VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Bumbuli ni Jimbo linaloongowa na Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia,Januari Makamba. CCM kindakindaki. Kada wa uhakika aliyepikwa akapikika. Akakabidhiwa Bumbuli ili aiongoze kama Mbunge. Lilikuwa Jimbo jipya lililohitaji Mbunge mpya. Bumbuli ikampata Januari Yusuph Makamba.
Bumbuli ina maumivu makali ya kimaendeleo. Haina miundombinu ya uhakika kama barabara. Barabara hazipitiki kwa tabasamu hasa wakati wa mvua. Zikiwa kwenye miinuko na kona,hazina hata changarawe. Zinateleza na kuogofya.
Masoko ya uhakika ya mazao. Mazao huzagaa hadi kuoza. Mbunge yuko Dar anaitumikia nchi. Maji safi na salama yapo kwa uchache na kwa wenye nazo. Wengi wanakunywa maji hatarishi na ya kujitoa mhanga.
Kuonana na Mbunge ni kwa njia ya facebook,twitter na instagram. Wanabumbuli wengi humuona Mbunge wao luningani tu. Maendeleo ya wananchi yamesimama. Yamebaki vilevile yakiwa yamepakwa chokaa badala ya rangi.
Taasisi ya Januari Makamba ya Maendeleo ya Bumbuli ipo mitandaoni ikinoga kwelikweli. Ina mipango na mikakati ya uhakika. Kwenye jamii halisi,hakuna kitu. Migogoro ya ardhi inazizima Bumbuli.
Wananchi lakini wanajivuna kuwa na Mbunge Naibu Waziri. Kuwa na Mbunge kijana anayetamani kuongoza nchi. Kwa hayo tu. Pia,kupata misaada ya hapa na pale toka mfuko wa Mbunge/Jimbo. Lakini,hawawezeshwi kujitegemea.
Januari na Bumbuli yake. Januari na Jimbo lake. Januari na wananchi wake. Januari na mikakati yake. Tafadhali wajali wananchi wako kimaendeleo yao ili wawe kielelezo cha kufaa kwako.
Jimboni kwanza!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam