January Makamba ndani ya shule ya msingi Ngongongare kule Ngurudoto.

Naytsory

JF-Expert Member
Nov 3, 2011
2,192
791
Wakuu inasemekana leo kuanzia saa kumi jioni kutakuwa na kikao cha ndani cha ccm kitakachofanyika katika madarasa ya shule ya msingi Ngongongare na katika kikao hicho atakuwepo January Makamba na Viongozi wengine wa chama ambao bado sijapata majina yao. Ikiwa kuna mtu aliye karibu na shule hiyo atufahamishe
kitakachoongelewa, binafsi kuna rafiki atahudhuria atakapotoka nitawapasha, lakini kama kuna aliyeko kwenye hicho kikao anaweza kutupa kinachoendelea on time.
 
Mi nilidhani Januari Makamba anaenda kumtafutia mwanae nafasi darasa la kwanza mahali hapo kumbe mambo bado ni yale yale ya kuminyia jicho nafasi ya Nassari hapo Arumeru?

Safari hii mipango ya wizi wa kura haitovumilika kamwe.
 
Huyu January Makamba kama atapelekwa Makumira University anaweza kubadilisha upepo wa kisiasa Arumeru Mashariki, kwani anaongea lugha wanayoielewa YOUNG VOTERS. January ni Mtaji kwa CCM na Mwiba kwa CDM as far as young voters are concerned.
 
Vipi ameenda kuendeleza siasa za kifalme! maana yeye pia ni beneficiary wa uongozi wa kurithishana!
 
Ikumbukwe ata Igunga awa Jamaa walikwenda mwishomwisho. Awa ndiyo wanaosuka mpango mzima wa wizi wa kura.
 
Na hiyo itakua ni DOSARI YA KUDUMU katika CV ya Makamba kisiasa mbele ya WaTanzania endapo atathibitisha kwa mara nyingine kwamba hana heshima kuacha demokrasia ifanye kazi yake bila kuingiliwa.

Sote tunakumbuka taarifa aliyotoa kwenye vyombo vya habari siku chache kabla ya uchaguzi Igunga kuhusu madai hewa kwamba CHADEMA wanaleta vijana kutoka Mara kuja kuleta vurugu na kwamba hilo CCM ITAJIBU MAPIGO; kilichofuata ilikua ni damu kila mahali ya wafuasi wa CDM wenyeji wa Igunga.

Hadi hivi sasa watoto wamebaki yatima kutokana na kauli zisizo na umakini kama hiyo aliyotoa Makamba; damu ya WaTanzania bado inaendelea kumlilia na wala hatutopenda kuliona hili likijirudia Arumeru.

The World is watching the situation very closely now than ever, and that's a fact anyway!!!!!!

Ikumbukwe ata Igunga awa Jamaa walikwenda mwishomwisho. Awa ndiyo wanaosuka mpango mzima wa wizi wa kura.
 
Huyu January Makamba kama atapelekwa Makumira University anaweza kubadilisha upepo wa kisiasa Arumeru Mashariki, kwani anaongea lugha wanayoielewa YOUNG VOTERS. January ni Mtaji kwa CCM na Mwiba kwa CDM as far as young voters are concerned.
Kwani kwa sasa upepo unaelekea wapi.
 
Huyu January Makamba kama atapelekwa Makumira University anaweza kubadilisha upepo wa kisiasa Arumeru Mashariki, kwani anaongea lugha wanayoielewa YOUNG VOTERS. January ni Mtaji kwa CCM na Mwiba kwa CDM as far as young voters are concerned.

Hivi wasomi wa Chuo Kikuu nao wanategemea kuamriwa na mtu mwingine juu ya mtu wa kumpigia kura?. Sifa ya wasomi ni uwezo wa kupima hoja za wagombea na sera za vyama vyao na kamwe sio kufuata msimamo wa mtu eti kwa sababu anaongea lugha ya 'young voters'!!
 
Jifariji..
 
Nani kasema wasomi wa chuo kikuu wanategemea kuamriwa na mtu kupiga kura?

Au huko kwenu maneno KUAMRIWA na KUSHAWISHIWA yana maana MOJA?
 
Nani kasema wasomi wa chuo kikuu wanategemea kuamriwa na mtu kupiga kura?

Au huko kwenu maneno KUAMRIWA na KUSHAWISHIWA yana maana MOJA?

Natumaini ujumbe umefika! hivyo vingine ni rahaja tu za kiswahili zisikupe tabu!
 
naomba tuungane wtz wote kuukana utawala huu naona wamempeleka prince mwingine huko arumeru
 
Siyo tetesi ni kweli na mpaka sasa kikao kinaendelea wako katika chumba cha darasa ila kupata kinachozumzwa ndiyo ngumu. Green gurd wako wengi wamezagaa nje. Kuna magari kama 6 yamepaki nje ya darasa.
 
Back
Top Bottom