January, Mnyika wapendekeza kutumika kwa mitambo ya Dowans kupunguza mgao wa umeme | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

January, Mnyika wapendekeza kutumika kwa mitambo ya Dowans kupunguza mgao wa umeme

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nicky82, Feb 15, 2011.

 1. Nicky82

  Nicky82 JF-Expert Member

  #1
  Feb 15, 2011
  Joined: Mar 14, 2009
  Messages: 939
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wakiongea katika kipindi cha Jambo Tanzania cha TBC1 leo asubuhi, J.Makamba kama m/kiti wa kamati ya bunge ya nishati na madini na Mnyika kama waziri kivuli wa nishati, wamependekeza ni lazima maamuzi magumu yafanyike ili kuwezesha mitambo ya Dowans kuwashwa ili kupunguza makali ya mgao.

  Kwa mujibu wa Makamba, mitambo ya dowans inazalisha MW 120 na itasaidia kupunguza makali ya mgao kwa 60-70%.Wote wametambua uwepo wa swala la dowans mahakamani.

  Mnyika: Mnyika amependekeza sheria ya uhujumu uchumi itumike katka swala la dowans. Huku akisema kuwa hawezi kwenda deep zaidi, Mniyka alimaanisha kuwa mitambo ya Dowans inapaswa kutaifishwa sbb ya ukweli kuwa mkataba wa dowans/richmond ni wa kitapeli na huwezi kuwa na mgao wakati mitambo iko pale imezimwa.

  Makamba: Makamba emependekeza kuwa usainiwe mkataba wa muda mfupi (hata wa miezi 3) na hao wenye mitambo ili kuwezeshwa mitambo kuwashwa maana kama hakutakuwa na mvua, basi Mtera itazimwa by March. Amependekeza uangaliwe utaratibu ambao hauta athiri kesi iliyopo

  Wote wawili Mnyika na Makamba wameonyesha kuwa utakuwa ni uzembe na kichekesho kwa nchi kuingia gizani au kuathiriwa na mgao wakati iko mitambo ambayo imezimwa huku viongozi wa juu wakikaa kimya na kushindwa kuchukua maamuzi magumu.

  Wadau hizi hoja mnazionaje?
   
 2. L

  LAT JF-Expert Member

  #2
  Feb 15, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  mbona ile mitambo kampuni ya DOWANS walishaiuza kwa kampuni moja ya Cyprus ..... labda hiyo kampuni ya Cyprus waingie nayo mikataba ...yatakuwa yale yale .... richmond kamrithisha dowans mkataba...halafu dowans kauza mitambo kwa kampuni ya Cyprus..je aliyenunua sio tapeli...?
   
 3. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #3
  Feb 15, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  Sidhani kuwa suluhisho la tatizo ni Dowans. Tatizo limekuwepo hata kabla ya matapeli wa Richmond/Dowans hawajaingia nchini.
  Tunajua hujuma mbali mbali zinazofanywa ili kuhalalisha Richmond/Dowans. Hawa watu wana nguvu sana ndani ya serikali. 'Wameiteka '' serikali na vyombo vyake kabisa.
  January Makamba alikuwa na jibu hata kabla ya kwenda mtera. January anaishi Tanzania na alikuwa msaidizi wa Rais, leo hawezi kutudanganya kuwa kwenda Mtera kumemfumbua macho kwa kitu asichokijua.
  Kazi ya serikali ni kutafuta suluhisho la matatizo ya nchi, si kusubiri njama za watu watatu wanaoyumbisha nchi bila sababu. Ni afadhali tuendelee kukaa gizani hadi tutakapopata mbadala, kuliko kuthibitisha utapeli kwa kukubali Dowans. Matapeli hawa wamelelewa na sasa wamefikia mahali wanafanya kile wanachotaka. Mikataba ya miezi 3 au 6 ni kujidhalilisha kuliko kukaa gizani.
  Ina niuma sana kuendelea kutoa ushindi kwa wahujumu na wahalifu hawa.
  January Makamba ahsante kwa ushauri wako uliotumwa, tunajua wewe na mzee wako ni beneficiary wa Mafisadi. Usitudanganye na kututia hasira tukafika mahali pa kufikiria kuazima vitabu kutoka Tunisia au Cairo. Waambie matapeli '' They can fool some people for sometime, they can't fool all people at all time''.
   
 4. BLUE BALAA

  BLUE BALAA JF-Expert Member

  #4
  Feb 15, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 899
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  I hope Makamba na mnyika wametoa ushauri wao kwa serikali katika sura ya kisiasa ila kabla ya kuanza kupress lazima zitafanyika reference za

  1. Procurement acts
  2. Technical consultation
  3. Due dilligence

  Tukumbuke hata Richmond scandal ilitokana na mishandling of fire fighting issues.

  Ushauri - wametoa mchango wao kisiasa na sasa wawaachie watendaji na watalaamu waliangalie hili swala. They should not expect to bring huge changes over the night, Hii ni nchi na siyo shamba la chai kwamba unaingia tu nakuagiza watu wachume chai.
   
 5. mundo

  mundo JF-Expert Member

  #5
  Feb 15, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 200
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi sisi watanzania tumelogwa?!!!!!!! Hii suala la RICHMOND, DOWANS......etc imekuwa too muuuuch.. Hivi kampuni ya mfukoni ambayo ilishambuliwa kiasi hicho.. inauwezo wa kuwa na mitambo ya kuzalisha umeme kiasi hicho....??????
   
 6. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #6
  Feb 15, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Huuu ni ujinga MAKAMBA ni ujinga mkubwa saana, Nilidhani tupo pamoja leo unaleta mambo ya umeme wa DOWANS, hao ni maadui wa nchi hii hatuhitaji tena kuwa na mkataba nao sanasana nikuwafukuza nchini kabisaa, ni bora tukae giza na kutafuta suluhisho la mda mrefu than kuzima mooto tuuu!
  Tumechoka kila mwaka umeme tatizo hakuna suluhisho la mda mrefu?? achieni serikali kama mmeshindwa kazi hivi ni nani anawalazimisha kukaa madarakani wakati kazi imewashinda??
   
 7. b

  boybsema Senior Member

  #7
  Feb 15, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 125
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  to hell, yaani tapeli umemkataa leoo hii unamlamba miguu akusaidie, how comes!!!
  Jamani, suluhisho la nchi kukaa gizani sio mitambo ya dowans hata kidogo,
  wengi wamekwisha ongea siku nyingi, kuhusu
  1. umeme wa upepo
  2. umeme wa makaa ya mawe
  3. umeme wa mkonge
  4. umeme kwenye bonde la rufiji
  5. tununue mitambo yetu wenyewe na sio kukondi mitambo
  ...kwa mantiki hiyo basi hakuna kiongozi hata
  mmoja aliyetingishika kuona mapendekezo yote hayo yanafaa, ila kiaacho kwao ni kuwa na mgao wa umeme ambao utawawezesha kuagiza majenereta kwa ajili ya kuchuuza na kuagiza mitambo kama ya dowans na kuhujumu uchumi wa nchi.
  We are not fools!! this is going to the end, we are fed up! oneday we going to explode like a missile and no one gona believe this!!!
  slowly, slowly it started in Tunisia, then Egypt and now Algeria, what follows is the provoked " peace island, Tanzania" who told you! dont fool us!
  We soon going to the streets to demand our rights and what has been stolen from us,
  we were cool for a long time, but now we will never shut/close our mouth!!!
   
 8. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #8
  Feb 15, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  AKIZUNGUMZA KWENYE KIPINDI CHA TBC ASUBUHI YA LEO,MH MBUNGE WA BUMBULI ALISEMA ANAFURAHI NA ANAAMINI KUMPATA JJ MNYIKA KWENYE KAMATI YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI NI MSAADA MKUBWA NA MNYIKA ATAWASAIDIA SANA KWANI NI KIJANA,MSOMI,MWEREVU NA ANA UWEZO MKUBWA SANA KATIKA KUPAMBANUA MAMBO.

  IKUMBUKWE NI JANA TUU JJ MNYIKA AMETANGAZWA KAMA WAZIRI KIVULI WA WIZARA YA NISHATI NA MADINI NA HIVYI KWA KANUNI ZA BUNGE JJ ANAINGIA MOJA KWA MOJA KWENYE KAMATI YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI AMBAYO MWENYEKITI WAKE NI JANUARI MAKAMBA AKA BARAK OBAMA KAMA ANAVYOPENDA KUITWA .

  vijana tunawategemea sana mlete mabadiliko makubwa ondoeni tofauti zenu za kichama pigeni mzigo
   
 9. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #9
  Feb 15, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  Nilisikia Januari akisema kuwa anaishauri serikali itumie mitambo ya DOWANS hili likoje wadau ni sahihi au la na je Mnyika anaunga mkono hoja hii ya Mwenyekiti wake au?
   
 10. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #10
  Feb 15, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  SINA IMANI NA JM KWANI MTOTO WA NYOKA ANAWEZA KUWA NYOKA MKUBWA zaidi
   
 11. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #11
  Feb 15, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Suala la kutumia mitambo ya Dowans ni kama kujichimbia kaburi tu. Hakuna haja ya kutumia mitambo ya Dowans badala yake wanunue generator za Serikali. Najua si bei ghali kama wanavyotulaghai hawa mafisadi.
   
 12. T

  Tata JF-Expert Member

  #12
  Feb 15, 2011
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,744
  Likes Received: 661
  Trophy Points: 280
  Issue hapa hasa ni nini? Je ni Makamba na Mnyika kuwa kwenye kamati moja? Ni Mnyika kuwa waziri kivuli na hivyo kuingia moja kwa moja kwenye kamati ya nishati na madini? Ni wabunge vijana kuwa kwenye kamati hiyo? Ni wao kuondoa tofauti zao kichama?

  Kwa ufupi haueleweki unachotaka tuchangie hapa.
   
 13. m

  mapambano JF-Expert Member

  #13
  Feb 15, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kila kitu kimekua siasa....nimechoka na hii Richmond na Dowans. Tumefika vipi hapa tulipo lakini??
   
 14. d

  dadyu New Member

  #14
  Feb 15, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mtazamo wangu huyu january makamba ni mmoja wa waliotumwa na mafisadi
  hata lile jimbo amefadhiliwa na huyu jamaa rostam na ni mtu wa karibu wa rostam aziz na nimtu wa karibu wa jakaya kikwete kama vile alivyo ngereja na mpango wa mwaka huu ni kutukamua tuone kwamba shida ya umeme ipo huku tuteseke mpaka mwisho na wao watoe suluhisho kutununulia hiyo mitambo ya rostam ukweli ni kwamba fool the peolpe some time but u cant fool all the people all the time
  tupo tuna elewa kuwa hiyo mitambo GE ni shiling ngapi mtu kama january kapata nafasi ya kubebwa bebwa na wazazi kama dada yake voda kampuni ya rostam na lowasa
  january hawezi kujua kwamba tupo tuliosoma na tuna fanya kazi pamoja na GE kampuni inayotengeneza majenerata hayo.suluhisho la kweli hawa watu waziri na rais wake na kina mzee makamba watuachie nchi yetu ili wale tusio rubuniwa kwa viajira vya akina rostam tutende haki,
   
 15. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #15
  Feb 15, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  mnh.................me siiimo
   
 16. K

  Kipara kikubwa Member

  #16
  Feb 15, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 95
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kwanza naomba nimpongeze January Makamba kwa kuonyesha ukomavu sana ktk kuchambua hoja. Kadhalika Mnyika; Nimeanza na January kwani Mnyika alishasikika sana hadharani tofauti na ndugu Makamba ambaye bahati mbaya watu wengi wamekuwa na negative naye sababu ya baba alivojaribu na kujitahidi kuvuruga CCM pale Lumumba. January km aasimama mwenyewe bado sisi vijana tunaouwezo wa kuibadilisha nchi ikawa vile tunavotaka sisi! Tutambue kuwa wazee wengi hawana muda mrefu, tutashika usukani sisi vijana muda si mrefu ni vema kuwa na mkakati wa pamoja wa kujenga taathira imara yenye vison kwa nchi yetu bila kujali vyama na itikadi. Mi leo nilifurahi kuwaona vijana wale wakijenga hoja si kutupiana lawama na vijembe, wanaonyesha ukomavu, na mi naona ni njia bora kwetu nasi kujua wajibu wetu.

  Baada ya kusema hayo, matatizo ya umeme tuliyonayo ni ya kujitakia na kutowajibika, acha suala la madini ya uranium ambayo mchakato wake unachukua muda mrefu lkn nataja maeneo machache tu ambayo lazima viongozi watueleze kwa nini hakuna jitihada toka uhuru hadi leo kumaliza tatizo la umeme. Singida kule kuna upepo kibao ungezalisha umeme.......Ukitoka Kilimanjaro km unakaribia korogwe pale nadhani tunajua upepo uliopo pale.......Makaa ya mawe ambayo tayari mkoa wa mbeya ulikuwa unapata umeme toka pale haya mambo yapoje.......Kuna pale Lusumo mpakani na Ruanda ambako ni kuweka turbine tu kwani kuna maporomoko natural made ambayo wataalamu wanasema kuwa umeme unaweza zalishwa kulisha east africa yote na kuuzwa. Upepo wamakambako.

  Gasi ya Mnazi bay inadaiwa kuwa kuwa visima zaidi ya vinne ambavyo vimeshakamilika na kila kisima kinauwezo wa kutoa huduma kwa miaka mia kwa nini hawaingizi ktk national grid? Sana sana waliwafrasturate wale jamaa wameondoka na kampuni ya umoja inachechemea, umeme upo kwa maana uzalishaji lakini eti usambazaji tu ni tatizo hii ni aibu

  Songasi nayo vp inaonyesha inawapatia tu ulaji watu lakini hakuna lolote. Hivi sie tumelogwa? Nashindwa kupata takwimu lakini maeneo niliyoyataja ni cake hatungekuwa na tatizo la umeme.

  Juzi nilimsikia ndugu Kagoswe akiuongelea mradi wa Singida, mradi ule ungeshaanza muda mrefu lakini mizengwe ya watu na ukichunguza ni huyu huyu Rostam alitaka awapore project kinamna wakati wao ndo wameinvest muda mrefu kufanya visibility study na hadi kipindi fulani kukawa na ugomvi wa RA na Mwakyembe kuwa naye ana share ktk hiyo kampuni ya uzalishaji umeme ya East Africa. Sawa sisi tunahitaji umeme kama wenye ambao si wazalendo mmetufikisha hapa ngoja tuone sisi wenyewe tunawezaje sasa kujikwamua, kikubwa wasiwe wamepata project kwa mizengwe. Kwa hiyo ndugu wana JF pamoja na kuanzisha mjadala juu ya katiba nadhani tujiorganize tuanzishe mjadala wa namna ya kukabiliana na tatizo la umeme nchini, tuitane wadau wote na serikali na watueleze tunaenda wapi, tutapataje maendeleo bila nishati? Kwa sasa naishia hapa. Lakini nchi hii ni yetu ni sisi wenye wajibu wa kuifanye iweze kuwa mahala salama pa kuishi.
   
 17. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #17
  Feb 15, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145


  Nadhani usemacho ni sawa kabisa ila me nilipenda kujua lini Viongozi wa nchi hii watafika kuelewa na kujitambua wajibu wao ndani ya taifa hili na uwajibikaji, kweli elimu walio ipata inatumika vibaya kuwanyongea kati wananchi kwanini nasema hayo hii mikataba yote ndio imetuleta hapa hawa au hizi tume hazikai kuwaajibisha walio tupoteza na pili inatubidi tu teseke kwanza ndio akili zije na kujua nini cha kufanya kwa hali hii ya kuwa na fire fighting every year we wont come up with intently solution every in this Poor country.

  Na kuondoka katika hii hali ni kufunga mianya yote iliyotuperekea kuwa na janga la kitaifa kwenye umeme tatizo letu kila kukicha twategemea mvua huo ni ufirisikaji wa akiri kwa viongozi washikao nyadhifa ambazo zinaitaji very credible and creative leaders na sio hawa wanatutangulizia si ha sa hapa.

  Reason za kutokuwa na umeme zimekuwa kabbo leo wazili atasingizia Maji hakuna na maji yakiwepo atasema kunahitaji kwa maintenance ya mitambo and its costly huwezi amini as if waha viongozi its very simple hawana strategic future plan?? au ndio wana create mianya ya rushwa na biashara zao?? Imefika wakati wajue haya ether kwa kulazimishwa au kwa kuangalia alama za nyakati

   
 18. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #18
  Feb 15, 2011
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mitambo ya Dowans ni ya kutaifisha hakuna haja ya kununua wala kukodisha kwani hata serikali ikununua mitambo ya Dowans bado si suruhisho la kuondoa tatizo la mgao wa umeme, machine zitafanya kazi siku moja mbili watasema zimeharibika na wao wanaendelea kulipwa za bure.
  Solution ni kungalia chanzo kingine cha umeme na kuhakisha taratibu za kununua na kuanza kuzalisha tayari utafiti na paper zilishaandikwa na wataalamu kwa vyanzo vifiatavyo
  1. umeme kwenye bonde la rufiji (stiglas Gourge) hauitaji mvua)
  2. umeme wa makaa ya mawe - Kiwira ipo tayari
  3. umeme wa upepo
  4. umeme wa mkonge
   
 19. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #19
  Feb 15, 2011
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Ni uamuzi wa busara, bora tupate umeme. Hii adha sasa basi jamani.
   
 20. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #20
  Feb 15, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  shetani la Dowans linarudi taratibu?hahahaha
  kweli hii sasa laana!!
   
Loading...