GE2025 January Makamba: Hoja kwamba nautaka Urais hizo ni ramli tu, muda bado upo

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Wont be the same

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,564
Reaction score
2,483
Mbunge wa Jimbo la Bumbuli anayemaliza muda wake, January Yusuph Makamba, amesema amepokea kwa moyo mkunjufu na utulivu maamuzi ya Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya kumuengua kwenye orodha ya wanachama wanaowania kuteuliwa kugombea ubunge katika jimbo hilo kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.

Makamba amezungumza hayo siku ya Jumatano wakati akizungumza na waandishi wa habari wa walioshtukiza na kufika ofisini kwake kwa lengo la kupata kauli yake kuhusu hatua hiyo ya chama.

“Ninaipokea na kuitii kwa moyo mmoja uamuzi wa Kamati Kuu. Mimi ni mwanachama na kiongozi mtiifu wa Chama Cha Mapinduzi. Chama kina taratibu zake, na wajibu wangu ni kutii maamuzi ya vikao vyake,” amesema Makamba.

Ameeleza kuwa ameshawasiliana rasmi na uongozi wa CCM ngazi ya wilaya na kuwaarifu utayari wake wa kushirikiana nao pamoja na wanachama wengine kuhakikisha chama kinashinda kwa kishindo katika uchaguzi huo.

Akizungumzia taarifa zinazosambaa mitandaoni na kwenye baadhi ya vyombo vya habari kwamba sababu ya yeye kukatwa ni kutokana na madai kuwa anadaiwa kuwa na nia ya kugombea urais wa Tanzania, Makamba amekanusha vikali madai hayo, akisisitiza kuwa hana nia hiyo kwa sasa na kwamba hajawahi kuonesha dhamira hiyo.

“Mimi si mgombea wa urais, wala sijawahi kutangaza nia hiyo. Hayo ni maneno yanayozunguka kwenye medani za siasa. Kwenye siasa changamoto kama hizi ni za kawaida, na mimi niko tayari kuzipokea kwa heshima na utulivu,” amesema.

Kuhusu tetesi zinazodai kuwa huenda akahama chama kutokana na kukatwa katika mchakato huo, Makamba amekanusha uvumi huo akisema bado yupo ndani ya CCM na kwamba chama hicho bado kinabeba imani na maono yake ya kisiasa.

“Niko CCM, na niko sana. Chama hiki ndicho kilichonilea, kimenipa nafasi za kuwatumikia wananchi na bado naamini katika misingi yake. Sio kila changamoto ni sababu ya mtu kuhamahama,” amesisitiza.

Makamba aliwahi kuwa mbunge wa Bumbuli kwa vipindi vitatu na kushika nyadhifa mbalimbali serikalini, ikiwa ni pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira, Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki na Waziri wa Nishati

Source Jambo TV
 
Mbunge wa Jimbo la Bumbuli anayemaliza muda wake, January Yusuph Makamba, amesema amepokea kwa moyo mkunjufu uamuzi ya Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya kumuengua kwenye orodha ya wanachama wanaowania kuteuliwa kugombea ubunge katika jimbo hilo kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.

Ameyasema hayo leo Jumatano Julai 30 alipoulizwa na waandishi wa habari kuhusu kutoteuliwa kwake kuwania ubunge wa jimbo hilo mwaka huu.

Chanzo: Jambo TV
 
View attachment 3424846

Source Jambo TV
Kuna chess inachezwa.

Amandla...
 
1. Rais ana wabunge wake.
2.Chambo kwa upinzani.
Huyu ni mtu muhimu mno kwa CCM. Kumuachia kirahisi hivyo kunatia shaka.

Amandla...
 
Mbunge wa Jimbo la Bumbuli anayemaliza muda wake, January Yusuph Makamba, amesema amepokea kwa moyo mkunjufu uamuzi ya Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya kumuengua kwenye orodha ya wanachama wanaowania kuteuliwa kugombea ubunge katika jimbo hilo kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.

Ameyasema hayo leo Jumatano Julai 30 alipoulizwa na waandishi wa habari kuhusu kutoteuliwa kwake kuwania ubunge wa jimbo hilo mwaka huu.

View attachment 3424844

View attachment 3424849
Chanzo: Jambo TV
Well, at least he carried himself like a grown man!
 
Huyu jamaa amejua kujizuia hisia zake

Nafikiri ile exposure ya kufanya kazi na Viongozi tofauti tofauti vimeweza kumjenga

Kila la heri kwenye maisha mengine nje ya Ubunge!
 
Mbunge wa Bumbuli anayemaliza muda wake na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) January Makamba amesema amekubaliana na uamuzi wa kamati kuu ya CCM ya kuondoa jina lake kwenye nafasi ya Ubunge Bumbili.

Makamba ameyasema hayo ikiwa ni siku chache baada ya kamati kuu ya CCM kutangaza majina ya wagombea Ubunge wa majimbo mbalimbali Tanzania huku jina lake likiachwa kwenye mchujo huo wa awali.

“Kwenye CCM Dhana ya kukatwa haipo ni aidha umependekezwa au umeteuliwa, kukatwa maana yakeni kwamba kuna nafasi unastahili ya kwako kwa hiyo umekatwa” January Makamba

“Wakati unapoomba nafasi hizi wote mnakuwa mpo sawa hauistahili kwa hiyo hakuna idea ya kukatwa kwa hiyo ni hukupendekezwa au haukuteuliwa sisi hatukuteuliwa” Makamba
 
Mbunge wa Jimbo la Bumbuli anayemaliza muda wake, January Yusuph Makamba, amesema amepokea kwa moyo mkunjufu na utulivu maamuzi ya Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya kumuengua kwenye orodha ya wanachama wanaowania kuteuliwa kugombea ubunge katika jimbo hilo kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.

Makamba amezungumza hayo siku ya Jumatano wakati akizungumza na waandishi wa habari wa walioshtukiza na kufika ofisini kwake kwa lengo la kupata kauli yake kuhusu hatua hiyo ya chama.

“Ninaipokea na kuitii kwa moyo mmoja uamuzi wa Kamati Kuu. Mimi ni mwanachama na kiongozi mtiifu wa Chama Cha Mapinduzi. Chama kina taratibu zake, na wajibu wangu ni kutii maamuzi ya vikao vyake,” amesema Makamba.

Ameeleza kuwa ameshawasiliana rasmi na uongozi wa CCM ngazi ya wilaya na kuwaarifu utayari wake wa kushirikiana nao pamoja na wanachama wengine kuhakikisha chama kinashinda kwa kishindo katika uchaguzi huo.

Akizungumzia taarifa zinazosambaa mitandaoni na kwenye baadhi ya vyombo vya habari kwamba sababu ya yeye kukatwa ni kutokana na madai kuwa anadaiwa kuwa na nia ya kugombea urais wa Tanzania, Makamba amekanusha vikali madai hayo, akisisitiza kuwa hana nia hiyo kwa sasa na kwamba hajawahi kuonesha dhamira hiyo.

“Mimi si mgombea wa urais, wala sijawahi kutangaza nia hiyo. Hayo ni maneno yanayozunguka kwenye medani za siasa. Kwenye siasa changamoto kama hizi ni za kawaida, na mimi niko tayari kuzipokea kwa heshima na utulivu,” amesema.

Kuhusu tetesi zinazodai kuwa huenda akahama chama kutokana na kukatwa katika mchakato huo, Makamba amekanusha uvumi huo akisema bado yupo ndani ya CCM na kwamba chama hicho bado kinabeba imani na maono yake ya kisiasa.

“Niko CCM, na niko sana. Chama hiki ndicho kilichonilea, kimenipa nafasi za kuwatumikia wananchi na bado naamini katika misingi yake. Sio kila changamoto ni sababu ya mtu kuhamahama,” amesisitiza.

Makamba aliwahi kuwa mbunge wa Bumbuli kwa vipindi vitatu na kushika nyadhifa mbalimbali serikalini, ikiwa ni pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira, Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki na Waziri wa Nishati

View attachment 3424846

Source Jambo TV
Ananyenyekea Ili huku mbeleni ateuliwe kwenye cheo Fulani asife njaa, huo ndo ukweli
 
Back
Top Bottom