January Makamba azomewa na Wanachuo

January Makamba azomewa na Wanachuo

OgwaluMapesa

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2008
Posts
10,942
Reaction score
437
January Makamba azomewa na mamia ya wanafunzi katika uchaguzi wa viongozi wa shirikisho hilo kwenye ukumbi wa Karimjee...

Kama imefikia hatua ya kuzomewa na wanafunzi ni muda mwafaka wa kujitafakari..... Kudoz wanafunzi "uzalendo wenu ndiyo mafanikio ya Taifa".....
 
Hivi makamba anafanya nini kama naibu waziri wa mawasiliano? Mbona makampuni ya simu yamebana sana watumiaji wa mitandao?
 
Pumbavu sana.......analeta siasa za urithi........
 
makamba alichoharibu nikutubania MB's tunashindwa kupakua materials..
 
Makamba anajichafua mapema.asilimia 87 ya wanachuo wanategemea MBS ktk harakati zao za masomo.kama alishindwa kuwatetea kafata nini huko?bora angepigwa kabisa
 
Mbona enzi za nyerere MB hazikuwepo na watu walikuwa wanasoma, tatizo mi wanafunzi ya siku hizi haipendi kusoma kazi kwenda club tu
 
Hahahahaha....nyota hizi bhana...Mr Edo wameandamana hadi kwake wanmtaka kama rais wao....
 
Huyu si ndo yule aliyetangaza kuwania Urais?

Nchi yangu weeeeee..!!! Kikwete ataalaaniwa sana kwa kufanya kiti cha Urais kuwa Rahisi namna hii.

BACK TANGANYIKA
 
nani kashinda uenyekiti,
katibu wa itikadi
mchumi
uhamasishaji
 
Wangemtwanga tofali ingekuwa poa tu!!! Hii mitandao ya Simu inatuibia sana kwenye Data wakati hata kodi hawalipi... CCM wanaangalia matumbo yao tu ...
 
Mbona enzi za nyerere MB hazikuwepo na watu walikuwa wanasoma, tatizo mi wanafunzi ya siku hizi haipendi kusoma kazi kwenda club tu

Mawazo mgando hayo, au bado unataka watu waendelee kuwa na imani za kizamani za kuwaambia watu kuwa ''una tabiri kesho vita itatokea burundi''.
Kawaida tunakwenda mbele, haturudi nyuma
 
Back
Top Bottom