January Makamba ajihami kupitia

Unaunga juhudi za wengine kufukuzwa huku hutaki Makamba kufuzwa, unfair treatment hii na maslahi binafsi nilitegemea kuwa sheria ichukue mkondo wake
 
Wa buddha huwa wanamsemo maarufu husemao:Three things cannot be long hidden.The sun,the moon and the truth.Anaweza kuwa amefanikiwa kulizima hili skendo kwa kumnyamazisha huyo mzungu kwa pesa,lakini hipo siku hili jinamizi litamjia tena.

Mimi binafsi huamini mtu anapokuwa amehudhika au kughadhibika na jambo fulani dhidi ya mtu fulani.Kile kimtokacho mdomoni kwa wakati huo ni ukweli mtupu.Mzungu ameyasema ya moyoni.Na imedhihirika kuna lengo lililomfanya huyu mzungu kuwa karibu na familia ya makamba.Kama makamba alivyokiri kuna madili makubwa na penyo aliloliona kupitia kwake kwa maana ndiyo michezo aliyoizoea kuicheza.

Kumbukeni MYTH IS MUCH MORE IMPORTANT AND TRUE THAN HISTORY.Wale waliosema wakina balile wanaandika stori za kusadikika kwenye gazeti la jamhuri,baadaye walikuja kuumbuka pale Magu aliposema walichoandika ni ukweli.Najua mnampenda January na mko radhi kumtetea kwa maslahi yenu.Hila tukumbuke Taifa ni kubwa kuliko mtu mmoja.
 
Tunataka harakati za ujenzi wa viwanda alivyoahidi ziende sambamba na hiyo safisha safisha vinginevyo ni propanda
mkuu inaonekana unampenda reformation leader Martin Luther enzi za dark ages
 
endeleeni kufukuzana na upepo tu.. Tunaishi kwa kuanzisha matukio ili kuwaondoa kule mliko ili mje huku kisha kule tuendelea
 
Huyu Muitaliano kana anamdai JM kwa nini asiende Mahakamani?
 
Huyu mleta mada inavoonesha atakuwa na uhusiano wa karibu na mh. Makamba. Maana alivotapika kwenye hii thread yake nikama amekunywa pombe uliooza.
 
Nafikiri Mh. Makamba angejitokeza ajitee mwenyewe kuliko hawa ambao naona kama wanazidi kuharibu zaidi
 
Mkuu kikao kimefanyika kwani
 
mioga, mijizi, mikwapuaji. Inaogopa ikijiajiri yenyewe haiwezi kujikwapulia.
 

Wakuu, tupeni feedback za huo mkutano kwa yule atakayezipata. Wengi tunataka kujua zaidi kuhusu "saga" hili.
 
Mkuu wasomi wetu ni majipu, wasoni wetu wapiga dili, wasomi wetu wezi, wasomi wetu waongo wanapenda kuishi unafiki, bora hata mie mkulima wa maharage Na mihogo kuliko hawa wanojiita wasomi

Wanaingia wakiwa safi. Punde kidogo tu, wanakuwa "corrupted" na mfumo wa serikali yao wenyewe.
 
Hongera mkuu, kumbe ni mkurugenzi. Watz 300 wanapata mahitaji kupitia Erythrocyte. Si jambo la kitoto.
 
Dah umezunguka weeeeeeee kumbe lengo kumtetea the makambaz ~~~~mtumishi/kiongozi wa umma haruhusiwi kupokea zawadi inayozidi elfu hamsini (50,000/=). Akifanya hivyo lazima aitaarifu mamlaka.........Tena kanuni imesungumzia zawadi ambayo chanzo chake unaifahamu sembuse midola from unknown source?
 
Utetezi kama huu ndo unatufanya hata wengine ambao bado tunampa benefit of doubt Makamba tuanze kuchoka.Bora kukaa kimya mjipange kwanza mtoe utetezi unaoeleweka vinginevyo hata kama anasingiziwa mnazidi kumchimbia "kaburi"

Ingawa wanasema aliyeleta kashfa hii ni kichaa tusimwamini, lakini nilivyosoma issue yote, nimegundua she is actually very intergent! Hata zile audio alizopost, ameweka kimtego sana, maana ni vipende tu. Hakuna anayejua mwendelezo wake kamili! lakini, hatua yake pia ya kusema she is buying time to allow the victim to talk, ni ya hatari zaidi, na haionyeshi kama huyu binti ni mjinga kama wengi wanavyofikiri.
 

Mkuu umetumia nguvu nyingi kama mtu unayemwandikia hajui wajibu wake na hajui kama ana vyombo vya kumsaidia.
Kwa taarifa yako kabla Rais hajazungusha panga lake, huchukua baadhi ya hatua kujiridhisha, kwa mfano kama issue hii ya JM inaharufu ya rushwa ndani yake maana yake kama JPM anashawishika kwenye maelezo ya awali kuwa huenda kuna Jinai imetendeka atakachofanya ni kuviamuru vyombo vyake vipelelezi na kumpa ukweli juu ya jambo husika. Maana yake vyombo hivyo vitapeleleza na kuchunguza kwa kuwahoji wahusika wazi na kisirisiri, watakusanya vielelezo na kuvipitia, Kisha wataandika taarifa na baadaye watampatia Rais ambaye baada ya kupewa briefing na kuisoma Taarifa bado akijiridhisha kuwa kuna makosa aidha ya Jinai au ya kimaadili atamwaita washauri wake wa masuala ya Utawala, na mshauri wa mambo ya Siasa atazungumza nao juu ya hiyo kadhia. Baada ya kushauriana na hao washauri atamwita mhusika na kumpa nafasi ya kujitetea, akishindwa kujiclear kuna option mbili, aidha apishe au asubili kutumbuliwa.

Sasa unachotaka kutuaminisha ni kuwa Presida akisikia jambo anakimbia kushika mkasi kutumbua bila kuangalia kama ni Jipu, Kovu, Upele au chunusi, yeye ni tumbu tumbua tu. Rais ana mikono Mingi, ana PCCB, Usalama wa Taifa, Jeshi la Polisi (CID), Ofisi ya mwendesha mashtaka wa serikali, ofisi ya mwanasheria Mkuu wa serikali, Ofisi ya Upelelezi wa makosa ya Jinai (DCI), Tume ya maadili kwa watumishi wa Umma, nk una maana vyombo vyote hivi vikisema fulani mchafu vitakuwa vimeshinikizwa na vijimaneno vya Mtandaoni.
 


Amekuwa Mh Rais akituomba tumuombee ili Mwenezi Mungu amjalie hekima na busara katika kututumikia. kamwe hawezi kufanya kwa mitandao ya kijamii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…