshaji kuwa huo mkataba tayari umesainiwa!, kwakwe neno draft agreement amelitafsiri kuwa ndio mkataba halisi, na neno kuwa initialed kwake ametafsiri kuwa huku ndiko kusainiwa kwenyewe!, hizi lugha za watu jamani, zisitufanye kuonekama waongo na wapotoshaji, tuwe wakweli daima, tell the truth and the truth will set you free!.

Mimi niliandika bandiko na kuyasema mazuri ya mkataba huo ni pamoja na
  1. Sasa mgogoro wa Acacia na serikali yetu, umemalizika rasmi kwa sababu sasa Acacia doesnt exist anymore.
  2. Migodi yote mitatu iliyokuwa chini ya Acacia, sasa itakuwa chini ya Barrick
  3. Yale makubaliano ya serikali yetu sasa yatatekelezwa.
  4. Kwa kuanzia tutalipwa dola milioni 300 zilizokuwa ni kishika uchumba, lakini sasa sio kishika uchumba tena bali ni kifuta machozi cha kusamehe lile deni kubwa la kodi la dola bilioni 190.
  5. Barrick ataunda kampuni mpya ya ubia na Tanzania kuchukuwa shughuli za Acacia
  6. Kwenye hiyo kampuni mpya, serikali ya Tanzania itakuwa na shares asilimia 16%.
  7. Bodi ya hiyo kampuni mpya itakuwa na Watanzania.
  8. Makao Makuu yatakuwa Mwanza, Tanzania
  9. Menejiment itakuwa na Watanzania.
  10. Tutagawana manufaa ya kiuchumi pasu kwa pasu, yaani 50/50.(NB.Manufaa ya kiuchumi ni economic benefits na sio faida profits)
  11. Watanzania wenye sifa wataajiriwa nafasi za juu.
  12. Wafanyakazi wa migodi, watasomeshwa elimu ya ujuzi kufikia kiwango cha sisi kuwa na wataalamu wa kila kitu kwenye migodi
  13. Manunuzi makubwa yatafanyika nchini.
  14. Makinikia yatachenjuliwa nchini pale ambapo Tanzania tutaonyesha uwezo.
  15. Migodi itatumia zaidi ya dola milioni 70 kila mwaka kutoa huduma za kijamii, CSR.
Ndipo Mhe. Zitto naya akaibuka na bandiko lenye kichwa cha habari
MAKUBALIANO YA SERIKALI NA BARRICK GOLD CHANGA LA MACHO

Zitto akaandika naomba kunukuu
"Kiambatanisho namba 4 kimeweka muhtasari wa kinachoitwa ‘Material Terms’ katika Makubaliano ya awali kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick Gold ambayo yamesainiwa (INITIALED) mwezi Mei mwaka huu. Kimsingi Barrick imelazimishwa na kanuni za masoko ya mitaji kuweka wazi makubaliano hayo. Ni masikitiko makubwa kuwa Serikali yetu haijathubutu hata kuliambia Bunge kuwa kuna makubaliano ya namna hiyo wakati wa Bunge la Bajeti, imesaini kwa siri kama ulivyosainiwa mkataba wa Buzwagi.

Ikumbukwe kuwa makubaliano hayo yamesainiwa wakati Bunge likiwa linaendelea na mkutano wake jijini Dodoma. Sisi kama wawakilishi wa Wananchi imebidi kusubiri masoko ya mitaji ya ‘MABEBERU’ wa London yaweke wazi masuala yanayohusu nchi yetu.

Ingekuwa nchi nyengine, Makubaliano haya ya KIMANGUNGO kati ya Serikali ya Rais Magufuli na Kampuni ya Barrick, ingetosha kuiondoa Serikali madarakani. Rais John Magufuli na Waziri Palamagamba Kabudi wameuza nchi yetu kwa kipande cha dhahabu. Wamelihujumu Taifa.

Kabwe Z.Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo
Vuga, Zanzibar
Julai 20, 2019" Mwisho wa kunukuu.

Nami nilimjibu naomba kujinukuu
"Mkuu Mhe. Zitto, kwanza asante kwa bandiko hili na uzalendo wako kwa nchi yako. Kwa vile mimi ni miongoni wa wana jf ambao tumeandika sana kuhusu hili, nitachangia baadhi ya vipengele vichache with due respect, na kwa wasiojua lugha ya Malikia, ni kwa heshima na taadhima, tuwe wakweli toka ndani ya nafsi zetu, tuache upotoshaji, just tell the truth and the truth will set you free, sii kweli kuwa mkataba huu umeisha sainiwa!, hilo neno (INITIALED) sio kuonyesha kuwa umesainiwa, bali katika mikataba, kunatakiwa signatories watie initials zao kwenye kila page ya draft kuonyesha wameelewa, lakini draft ni draft na mkataba ni mkataba!, ku INITIALED sio kusaini.

Hicho kiambanisho 4 ni draft, na mimi nimekiweka kwenye bandiko langu kuhusu kununuliwa kwa kampuni yang Acacia

Huu ndio utakuwa ushindi wa kwanza wa kishindo wa rais Magufuli na awamu ya tano katika vita dhidi ya rasilimali madini na ndio kuanza rasmi utekelezaji wa kwanza wa sheria mpya ya madini.
Hongera Prof. Kabudi, Hongera Rais Dr. Magufuli na Hongera sisi Watanzania wote katika ujumla wetu japo kwenye hili la makinikia, bado kuna mambo hayajakaa vizuri.

Hatuwezi kusema kila kitu mpaka baada ya kusainiwa kwa makubaliano hayo, na nikasisitiza kwenye makinikia kuna lakini sikuiweka hiyo lakini kwa sababu bado hatujaona makubaliano yaliyofikiwa, hayo ni mapendekezo tuu, yaani draft, siku zote drafts zote huwa ni tentative, inaweza kubadilika, hivyo naomba kusisitiza katika hili tuwe wakweli, tuvute subra na tutumie ukweli, tuache upotoshaji!. Japo pia nakiri baadhi yang hoja za Zitto zina mashiko na zilitasaidia sana taifa kuboresha makubaliano haya kabla hayajasainiwa.

Sijamuita Zitto mpotoshaji, nimesema kwenye hoja zake kuna upotoshaji. Kwa vile Zitto namfahamu fika toka enzi zetu za UDSM, hivyo naifahamu intelect ya Zitto, haiwezekani katika kiambatanisho hicho, awe hayajaona maneno haya
"Appendix 4 Summary of the material terms of the current draft documentation under discussion (but not yet finalised) with the GoT The discussions between Barrick and the GoT have advanced to the point where draft documentation was initialled by the GoT on 19 May 2019". Hapa maana yake hii ni draft tuu imekuwa initialled na GOT lakini haijawa finalized, kwa Zitto ninayemjua mimi, haiwezekani Zitto awe hakuyaona maneno haya.

Kwenye document hiyo, kuna maneno ya capital letters na bold
"THERE IS NO CERTAINTY THAT THE TRANSACTION DOCUMENTS WILL BE AGREED WITH THE GOT IF THE SCHEME BECOMES EFFECTIVE AND THE TERMS OF THE FINAL FORM OF TRANSACTION DOCUMENTS, IF AGREED, MAY DIFFER FROM THOSE SUMMARIZED BELOW."
Siamini kuwa Zitto hakuyaona maneno haya, kwa wasio jua lugha ya Malikia ni "hakuna uhakika kama makubaliano haya yatakubaliwa na GOT, na hata yakikubaliwa, yanaweza kuwa ni tofauti na kilichokubaliwa hapa!. Hivyo Zitto kusema ni mkataba umesainiwa, huu sio sahihi, ni upotoshaji kwa makusudi tuu sio kuwa hakuona mistari hiyo!.

Kwenye kipengele cha 11 cha makubaliano hayo kinasema wazi kuwa
"11. The conditions set out in (a) to (g) of paragraph A10 above may be waived by the Acacia parties and the conditions set out in (h) to (i) of paragraph A10 above may be waived by the GoT. "
Hapa wanasema masharti ya mkataba huu yaliyowekwa kwa ibara ya 10, yanaweza kukubaliwa au kukataliwa na Acacia, au na GOT kuthibitisha kuwa makubaliano haya sio final and conclusive, haiwezekani Zitto ninayemjua mimi, hakuliona hili!.

Kipengele cha 12 kinasema
"12. Those provisions which are stated to become effective on signing of the Framework Agreement"
Hapa kwa lugha ya Malkia ni masharti hayo, yatatakiwa kutekelezwa baada ya kusaibiwa kwa makubaliano hayo, bado hakuna makubaliano yoyote yaliyosainiwa!. Siamini kuwa Zitto hakuliona hilo.

Kwenye kiambatisho hicho kuna hii para
"The discussions between Barrick and the GoT have advanced to the point where draft documentation was initialled by the GoT on 19 May 2019, albeit with a number of substantive issues still outstanding which are subject to further discussion. Whilst a basis for settlement has been developed, the terms have not yet been finalised"
Naamini kabisa Zitto anajua maana ya maneno hayo, hawa jamaa wanasema bado kuna issues ni still outstanding na zinahitaji majadiliano zaidi.

Sasa ili kumtendea haki Mhe. Zitto, naomba kuziweka hoja zake zote 5 na kusema hoja zipi ni za kweli na hoja zipi ni za upotoshaji tuu.

1. Zitto Anasema: Dola Milioni 300 za kumaliza mgogoro KIINI MACHO
Serikali imekubaliana na Barrick kuwa italipwa Dola milioni 300 (wastani wa TZS 700 Bilioni) kama malipo ya kumaliza mgogoro wote (full, final and complete settlement) na SIO kishika uchumba kama Serikali ilivyoeleza umma. Barrick watalipa fedha hizi kwa muda wa MIAKA 7 na zitakuwa ni baada ya kuondoa madai yote ya kodi ambayo Acacia inaidai Tanzania.

Itakumbukwa kuwa Acacia Group ina madai ya marejesho ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT refunds) inayofikia takribani Dola za Marekani milioni 240 (wastani wa 552 Bilioni). Hivyo katika malipo ya Dola za Marekani Milioni 300, zitakazobakia baada ya kutoa madai ya VAT refunds ni Dola Milioni 60 (wastani wa 138 Bilioni) tu. Kama tutakavyoona katika hoja ya pili hapa chini hata hizi Dola za Marekani Milioni 60 kimsingi hazitatolewa.

Kwenye hoja hii Zitto kuna sehemu amesema kweli, hapa tumepigwa. lakini kuna sehemu Zitto sio tuu hakusema kweli bali amepotosha. Kwa vile Mhe. Zitto ni Mbunge akisema kitu ndipo watu wanakizingatia na kukitilia maanani, hivyo hii observation ya Zitto will make a big impact kwenye the final draft. Na hili la dola milioni 300 ndio kalipotosha wakati sisi akina kajamba nani, ma lumpen proletariat' hili tuliliona kitambo na tukalisemea sana humu, because we are nobody, no one heard lakini sasa kulisemea Zitto, kila mtu atasikia.

Baada ya Barrick kuinunua Acacia, ni kweli tutalipwa kifuta machozi cha dola milioni 300, sii kweli kuwa malipo haya yatatolewa baada ya kuondoa VAT refund, bali kweli kuwa malipo haya yatalipwa katika kipindi cha miaka 7.
Tukiisha saini tuu mkataba, tutalipwa upfront ya dola milioni 100. Hivyo hoja ya Zitto kuwa kwenye dola milioni 300, tutaambulia dola milioni 60 sii kweli. Ile siku Barrick wanakuja kusaini mkataba, ile kuangusha tuu wino kusaini, kitita cha dola milioni 100 kinawekwa mezani as upfront payment kama ilivyoelezwa hapa
"There will be an initial upfront “payment” by way of assignment to the GoT of minerals contained in containers at Dar es Salaam port with a value of US$100 million". Shilingi milioni 200 zilizobakia, ndizo zitalipwa katika mikupuo 6 ya dola milioni 33.33 kwa mwaka katika miaka 6.

Pamoja ya Zitto kutokuwa mkweli, lakini ukweli wa Zitto kuwa tunapigwa uko pale pale. Tunapigwa kwa sababu hizi dola milioni 300, tuliahidiwa as goodwill money, hasikupaswa kuwa conditional wala hazikupaswa kulipwa kido kidogo, zilipaswa kulipwa there and then.

Kitu cha pili kwa vile hiki kilikuwa ni kishika uchumba tuu na kuonyeshea goodwill ya kulipia mahari kamili ya binti yetu ambayo ni dola bilioni 190, lakini serikali yetu imesamehe mahari yote, na kile kishika uchumba sasa ndio kigeuzwa kifuta machozi, hapa sasa ndipo tulipopigwa!. Hapa nilishauri serikali yetu lazima itufafanulie Watanzania the basis ya msamaha huu.

2. Zitto Anasema: Barrick Gold Wamesamehewa Kodi ya Ongezeko la Mtaji USD 85.6M
Serikali ya Tanzania imetoa misamaha mbalimbali ya Kodi kwa Kampuni ya Barrick Gold katika makubaliano yaliyoingiwa ikiwemo kodi ya ‘Capital Gains’ ambayo inatokana na mauzo ya hisa za Acacia kwa Barrick. Itakumbukwa kuwa mwaka 2012 Bunge lilitunga sheria ya kutoa Kodi ya Ongezeko la Mtaji kwa mauzo ya mali zilizopo Tanzania ili kudhibiti ukwepaji wa Kodi.

Barrick inainunua Acacia kwa Hisa ambazo Barrick haikuwa inamiliki ambazo zimepewa thamani ya Dola Milioni 428. Capital Gains Tax ya 20% ilipaswa kulipwa lakini Rais Magufuli na Profesa Kabudi wametoa ‘waiver’ (Msamaha) na kupoteza Mapato halali na ya kisheria kwa nchi yetu ya Dola Milioni 85.6 (wastani wa TZS 200 Bilioni). Tukirejea hoja ya kwanza hapo juu utaona kuwa sio tu Tanzania kiuhalisia haitapata Dola Milioni 300, bali pia tunaipa zawadi Barrick ya Dola Milioni 25.6 (wastani wa TZS 59 Bilioni) za ziada.

Mimi nimejibu: Hili ni kweli, hawa wamesamehewa na ni kawaida kwa serikali yetu kutoa misamaha ya aina hii kwa kutotoza capital gain tax kwenye acquisitions kibao, au kwenye hostile take overs,
Celtel ilibadilika kuwa Zain, ikabadilika kuwa Airtel, hakuna tulicholipwa!.
Sheraton ilibadilika kuwa Moven Pick, Royal Palm sasa Serena sijui kama tulilipwa kitu!.
Mobitel, iligeuka kuwa Tigo sijui kama tulilipwa kitu!.
Kibo Breweries ilikuwa taken over kwenye hostile take over, sijui kama tulilipwa kitu, hivyo hapa Zitto is right, but its not the first time, kama kule kuingine tumetoa misamaha hiyo, why not now?.

Zitto amesema:Tanzania kupewa Hisa 16% za daraja B lakini Watanzania kunyimwa umiliki wa 30% kupitia Soko la Hisa la DSE
Ni kweli kuwa Serikali itapewa hisa za bure 16% kwenye Kampuni tanzu zote za Acacia hapa nchini kama tulivyoambiwa na Serikali. Lakini hisa hizo ni za Daraja la B ambazo ni hisa dhaifu kulinganisha na zile za Daraja la kwanza. Hisa hizo haziruhusiwi kuuzwa, hazina kura kwa masuala fulani fulani ya Kampuni na huwezi hata kuziweka kama dhamana ya mikopo. Hata mgawo wa gawio hisa hizi hupata baada ya wale wa daraja A kulipwa kwa ukamilifu.

Licha ya makubaliano haya ya hovyo na yasiyo na tija, Serikali yetu imetoa ‘waiver’ (msamaha) kwa Barrick kutoorodhesha hisa kwenye Soko la Hisa la Tanzania. Sheria ya Madini ya mwaka 2010 (Wakati wa Waziri William Ngeleja) na Kanuni zake iliweka sharti kwamba ni lazima makampuni ya madini yauze 30% ya hisa kwa Watanzania kwenye soko la Hisa la Tanzania.

Makubaliano ya Mei 2019 kati ya Barrick na Serikali ya Tanzania yametoa msamaha kwa Barrick kutekeleza sharti hilo la kisheria. Uamuzi huu unavunja sheria za nchi, ni hujuma kwa Watanzania kumiliki maliasili zao na ni ukosefu wa maarifa ya kiuchumi kwa kiwango kisichomithilika wala kuvumilika.

Mimi Nimejibu: Hili la hisa za daraja B ni kweli lakini sii kweli kuwa Watanzania tumenyimwa umiliki wa 30% kupitia DSE!.
Hizi hisa aslimia 16 za Tanzania, ni free carried shares, tumepewa bure, na kote free carried shares huwa haziuzwi ila sii kweli kuwa hazina voting rights. Pia sii kweli kuwa Watanzania tumenyimwa umiliki wa 30% kupitia DSE!.
Naomba hapa ikumbukwe, shares zinazouzwa ni shares za Acacia zinazo trade kwenye London Stock Exchange tuu, hata yale mambo ya PUSU ni mambo yao, sijasikia lolote kuhusu shares za Acacia zinazo trade kwenye DSE, hivyo business ya hisa za Acacia ndani ya DSE zinaendelea as usual.Hata baada ya sale kukamilika, hivyo kampuni mpya italazimika kuuza 30% ya hisa zake kwenye DSE na Watanzania wenye fedha, watakuwa free kununua hisa hizo kwenye soko.

Tukija kwenye voting rights, sii kweli kuwa Tanzania hatuna voting rights, bali ni kawaida kwa free shares zote hazina voting rights ya pro rata ya share to shares bali tuna voting rights za block shares. Sisi Tanzania wenye free carried shares za 16%, serikali yetu iteteua mjumbe mmoja wa bodi ambaye ni Mtanzania, ataingia na kuwa mjumbe wa bodi ya hiyo kampuni mpya, kwa zile asilimia 16% za shares zetu na ndani ya kikao cha bodi, atakuwa na voting righs za kupiga kura 1 as a block vote kuwakilisha zile shares 14, wakati wajumbe wengine wa bodi, watakaowakilisha zile subscribed shares za asilimia 84%, wanatakuwa na voting rights ya votes 84 kwa uwiano wa share to shares votes pro rata according to shares subscription. Hivyo ndani ya bodi ya hiyo kampuni Mtanzania atakayeingia humo, atakuwa anapiga kura moja kuwakilisha the block ya zile shares zetu 16 za bure, na katika mgao wa faida, sii kweli kuwa tutapata mgao baada ya wale wengine, huu ni uongo!, Tanzania tunagaiwa mgao sawa kabisa wa faida kwa mujibu wa shares hizo.

Kwa wasio jua kuhusu shares za group A na group B shares za group A ni shares za watu walio invest kwa kutoa fedha zao kununua shares, yaani subscribed shares, na shares group B ni shares za heshima, shares za hisani zinazotolewa bure, shares hizi za hisani haziruhusiwi kuuzwa, wala kuwa disposed or transferred na zina block votes rights. Hili hufanyika kwa makampuni kuwapa hisa za heshima land owners, mfano UAE, hakuna foreigner anayeruhusiwa kumiliki ardhi, ardhi yote ni ya wazawa, hivyo investor akija lazima aingie ubia na wazawa mzawa anatoa land, investo ana jenga, kama alivyofanya Rugemalila kwenye IPTL alitoa ardhi yake na kupewa 30 m% ya shares, IPTL ikaikwa kwa PAP, Ruhemalila akalipwa shares zake, akagawa fedha zake, sasa anateswa bure bila kosa lolote!.

Zitto Amesema: Bunge lafungwa mikono kubadili sheria yeyote
Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick wamekubaliana kuwa baada ya mkataba wao kukamilika Bunge la Tanzania haliwezi kutunga sheria yeyote ambayo itabadili makubaliano hayo na kodi zote zilizokuwa zinafanya kazi wakati wa kuingia makubaliano hazitaweza kubadilishwa kipindi chote ambacho Barrick watakuwa wanafanya kazi Tanzania (fiscal stabilisation).

Makubaliano ya namna hii ndiyo kitu kilicholeta Buzwagi mwaka 2007 ambapo Serikali za Rais Mkapa na Rais Kikwete ziliingia mikataba ya kulifunga Bunge kutimiza majukumu yake ya kikatiba kama Dola (sovereign). Sheria ya Madini yam waka 2010 iliondoa sharti hili kufuatia mapendekezo ya Kamati ya Bomani. Rais Magufuli na Waziri Kabudi wameturudisha kwenye unyonyaji wa kihayawani kabisa.

Mimi nimejibu: Kwenye hili pia Zitto hajasema kweli, kwenye document hii yenye kurasa 91, hakuna popote Bunge la JMT limetajwa!. Makubaliano haya yatatawaliwa na sheria za Tanzania. Hakuna popote Bunge limetajwa, bali kilisemwa ni maadam sheria iliyotungwa ninaelekeza free carried shares ni asilimia 16%, baada ya kusainiwa kwa makubaliano haya, serikali haiwezi kuongeza kile kiwango cha shares zaidi ya asilimia 16% za kisheria unilateral, kama ilivyofanya kwa sheria mpya ya madini "the GoT will not unilaterally seek to increase its share ownership or economic participation rights in the TMC", hii maana yake, serikali haiwezi kujiamua yenyewe pekee bila kuishirikisha Barrick.

Hili mimi nililizungumzia kitambo ile tuu tunabadili sheria, kuwa kisheria, sheria yoyote ambayo ni sheria nzuri, inaanza kufanya kazi tangu pale inapotungwa. Sheria yoyote inayotungwa halafu ina act retrorespect is a bad law. Hivyo tulipopitisha sheria mpya, nikasema tuwashukuru sana Barrick wamekubali kuanza upya kwa sheria mpya, Hakuna mwingine yoyote mwenye mkataba wa zamani amekubali kubadili na kutumia sheria mpya na hatuwezi kuwalazisha.

Zitto amesema: Barrick wameruhusiwa kufungua kesi ughaibuni kinyume na Sheria

Kwa mujibu wa sheria mpya za madini za mwaka 2017 makampuni yamezuiliwa kufungua mashauri yake nje ya Tanzania. Migogoro yote inapaswa kushughulikiwa na mahakama za ndani ya nchi. Serikali ya Tanzania imekubaliana na Barrick kuwa migogoro itafanyika kwa mujibu wa kanuni za UNICITRAL na Rais wa Kituo cha usuluhishi wa migogoro cha Singapore ndio atateua wasuluhishi ambao hapatakuwa na Mtanzania.

Mimi nimejibu: Kwenye hili, Zitto yuko right 100% kipengele kwenye sheria yetu mpya kinachokataza usuluhisi nje ya Tanzania ni hiki
View attachment 1159270

Ile siku sheria hii inapitishwa Bungeni, mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Waziri Kivuli wa sheria, Tundu Lissu, alionya kuhusu hili kuwa hatuwezi kupitisha sheria ambayo hatuwezi kuitekeleza and soon tutakuja kuifanyia marekebisho. Hivyo hapa Zitto yuko right, makubaliona haya ni kinyume cha sheria, hivyo ni illegal.
Hitimisho.
Kuwa Upinzani basic kazi yake iwe ni kupinga tuu kila kitu, kiwe kizuri kiwe kibaya wao ni kuinga tuu. Kazi rasmi ya upinzani sii kupinga tuu, bali ni kupinga kuonyesha makosa na
kwa hoja mbadala za ukweli na sio kwa hoja za uongo na upotoshaji na kwenye jambo lenye maslahi kwa taifa kama hili la rasilimali madini, Wapinzani, CCM, SerikalI na Watanzania wote tusimame as one tuongee kwa sauti moja.
Wito kwa Wapinzani: Sio kupinga tuu kila kitu, kwenye maslahi ya Taifa tuwe kitu kimoja.
Wito kwa Serikali: Ikubali Kusisitiza hoja za msingi za upinzani na kuzifanyia kazi.
Tanzania ni nchi yetu sote, sio Tanzania ya CCM pekee au Tanzania ya serikali ni
Tanzania ya Watanzania wote wakiwemo CCM, serikali, wapinzani na hata akina sisi tusio na vyama, let's stand as one.

Jumatatu njema
Paskali
Rugemalila kwenye IPTL alitoa ardhi yake na kupewa 30 m% ya shares, IPTL ikaikwa kwa PAP, Ruhemalila akalipwa shares zake, akagawa fedha zake, sasa anateswa bure bila kosa lolote!.

ARE YOU SURE
 
Wanabodi
Huu ni muswada wa makala ya gazeti.
Nimepata fursa kuendeleza zile makala zangu za "Kwa Maslahi Ya Taifa", ambazo ni makala elimishi katika nyanja za kisiasa, kiuchumi na kijamii kwa lengo la kulisaidia taifa letu lisonge mbele. Makala ya leo inazumzia
kazi ya vyama vya upinzani ni kupinga, lakini sio kupinga tuu kila kitu, kunapotokea jambo kubwa lenye maslahi ya taifa, hapa Watanzania wote tunapaswa kuungana na kuwa kitu kimoja, wakiwemo wapinzani, kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa kwa kuwa wakweli, tusipotoshe bali tulisaidie taifa letu kwa michango ya kujenga na kusaidia, na ikitokea serikali iliyoko madarakani inakosea katika jambo la maslahi kwa taifa, serikali inakosolewa constructively kwa kupewa mapendekezo mbadala na sio kwa kubebwa, kutukanwa na kusakamwa.

Rais Magufuli na serikali yake ya awamu ya tano alipoingia tuu madarakani, alitangaza vita nyingi nyingi ikiwemo vita ya dhidi ya rushwa, ufisadi na ubadhirifu kwa tumbua tumbua. Vita dhidi ya ujinga kwa kutoa elimu bure, kuongeza mikopo ya elimu ya juu na kujenga mashule na kuongeza waalimu. Vita dhidi ya maradhi kwa kuongeza bajeti ya afya, kujenga vituo vya afya, zahanati, mahospitali, upatikanaji na usambazaji wa madawa na kuongeza watumishi wa afya. Vita dhidi ya uvivu na uzururaji kwa falsafa yake ya hapa kazi tuu kwa kusisitiza kila mtu afanye kazi. Hata tangazo la kupiga marufuku mikutano ya siasa na maandamano, lengo lake ni zuri, uchaguzi umepita, watu wasikalie tuu kupiga siasa na uzururaji wa maandamano na badala yake watu wafanye kazi.

Kati ya vita zote ambazo Rais Magufuli na serikali yake ameitangaza, vita ngumu ni vita ya kiuchumi ili kupambana na adui umasikini, hii ndio vita kubwa zaidi na ngumu zaidi kuliko vita zote. Rais Magufuli ameigawanya vita hii katika maeneo tofauti tofauti ikiwemo, kujenga Tanzania ya Viwanda, kujenga miondombinu wezeshi, ndio maana tunashuhudia ndege za ATCL zinapaa duniani kote, meli zinajengwa, miradi mikubwa ya reli ya SGR, mabarabara, flyovers, umeme wa Stigler nakadhalika.

Hii vita dhidi ya kulinda rasilimali za taifa ndio vita ngumu kuliko vita zote kwa sababu inahusisha na kupambana na maadui wenye nguvu wakiwemo mabepari wakubwa, makabaila na mabeberu kupitia mashirika makubwa ya kimataifa.
Katika kupambana na vita kwa sekta ya madini, rais Magufuli akasitisha usafirishaji wa mchanga wa dhahabu kwa jina la makinikia, mchanga huo ni wa kampuni ya Acacia ambayo ni kampuni tanzu ya Barrick ya Canada. Tukatunga sheria mpya ya madini kuwa kuanzia sasa, TanzaniaTanzania itamiliki asilimia 16% ya rasilimali zote za ardhini. Hatua hii Tanzania kama nchi tukapata misukosuko ya kutingishwa tulegeze msimamo, ikiwemo ndege zetu kuzuiwa huko Canada, tukapambana hadi ndege zikatoka.

Katika kuutatua mgogoro wa makinikia serikali yetu ikafanya mazungumzo na Barrick yaliyodumu kwa zaidi ya miaka miwili ambapo ni wiki iliyopita tuu ndipo mgogoro huu umemalizika rasmi kwa Barrick kushika hatumu za Acacia hivyo sasa makubaliano yatasainiwa wakati wowote.Mazungumzo haya yalikuwa siri na mkataba pia ulikuwa siri lakini kufuatia wenzetu wazungu kuwa wazi zaidi, katika mauziano ya Barrick na Acacia, mkataba huu ukawekwa wazi na kuzua mijadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii ukiwemo mtandao unaoongoza kwa mijadala, mtandao wa Jamii Forums.

Katika kuujadili mkataba huo baadhi ya wanasiasa wa kambi ya upinzani waki utumia mkataba huo kujipatia umaarufu na kujijenga kisiasa kwa kutumia baadhi ya hoja za ukweli, kuchanganya na uongo na hata kutumia upotoshaji wa makusudi kama kuaminisha watu kuwa huu mkataba tayari umeisha sainiwa kitu ambacho sii kweli bali ni upotoshaji wa makusudi au wa bahati mbaya kutokana na kutokutafsiri vizuri lugha ya Malikia.

Wapenzi wasomaji wangu kwa vile mkataba huu ni wa lugha ya Kiingereza, nitalazimika kutumia baadhi ya maneno ya Kiingereza kwa ajili ya uhalisia

Mhe. Zitto alipoona ile Draft Agreement ikielezwa kuwa imekuwa initialed, akaibuka na upotoshaji kuwa huo mkataba tayari umesainiwa!, kwakwe neno draft agreement amelitafsiri kuwa ndio mkataba halisi, na neno kuwa initialed kwake ametafsiri kuwa huku ndiko kusainiwa kwenyewe!, hizi lugha za watu jamani, zisitufanye kuonekama waongo na wapotoshaji, tuwe wakweli daima, tell the truth and the truth will set you free!.

Mimi niliandika bandiko na kuyasema mazuri ya mkataba huo ni pamoja na
  1. Sasa mgogoro wa Acacia na serikali yetu, umemalizika rasmi kwa sababu sasa Acacia doesnt exist anymore.
  2. Migodi yote mitatu iliyokuwa chini ya Acacia, sasa itakuwa chini ya Barrick
  3. Yale makubaliano ya serikali yetu sasa yatatekelezwa.
  4. Kwa kuanzia tutalipwa dola milioni 300 zilizokuwa ni kishika uchumba, lakini sasa sio kishika uchumba tena bali ni kifuta machozi cha kusamehe lile deni kubwa la kodi la dola bilioni 190.
  5. Barrick ataunda kampuni mpya ya ubia na Tanzania kuchukuwa shughuli za Acacia
  6. Kwenye hiyo kampuni mpya, serikali ya Tanzania itakuwa na shares asilimia 16%.
  7. Bodi ya hiyo kampuni mpya itakuwa na Watanzania.
  8. Makao Makuu yatakuwa Mwanza, Tanzania
  9. Menejiment itakuwa na Watanzania.
  10. Tutagawana manufaa ya kiuchumi pasu kwa pasu, yaani 50/50.(NB.Manufaa ya kiuchumi ni economic benefits na sio faida profits)
  11. Watanzania wenye sifa wataajiriwa nafasi za juu.
  12. Wafanyakazi wa migodi, watasomeshwa elimu ya ujuzi kufikia kiwango cha sisi kuwa na wataalamu wa kila kitu kwenye migodi
  13. Manunuzi makubwa yatafanyika nchini.
  14. Makinikia yatachenjuliwa nchini pale ambapo Tanzania tutaonyesha uwezo.
  15. Migodi itatumia zaidi ya dola milioni 70 kila mwaka kwa CSR.
Zitto amesema:Tanzania kupewa Hisa 16% za daraja B lakini Watanzania kunyimwa umiliki wa 30% kupitia Soko la Hisa la DSE
Ni kweli kuwa Serikali itapewa hisa za bure 16% kwenye Kampuni tanzu zote za Acacia hapa nchini kama tulivyoambiwa na Serikali. Lakini hisa hizo ni za Daraja la B ambazo ni hisa dhaifu kulinganisha na zile za Daraja la kwanza. Hisa hizo haziruhusiwi kuuzwa, hazina kura kwa masuala fulani fulani ya Kampuni na huwezi hata kuziweka kama dhamana ya mikopo. Hata mgawo wa gawio hisa hizi hupata baada ya wale wa daraja A kulipwa kwa ukamilifu.

Licha ya makubaliano haya ya hovyo na yasiyo na tija, Serikali yetu imetoa ‘waiver’ (msamaha) kwa Barrick kutoorodhesha hisa kwenye Soko la Hisa la Tanzania. Sheria ya Madini ya mwaka 2010 (Wakati wa Waziri William Ngeleja) na Kanuni zake iliweka sharti kwamba ni lazima makampuni ya madini yauze 30% ya hisa kwa Watanzania kwenye soko la Hisa la Tanzania.

Makubaliano ya Mei 2019 kati ya Barrick na Serikali ya Tanzania yametoa msamaha kwa Barrick kutekeleza sharti hilo la kisheria. Uamuzi huu unavunja sheria za nchi, ni hujuma kwa Watanzania kumiliki maliasili zao na ni ukosefu wa maarifa ya kiuchumi kwa kiwango kisichomithilika wala kuvumilika.

Mimi Nimejibu: Hili la hisa za daraja B ni kweli lakini sii kweli kuwa Watanzania tumenyimwa umiliki wa 30% kupitia DSE!.
Hizi hisa aslimia 16 za Tanzania, ni free carried shares, tumepewa bure, na kote free carried shares huwa haziuzwi ila sii kweli kuwa hazina voting rights. Pia sii kweli kuwa Watanzania tumenyimwa umiliki wa 30% kupitia DSE!.
Naomba hapa ikumbukwe, shares zinazouzwa ni shares za Acacia zinazo trade kwenye London Stock Exchange tuu, hata yale mambo ya PUSU ni mambo yao, sijasikia lolote kuhusu shares za Acacia zinazo trade kwenye DSE, hivyo business ya hisa za Acacia ndani ya DSE zinaendelea as usual.Hata baada ya sale kukamilika, hivyo kampuni mpya italazimika kuuza 30% ya hisa zake kwenye DSE na Watanzania wenye fedha, watakuwa free kununua hisa hizo kwenye soko.

Tukija kwenye voting rights, sii kweli kuwa Tanzania hatuna voting rights, bali ni kawaida kwa free shares zote hazina voting rights ya pro rata ya share to shares bali tuna voting rights za block shares. Sisi Tanzania wenye free carried shares za 16%, serikali yetu iteteua mjumbe mmoja wa bodi ambaye ni Mtanzania, ataingia na kuwa mjumbe wa bodi ya hiyo kampuni mpya, kwa zile asilimia 16% za shares zetu na ndani ya kikao cha bodi, atakuwa na voting righs za kupiga kura 1 as a block vote kuwakilisha zile shares 16%, wakati wajumbe wengine wa bodi, watakaowakilisha zile subscribed shares za asilimia 84%, wanatakuwa na voting rights ya votes 84 kwa uwiano wa share to shares votes pro rata according to shares subscription. Hivyo ndani ya bodi ya hiyo kampuni Mtanzania atakayeingia humo, atakuwa anapiga kura moja kuwakilisha the block ya zile shares zetu 16 za bure, na katika mgao wa faida, sii kweli kuwa tutapata mgao baada ya wale wengine, huu ni uongo!, Tanzania tunagaiwa mgao sawa kabisa wa faida kwa mujibu wa shares hizo.

Kwa wasio jua kuhusu shares za group A na group B shares za group A ni shares za watu walio invest kwa kutoa fedha zao kununua shares, yaani subscribed shares, na shares group B ni shares za heshima, shares za hisani zinazotolewa bure, shares hizi za hisani haziruhusiwi kuuzwa, wala kuwa disposed or transferred na zina block votes rights. Hili hufanyika kwa makampuni kuwapa hisa za heshima land owners, mfano UAE, hakuna foreigner anayeruhusiwa kumiliki ardhi, ardhi yote ni ya wazawa, hivyo investor akija lazima aingie ubia na wazawa mzawa anatoa land, investo ana jenga, kama alivyofanya Rugemalila kwenye IPTL alitoa ardhi yake na kupewa 30 m% ya shares, IPTL ikaikwa kwa PAP, Ruhemalila akalipwa shares zake, akagawa fedha zake, sasa anateswa bure bila kosa lolote!
Paskali
Tueleze mchakato wa dividend ya 16% shares,

Hizo ndo issue za kujadili ili tujue tunanufaika au tunadanganywa na figure,
Karibu
P
 
Leo ndio huu mkataba umesainiwa rasmi, tunasubiri kupata contents za tulichokubaliana, ili tuweze kudadavua.
P
 
Wanabodi
kazi ya vyama vya upinzani ni kupinga, lakini sio kupinga tuu kila kitu, kunapotokea jambo kubwa lenye maslahi ya taifa, hapa Watanzania wote tunapaswa kuungana na kuwa kitu kimoja, wakiwemo wapinzani, kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa kwa kuwa wakweli, tusipotoshe bali tulisaidie taifa letu kwa michango ya kujenga na kusaidia, na ikitokea serikali iliyoko madarakani inakosea katika jambo la maslahi kwa taifa, serikali inakosolewa constructively kwa kupewa mapendekezo mbadala na sio kwa kubezwa, kutukanwa na kusakamwa.
Paskali
Hata hili janga la korona ni janga la kitaifa, hivyo Watanzania tushikamane, tusimame as one. Wapinzani, toeni Ushirikiano kwa serikali katika hatua pendekezwa kuzuia kuenea kwa janga hili ikiwemo kutokuwepo kwa mikusanyiko.
Together we can.
P
 
Wanabodi
Wito kwa Wapinzani: Sio kupinga tuu kila kitu, kwenye maslahi ya Taifa tuwe kitu kimoja.
Wito kwa Serikali: Ikubali Kusisitiza hoja za msingi za upinzani na kuzifanyia kazi.
Tanzania ni nchi yetu sote, sio Tanzania ya CCM pekee au Tanzania ya serikali ni
Tanzania ya Watanzania wote wakiwemo CCM, serikali, wapinzani na hata akina sisi wenye vyama kimya kimya, let's stand as one.
Paskali
Vurugu za uchaguzi zinazokwamisha maendeleo ni tabia mbaya za wapinzani kupinga kila kitu hata mambo ya msingi, na moja ya matatizo makubwa ya uchaguzi ni kwa wapinzani wanaposhindwa, wanagoma kukubali matokeo.
Natoa wito kwa wapinzani, mkishindwa kihalali, kubalini matokeo.
P
 
Ungeni mkono japo kidogo enyi CDM! sio kila kitu mnakipiga 'tanchi'.
Mkuu kinje ketile , naunga mkono hoja, Chadema ni upinzani uchwala tuu, kila kitu kupinga, hata kufanyike mazuri vipi wao hawayaoni, Jicho lao linaona mabaya tuu na mapungufu tuu!, lakini mema na mazuri hawayaoni!.

Kiongozi hatuwezi kuwa na mtazamo sawa. Japo mimi ni mwana CCM, lakini siwezi waambia upinzani ungeni mkono hili na lile linalofanywa nasi. Kwani sisi CCM tumeshawahi unga mkono jambo gani la upinzani? Mbona kila wazo hata zuri huwa tunapinga hadharani? Baadhi huwa tunayachukua juu juu, kimya kimya na kujifanya ni mawazo yetu wala hatukiri tumekwapua upande wa pili? Hii kitu ya kupinga kila kitu iko pande zote.
 
Wanabodi
Kuwa Upinzani basic kazi yake iwe ni kupinga tuu kila kitu, kiwe kizuri kiwe kibaya wao ni kupinga tuu. Kazi rasmi ya upinzani sii kupinga tuu, bali ni kupinga kuonyesha makosa na
kwa hoja mbadala za ukweli na sio kwa hoja za uongo na upotoshaji na kwenye jambo lenye maslahi kwa taifa kama hili la rasilimali madini, Wapinzani, CCM, SerikalI na Watanzania wote tusimame as one tuongee kwa sauti moja.
Wito kwa Wapinzani: Sio kupinga tuu kila kitu, kwenye maslahi ya Taifa tuwe kitu kimoja.
Wito kwa Serikali: Ikubali Kusisitiza hoja za msingi za upinzani na kuzifanyia kazi.
Tanzania ni nchi yetu sote, sio Tanzania ya CCM pekee au Tanzania ya serikali ni
Tanzania ya Watanzania wote wakiwemo CCM, serikali, wapinzani na hata akina sisi wenye vyama kimya kimya, let's stand as one.

Jumatatu njema
Paskali
Mnashindwa vipi kukaa na kujadili masuala ya msingi kama kuboresha huduma afya, elimu na upatikanaji wa umeme?

Mnabakia kila kona kushupalia juu ya takwimu za foreign reseve ambazo zimekosewa bahati mbaya. Kwani hamjui kuwa mil 6000 ni sawa na bil 6.

Tumieni busara kujadili masuala ya msingi ili wananchi wa kawaida wawaelewe.
Mkuu Idugunde , naunga mkono hoja. Kiukweli Tanzania, ni kama hatuna. upinzani kabisa, kwasababu hatuna upinzani makini.

P.
 
Wanabodi
Huu ni muswada wa makala ya gazeti.
Nimepata fursa kuendeleza zile makala zangu za "Kwa Maslahi Ya Taifa", ambazo ni makala elimishi katika nyanja za kisiasa, kiuchumi na kijamii kwa lengo la kulisaidia taifa letu lisonge mbele. Makala ya leo inazumzia
kazi ya vyama vya upinzani ni kupinga, lakini sio kupinga tuu kila kitu, kunapotokea jambo kubwa lenye maslahi ya taifa, hapa Watanzania wote tunapaswa kuungana na kuwa kitu kimoja, wakiwemo wapinzani, kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa kwa kuwa wakweli, tusipotoshe bali tulisaidie taifa letu kwa michango ya kujenga na kusaidia, na ikitokea serikali iliyoko madarakani inakosea katika jambo la maslahi kwa taifa, serikali inakosolewa constructively kwa kupewa mapendekezo mbadala na sio kwa kubezwa, kutukanwa na kusakamwa.

Rais Magufuli na serikali yake ya awamu ya tano alipoingia tuu madarakani, alitangaza vita nyingi nyingi ikiwemo vita ya dhidi ya rushwa, ufisadi na ubadhirifu kwa tumbua tumbua. Vita dhidi ya ujinga kwa kutoa elimu bure, kuongeza mikopo ya elimu ya juu na kujenga mashule na kuongeza waalimu. Vita dhidi ya maradhi kwa kuongeza bajeti ya afya, kujenga vituo vya afya, zahanati, mahospitali, upatikanaji na usambazaji wa madawa na kuongeza watumishi wa afya. Vita dhidi ya uvivu na uzururaji kwa falsafa yake ya hapa kazi tuu kwa kusisitiza kila mtu afanye kazi. Hata tangazo la kupiga marufuku mikutano ya siasa na maandamano, lengo lake ni zuri, uchaguzi umepita, watu wasikalie tuu kupiga siasa na uzururaji wa maandamano na badala yake watu wafanye kazi.

Kati ya vita zote ambazo Rais Magufuli na serikali yake ameitangaza, vita ngumu ni vita ya kiuchumi ili kupambana na adui umasikini, hii ndio vita kubwa zaidi na ngumu zaidi kuliko vita zote. Rais Magufuli ameigawanya vita hii katika maeneo tofauti tofauti ikiwemo, kujenga Tanzania ya Viwanda, kujenga miondombinu wezeshi, ndio maana tunashuhudia ndege za ATCL zinapaa duniani kote, meli zinajengwa, miradi mikubwa ya reli ya SGR, mabarabara, flyovers, umeme wa Stigler nakadhalika.

Hitimisho.
Kuwa Upinzani basic kazi yake iwe ni kupinga tuu kila kitu, kiwe kizuri kiwe kibaya wao ni kupinga tuu. Kazi rasmi ya upinzani sii kupinga tuu, bali ni kupinga kuonyesha makosa na
kwa hoja mbadala za ukweli na sio kwa hoja za uongo na upotoshaji na kwenye jambo lenye maslahi kwa taifa kama hili la rasilimali madini, Wapinzani, CCM, SerikalI na Watanzania wote tusimame as one tuongee kwa sauti moja.
Wito kwa Wapinzani: Sio kupinga tuu kila kitu, kwenye maslahi ya Taifa tuwe kitu kimoja.
Wito kwa Serikali: Ikubali Kusisitiza hoja za msingi za upinzani na kuzifanyia kazi.
Tanzania ni nchi yetu sote, sio Tanzania ya CCM pekee au Tanzania ya serikali ni
Tanzania ya Watanzania wote wakiwemo CCM, serikali, wapinzani na hata akina sisi wenye vyama kimya kimya, let's stand as one.

Jumatatu njema
Paskali
Umoja unaanza pale tu watawala wakianza kuheshimu nakutambua mchango wa wapinzani huwezi kujiona upo sahihi katika kila kitu na ukataka uungwe mkono na kudhani ndio uzalendo haiwezekani kabisa mfanane maono na mawazo katika kujenga nchi ndio mana leo hii kama kweli watu wangekuwa wanatumia akili na sio mkumbo wasingeruhusu aliyofanya Bashite au wabunge 19 waliofukuzwa ana chama chao kuwepo bungeni sasa kila mtu ashinde mechi zake tu
 
Wanabodi,

Hitimisho
Kuwa Upinzani basic kazi yake iwe ni kupinga tuu kila kitu, kiwe kizuri kiwe kibaya wao ni kupinga tuu. Kazi rasmi ya upinzani sii kupinga tuu, bali ni kupinga kuonyesha makosa na kwa hoja mbadala za ukweli na sio kwa hoja za uongo na upotoshaji na kwenye jambo lenye maslahi kwa taifa kama hili la rasilimali madini, Wapinzani, CCM, SerikalI na Watanzania wote tusimame as one tuongee lugha moja kwa sauti moja.

Wito kwa Wapinzani: Sio kupinga tuu kila kitu, kwenye maslahi ya Taifa tuwe kitu kimoja. Wito kwa Serikali: Ikubali Kusisitiza hoja za msingi za upinzani na kuzifanyia kazi. Tanzania ni nchi yetu sote, sio Tanzania ya CCM pekee au Tanzania ya serikali ni Tanzania ya Watanzania wote wakiwemo CCM, serikali, wapinzani na hata akina sisi wenye vyama kimya kimya, let's stand as one.

Jumatatu njema
Paskali
Kuna watu wanaoenda kupinga kila kitu kwao. Kwao ni ule utamaduni wa kulalama tu na wanapata shida kumpongeza vilevile hawawezi kupongeza Rais hata kama kafanya mazuri.
Mkuu Kamundu , hii no hoja ya msingi sana!. Naunga mkono hoja
P
 
Japo kazi ya CCM ni kumsifia sifia tu, lakini sio kusifia Kila kitu , kwenye maslahi ya TAIFA tutangulize U-UTAIFA , tuwe wamoja , wakweli na tusipotoshe na tuachane na tabia za UCHAWAISM.
 
Wanabodi,

Huu ni muswada wa makala ya gazeti.

Nimepata fursa kuendeleza zile makala zangu za "Kwa Maslahi Ya Taifa", ambazo ni makala elimishi katika nyanja za kisiasa, kiuchumi na kijamii kwa lengo la kulisaidia taifa letu lisonge mbele. Makala ya leo inazungumzia
kazi ya vyama vya upinzani ni kupinga, lakini sio kupinga tuu kila kitu, kunapotokea jambo kubwa lenye maslahi ya taifa, hapa Watanzania wote tunapaswa kuungana na kuwa kitu kimoja, wakiwemo wapinzani, kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa kwa kuwa wakweli, tusipotoshe bali tulisaidie taifa letu kwa michango ya kujenga na kusaidia, na ikitokea serikali iliyoko madarakani inakosea katika jambo la maslahi kwa taifa, serikali inakosolewa constructively kwa kupewa mapendekezo mbadala na sio kwa kubezwa, kutukanwa na kusakamwa.

Hitimisho
Kuwa Upinzani basic kazi yake isiwe ni kupinga tuu kila kitu, kiwe kizuri kiwe kibaya wao ni kupinga tuu. Kazi rasmi ya upinzani sii kupinga tuu, bali ni kupinga kuonyesha makosa na kwa hoja mbadala za ukweli na sio kwa hoja za uongo na upotoshaji na kwenye jambo lenye maslahi kwa taifa kama hili la rasilimali madini, Wapinzani, CCM, SerikalI na Watanzania wote tusimame as one tuongee lugha moja kwa sauti moja.

Wito kwa Wapinzani: Sio kupinga tuu kila kitu, kwenye maslahi ya Taifa tuwe kitu kimoja. Wito kwa Serikali: Ikubali Kusikiliza hoja za msingi za upinzani na kuzifanyia kazi. Tanzania ni nchi yetu sote, sio Tanzania ya CCM pekee au Tanzania ya serikali ni Tanzania ya Watanzania wote wakiwemo CCM, serikali, wapinzani na hata akina sisi wenye vyama kimya kimya, let's stand as one.

Jumatatu njema
Paskali
Nimenote kwenye hili la mafuriko na maporomoko Katesh, japo Chadema kama chama, CHADEMA yatuma salamu za rambirambi kufuatia mafuriko makubwa yaliyosababisha maafa huko Hanang lakini viongozi wake huku mitandaoni ni ukosoaji la lawama kwa kwenda mbele
kwa kukosoa kila kinachofanyika!. CHADEMA, watu wa Hanang wanahitaji misaada sio lawama zenu
Akufaae kwa dhiki ndio rafiki wa kweli.

Baada ya matatizo yaliyowakumba ndugu zetu wa Hanang tumeona CHADEMA wakitumia muda mwingi kuishambulia na kuikosoa serikali namna inavyodili na crisis ya mafuriko.

Watu wa Hanang wanahitaji misaada sana kuliko kelele ambazo haziwaongezei lolote.

Hawahitaji magorofa wala mavitu makubwa wanataka wapate chakula maji mavazi vikinga baridi na sehemu za kujihifadhi.

Kama ambavyo uwa mnakuwa wepesi viongozi wenu wa kitaifa wakiwa kwenye kesi mnachangishana basi changishaneni hata viroba vya sukari au mashuka mpeleke kwenye majanga achaneni na kelele tupu haziwasaidii waanga.

Punguzeni janja janja watu wa huko wanauhitaji !
Mkuu sinza pazuri,
Naunga mkono hoja, kwenye majanga ya Kitaifa, lets stand united as one, kushikana mikono kusaidia!.

Kwenye majanga ya Kitaifa kama hili la Katesh, let's stand as one, tushikane mikono kusaidia!.
P
 
5
Wanabodi,

Huu ni muswada wa makala ya gazeti.

Nimepata fursa kuendeleza zile makala zangu za "Kwa Maslahi Ya Taifa", ambazo ni makala elimishi katika nyanja za kisiasa, kiuchumi na kijamii kwa lengo la kulisaidia taifa letu lisonge mbele. Makala ya leo inazungumzia
kazi ya vyama vya upinzani ni kupinga, lakini sio kupinga tuu kila kitu, kunapotokea jambo kubwa lenye maslahi ya taifa, hapa Watanzania wote tunapaswa kuungana na kuwa kitu kimoja, wakiwemo wapinzani, kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa kwa kuwa wakweli, tusipotoshe bali tulisaidie taifa letu kwa michango ya kujenga na kusaidia, na ikitokea serikali iliyoko madarakani inakosea katika jambo la maslahi kwa taifa, serikali inakosolewa constructively kwa kupewa mapendekezo mbadala na sio kwa kubezwa, kutukanwa na kusakamwa.

Rais Magufuli na serikali yake ya awamu ya tano alipoingia tuu madarakani, alitangaza vita nyingi nyingi ikiwemo vita ya dhidi ya rushwa, ufisadi na ubadhirifu kwa tumbua tumbua. Vita dhidi ya ujinga kwa kutoa elimu bure, kuongeza mikopo ya elimu ya juu na kujenga mashule na kuongeza waalimu. Vita dhidi ya maradhi kwa kuongeza bajeti ya afya, kujenga vituo vya afya, zahanati, mahospitali, upatikanaji na usambazaji wa madawa na kuongeza watumishi wa afya. Vita dhidi ya uvivu na uzururaji kwa falsafa yake ya hapa kazi tuu kwa kusisitiza kila mtu afanye kazi. Hata tangazo la kupiga marufuku mikutano ya siasa na maandamano, lengo lake ni zuri, uchaguzi umepita, watu wasikalie tuu kupiga siasa na uzururaji wa maandamano na badala yake watu wafanye kazi.

Kati ya vita zote ambazo Rais Magufuli na serikali yake ameitangaza, vita ngumu ni vita ya kiuchumi ili kupambana na adui umasikini, hii ndio vita kubwa zaidi na ngumu zaidi kuliko vita zote. Rais Magufuli ameigawanya vita hii katika maeneo tofauti tofauti ikiwemo, kujenga Tanzania ya Viwanda, kujenga miondombinu wezeshi, ndio maana tunashuhudia ndege za ATCL zinapaa duniani kote, meli zinajengwa, miradi mikubwa ya reli ya SGR, mabarabara, flyovers, umeme wa Stigler nakadhalika.

Hitimisho
Kuwa Upinzani basic kazi yake iwe ni kupinga tuu kila kitu, kiwe kizuri kiwe kibaya wao ni kupinga tuu. Kazi rasmi ya upinzani sii kupinga tuu, bali ni kupinga kuonyesha makosa na kwa hoja mbadala za ukweli na sio kwa hoja za uongo na upotoshaji na kwenye jambo lenye maslahi kwa taifa kama hili la rasilimali madini, Wapinzani, CCM, SerikalI na Watanzania wote tusimame as one tuongee lugha moja kwa sauti moja.

Wito kwa Wapinzani: Sio kupinga tuu kila kitu, kwenye maslahi ya Taifa tuwe kitu kimoja. Wito kwa Serikali: Ikubali Kusikiliza hoja za msingi za upinzani na kuzifanyia kazi. Tanzania ni nchi yetu sote, sio Tanzania ya CCM pekee au Tanzania ya serikali ni Tanzania ya Watanzania wote wakiwemo CCM, serikali, wapinzani na hata akina sisi wenye vyama kimya kimya, let's stand as one.

Jumatatu njema
Paskali
5y

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom