January Makamba ahojiwa na Jeshi la Polisi kuhusu sakata la Mo Dewji kutekwa

We
Huwa katika mambo ya saikolojia ni rahisi kueleza kile kilichoko ndani ya moyo wako bila wewe kujua. Ndio maana wanasaikolojia wakikuhoji wataelewa mambo mengi juu yako bila wewe kujua umewaambia nini.

Sasa hii kauli ya Makamba imenishitua sana, "sijakamatwa na Polisi niko salama". Ni jambo la kutisha sana kwamba hata waziri katika serikali ya awamu ya tano anakiri kwamba Mtanzania yeyote akikamatwa na Polisi basi hayuko salama tena! Au kwa namna nyingine, anaashiria Polisi kukufuatilia ni dalili ya kwamba hauko salama!

Lakini kila wakati tunavyoshuhudia mauaji ya raia wakiwa chini ya Polisi basi hatupaswi kushangazwa na kauli ya Makamba.
We mtu, uko vizuri sana. I Iove this argument!
 
Mbona Manara alilala ndani.Kwa nini Makamba aonewe Hurumaa?
Kumlaza Ndani Waziri inahitjka go ahead ya ALIYEMTEUA.

Na Waziri anaitwa na IGP sio na RPC

The case Brigedia General au Major General akiwa na kosa la kiraia, IGP ndio anamwomba aende kituoni baada ya kupata go ahead ya CDF

Hiyo ni Protocol ya Mamlaka

Labda kama awam hii inaamua kukanyaga taratibu tu kwa VIBURI na ULEVI wa Madaraka
 
Kumlaza Ndani Waziri inahitjka go ahead ya ALIYEMTEUA.

Na Waziri anaitwa na IGP sio na RPC

The case Brigedia General au Major General akiwa na kosa la kiraia, IGP ndio anamwomba aende kituoni baada ya kupata go ahead ya CDF

Hiyo ni Protocol ya Mamlaka

Labda kama awam hii inaamua kukanyaga taratibu tu kwa VIBURI na ULEVI wa Madaraka
Asante kwa majibu mazuri.Swali la nyongeza.Je ilikuwa sahihi Manara kukaa Lupango?
 
Kufuatia kutekwa kwa Mo siku za hivi karibu na kupatikana baadae,waziri wa Muungano na Mazingira January Makamba Jana ,aliitwa polisi ili kutoa taarifa zaidi kutekwa kwa Mo.

====

Taarifa za ndani zilizotufikia zinasema kuwa Jeshi la Polisi limemkamata na kumuhoji Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba kwa saa kadhaa mpaka saa mbili za usiku jana Jumapili kujua uhusika wake katika suala la kutekwa kwa MO Dewji.

Jeshi la Polisi limethibitisha kumhoji Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba kuhusu suala la mfanyabiashara Mohammed Dewji ‘Mo’ aliyetekwa Oktoba 11 na kupatikana Oktoba 20, 2018

Kupitia ukurasa wake wa Twitter waziri huyo ameandika, hajakamatwa na polisi na kuwa yupo salama. "Sijakamatwa na polisi. Niko salama. "
January Makamba akitoa ufafanuzi kuhusu kuitwa Polisi amesema...

Polisi walinipigia simu kuniomba, kama rafiki wa @moodewji, niwasaidie kama kuna chochote cha ziada ambacho Mo aliniambia kinachoweza kusaidia uchunguzi. Niliwaeleza. Wakasema kinafanana na alichowaeleza. Wakanishukuru. Wamefanya hivi pia kwa wanafamilia. Sikukamatwa.
Muda wa saa 4:51 AM ya tarehe 20 Oct 2018 Mara ya Dewji kupatikana, Makamba aliandika kwenye mtandao wa Twitter kwamba kaongea na Dewji. "Nimemuona na kuongea kwa kirefu na Mohammed Dewji. Ni mzima wa afya isipokuwa ana alama za kufungwa kamba mikononi na miguuni. Mnamo saa nane usiku, watekaji waliamua kumtupa kwenye maeneo ya viwanja vya Gymkana. Naamini Polisi watatoa taarifa za ziada kuhusu kilichojiri."
Tushaelewa
IMG-20181022-WA0026.jpeg
 
Kwa mujibu wa SAUTI KUBWA, baraza LA mawaziri, na waziri wa aridhi alipewa maelekezo ya kumkabili Mo ili ayaachie hayo maeneo tajwa, Mo aliwadindia akawaambia hayo maeneo nimekopea kwenye mabank huko ughaibuni, jiwe kusika hayo alichanganyikiwa, akaamuru vijana wakamlete Mo...... Itaendelea
Tunasubiri....
 
Hata kwa akili ndogo uliyonayo hujafikiria kwanini MO hakupelekwa polisi kuandikisha maelezo baada ya kupatikana kama alivyofanyiwa Abdul Nondo ?
Nondo alijiteka, akaenda kwa Mpenzi wake, akaoga vizuri.. Kwani Roma aliandikishwa maelezo?
 
Mh. Waziri hapa alitakiwa aseme hivi: "SIJAKAMATWA NA POLISI, NIKO HURU". Actually inapotokea kuwa uko mikononi mwa Polisi bila kujali wewe ni mhalifu ama la, unakuwa uko salama zaidi, assumming hukuwa umeanzisha vita ya kupingana nao kabla hawajakutia mikononi. Mimi kwa mfano mwaka 2010 niliwahi kukaa lock-up kwa muda wa siku (3) tatu pale Polisi Mafinga, na lock-up hiyo ilikuwa ni ya usalama zaidi kwangu kuliko kama ningekaa nje sehemu nyingine yeyote ile tofauti na kituo cha Polisi. Hata hivyo SIKUWA MHALIFU, lakini still, niliwashukuru mno polisi kwa kuniweka lock-up! Kwa hiyo si kila tukio linalopelekea polisi kumshikilia mtu ni la hatari!
We ndo nani mpaka umpangie cha kusema? Na kama anamaanisha alichosema? Wangapi wamefia mikononi mwa polisi?
 
Back
Top Bottom