January Makamba: Mzee anieleza siri juu ya mzee Nnauye, mzazi wa Nape

Ile hotuba kali ya Nape bungeni dhidi ya gesi huko kusini inawafanya kuweweseka,hapo anatafuta cheo kwa kuonyesha Nape ni mfitini kwa serikali na watu kama baba yake mzee Nnauye.
Sad!
Kutokana na tafsiri yako au makamba mwenyewe?
 
Kila mtu anatoa tafsiri ya kwake. Tafsiri ya nani itakuwa sahihi?
 
Kila mtu anatoa tafsiri ya kwake. Tafsiri ya nani itakuwa sahihi?
Mzee alishtakiwa kuiba nyama (ng'ombe) kwenye sherehe, kesi ikafanyika waliohudhuria kwenye sherehe mmojawapo akaulizwa ubwabwa ulikuwa mkavu au ulikuwa na nyama? akajibu ulikuwa na nyama, kesi ikaisha walioshtaki wakashushuka .Nilikuwa nashangaa sana mwanafunzi anarisiti masoma yote na la kiswahili ss nimeamini.
 
Mmh!! Kwaiyo nilifeli kiswahili?

Ila asante kwa kudadavua mkuu.
 

Tafsiri hiyo yako WEWE!

January Makamba na baba yake ni hard core establishment henchmen, wanaokitetea chama dhidi ya Nape Nnauye anaekishambulia chama kwamba miradi kama Stieglers na ndege za ATC ni miundombinu mchepuko mbali na ilani ya uchaguzi.

Henchmen wa kisiasa au wa magenge ya mafioso hutumika kwa kazi chafu, hapa familia ya Nape inachafuliwa kwamba Moses Mnauye, ambae alikuwa kiongozi mzito chamani alihusika kumuonea na kumfukuza Yusuph Makamba mpaka siku aliyoulizwa, wewe mgeni wa heshima wa chama mlionifukuza, acha fitina, nyama ulikula hukula?
 
Pitia ujumbe wa Makamba anaosema kaupata alivyoenda kijijini kumuona mzee Makamba

January , hekima ya wazee kama Makamba ndiyo inayopooza munkari ya vijana.
Mshukuru Mungu sana hata sisi wazee wetu waliyapitia hayo katika utumishi wa serikali.
Mimi mzee wangu pia alipitia mapito hayo, na alinieleza kisa mfano kama huo huo nilipoonewa vibaya na wakubwa sana serikalini.
Bahati mbaya Mungu alishamchukua baba yangu.
Lakini nilichokiona ni kwamba aliyenionea alikuja pata matatizo makubwa mno, kiasi cha yeye kufikia ukomo wa maisha.
Kisasi si chetu, ni cha Mwenyezi Mungu.
 
Mmmh.. Swali hilo kuwa kama ndio utetezi siukubali, labda Mwalimu alimuonea huruma kwa jinsi alikuwa amechoka na kumrudisha CCM kazini
 
Mmekazania kujadili ubwabwa na nyama, badala ya kuangalia kiini kilichomo ndani ya ujumbe. Mmekazania tu, nyama, nyama, ubwabwa, ubwabwa. Acheni kukurupuka, someni taratibu na kwa makini ili mpate ujumbe. Mnajadili mada utadhani kama watoto wa darasa la kwanza. Ebo!!
 

Yaani wewe ndiyo bure kabisa. Unajadili mada utadhani graduate wa shule za "ngumbaru".

Ngumbaru ni elimu ya watu wazima wasiojua kusoma na kuandika miaka ile ya 70 na 80. Wazee wale walikuwa wanasomea chini ya miembe.
 
Mmmh.. Swali hilo kuwa kama ndio utetezi siukubali, labda Mwalimu alimuonea huruma kwa jinsi alikuwa amechoka na kumrudisha CCM kazini
Mkuu pengine hujawahi kuwa na ndugu au wewe mwenyewe kutumikia Taifa katika ngazi za juu.
Huko juu usione watu wanafunga tai na kupelekwa na maV8, ubatili mtupu.

Kuna kitu kinaitwa FITNA!
Na hii wanafanyiana wenyewe kwa wenyewe katika CCM na serikali.
Ukitengenezewa zengwe, kwanza unatolewa wadhifa na waliokutengenezea wanakaba hicho cheo.

Hata ukija jitetea vizuri bado unaweza kutorudi pale ulipokuwa.
Ndivyo nchi incyo kwenda.
FITNA is an official serving unspoken policy.
 
Sasa si inawezekana alinunua nyama kilo 10 buchani kwa ajili ya wageni rasmi na wale ng'ombe na mbuzi akawaswaga kuwapeleka kijijini kwake. Ufisadi ulianza zamani nchi hii!
Kweli kabisa hata vipande vyanyama vikiwa sita wanakula wageni tuu. Ufisadi ccm ni jadi aisee
 
Malipo ni hapa hapa Duniani dhambi ya mzee wake Nape Imelipwa kwa Nape leo ahhh ahh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…