Wakiongea katika kipindi cha Jambo Tanzania cha TBC1 leo asubuhi, J.Makamba kama m/kiti wa kamati ya bunge ya nishati na madini na Mnyika kama waziri kivuli wa nishati, wamependekeza ni lazima maamuzi magumu yafanyike ili kuwezesha mitambo ya Dowans kuwashwa ili kupunguza makali ya mgao.
Kwa mujibu wa Makamba, mitambo ya dowans inazalisha MW 120 na itasaidia kupunguza makali ya mgao kwa 60-70%.Wote wametambua uwepo wa swala la dowans mahakamani.
Mnyika: Mnyika amependekeza sheria ya uhujumu uchumi itumike katka swala la dowans. Huku akisema kuwa hawezi kwenda deep zaidi, Mniyka alimaanisha kuwa mitambo ya Dowans inapaswa kutaifishwa sbb ya ukweli kuwa mkataba wa dowans/richmond ni wa kitapeli na huwezi kuwa na mgao wakati mitambo iko pale imezimwa.
Makamba: Makamba emependekeza kuwa usainiwe mkataba wa muda mfupi (hata wa miezi 3) na hao wenye mitambo ili kuwezeshwa mitambo kuwashwa maana kama hakutakuwa na mvua, basi Mtera itazimwa by March. Amependekeza uangaliwe utaratibu ambao hauta athiri kesi iliyopo
Wote wawili Mnyika na Makamba wameonyesha kuwa utakuwa ni uzembe na kichekesho kwa nchi kuingia gizani au kuathiriwa na mgao wakati iko mitambo ambayo imezimwa huku viongozi wa juu wakikaa kimya na kushindwa kuchukua maamuzi magumu.
Wadau hizi hoja mnazionaje?
Haina neno kama kamkataba hako ka miezi 6 katakuwa ni ka bure...kinyume cha hapo nitamuona na Mnyika kesha haribikiwa.
Nauliza haya maswali nikiwa na uchungu; naomba ndugu zangu watanzania munielewe na kunieleza ukweli.
USHAURI:
- Hivi kwa kuendelea kuamini kuwa suluhu la tatizo la umeme ni MITAMBO YA DOWANS (100MW) sisi tuna akili nzuri kweli?
- Hivi watanzania tunajua maana ya dhalura?
- Hivi sisi tunatunza kumbukumbu ya yaliyopita, mbona Idrisa alituaminisha kuwa njia pekee kunusuru taifa ilikuwa kununua hiyo mitambo la sivyo nchi ingeingia gizani! Mitambo haikununuliwa na giza halikuwapo. JE TANESCO WAMEFANYA NINI TOKEA HAPO?
- Kama tuna akili nzuri tunatakiwa tujue kuwa kama mtera na kwingine kukifungwa kwa kukosa mvua, na tukawasha IPTL, Dowans na Songas bado tutakuwa na mgao mkubwa sana
- Hivi ni kazi ya wabunge kuamua mikakati ya shirika la Tanesco?. Ningependa wabunge wajadili mipango inayopendekezwa na tanesco na si wao kuwaeleza tanesco na wizara wafanye nini!
- Hivi uko mbele ikijulikana kuna matatizo katika huu mkakati wa dharura, je hawa wabunge watawajibishwa na nani?
- Hiyo kamati badala ya kuangaika na kuiamulia Tanesco kukodi mitambo ya Dowans, iwaulize tokea kipindi wamezuiwa kununua mitambo hiyo muda wote walikuwa wanafanya nini mpaka leo tena kuna dhalura?
- Wawaeleze Tanesco hivi; kama tanesco inaamini njia ya kunusulu taifa ni kuwa na mitambo ya 100MW (like dowan) basi wanunue hiyo mitambo wakaenayo standby hapo ubungo!
Naomba kuwasilisha kwa uchungu...........!
Mbwa karudia matapishi yake!Nawapa pole sana vijana hao. Wameshindwa kabisa kuona mbali.Lakini naomba waelewe kwamba kwa kukubali kutumia mitambo hiyo, wameipa Dowans legitimacy.Dawa ni kuisusia kabisa.Tuko tayari kukaa gizani kuliko kuwaangukia mafisadi.Au mafisadi wameshawalainisha?
Ungependa source? Bunge, magazeti..anza na mwananchi..
kwanza aliandika kitabu on Bumbuli, mara akapewa ubunge wa Bumbuli. Alafu akaandika barua kwa waziri wa nishati, mara akapewa uenyekiti wa kamati ya nishati... Huyu mtoto wa Makaamba, mwana wa kaatibu wa chama ambacho RA kakiweka kapuni, je tunaweza kuwa na imani nae?
Na inakuaje wkt bado tuna sakata la tulipe au la, ati tunasema tukodishe au kutaifisha mitambo? Naona mazingaombwe zaidi ya maamuzi ya kisheria au kitaaluma! Umeenda wap uzalendo, wa hiari au kulazmishwa? WAKE UP PEOPLE!?
Wana JF
Rekodi zilizopo zinaonesha Dowans ilikuwa ikizalisha umeme megawati mia kwa kila siku
ule ambao uliingizwa gridi ya taifa na kuuzwa kwa bilioni 1.52 kwa ujumla wake kwa hesabu hii unapotoa gharama za uzalishaji ambazo ni wastani wa sh. milioni 750 kwa siku na bei ya unit moja sh.74.84, kiasi kilichobaki milioni 752 kwa siku inayoingia, na kutoka wataalamu wa hesabu wanena baada ya kutoa milioni 152 ilokuwa ikilipwa kampuni hiyo (Capacity Charge) Serikali kupitia Tanesco ilikuwa ikivuna milioni 600 kwa siku jambo ambalo kamati ya Bunge, Sita wala Mwakyembe wamekuwa na kigugumizi kueleza watanzania ukweli..
Tujadili
As long as anayelipwa ni doawans na ni RA hakuna mtu atakubali ukweli
Mitambo ya Dowans ni ya kutaifisha hakuna haja ya kununua wala kukodisha kwani hata serikali ikununua mitambo ya Dowans bado si suruhisho la kuondoa tatizo la mgao wa umeme, machine zitafanya kazi siku moja mbili watasema zimeharibika na wao wanaendelea kulipwa za bure.
Solution ni kungalia chanzo kingine cha umeme na kuhakisha taratibu za kununua na kuanza kuzalisha tayari utafiti na paper zilishaandikwa na wataalamu kwa vyanzo vifiatavyo
1. umeme kwenye bonde la rufiji (stiglas Gourge) hauitaji mvua)
2. umeme wa makaa ya mawe - Kiwira ipo tayari
3. umeme wa upepo
4. umeme wa mkonge
As long as anayelipwa ni doawans na ni RA hakuna mtu atakubali ukweli